Hatua 4 Za Tendo La Ndoa

hatua nne za tendo la ndoa

Mtu anapofanya tendo la ndoa mwili wake hupitia hatua kadhaa. Mzunguko wa mwitiko wa kimapenzi unaelezea mwitiko wa kimwili na kihisia ambao mtu anapitia baada ya kupata kiamsho (kichocheo) cha kufanya mapenzi. Mzunguko huu una hatua nne ambazo zinaelezea vitu vinavyotokea katika mwili mtu akifanya mapenzi , akiwa peke yake au akiwa na mwenzi. Mada yetu ya leo, kwa hiyo, ni maelezo ya hatua  nne za tendo la ndoa, hatua ambazo zinahusu jinsia zote, wanaume na wanawake.

Watu huzipitia hatua hizi nne kwa namna tofauti, hakuna watu wawili ambao watapata hisia zinazolingana katika hatua hizo nne.

Hatua hizo nne hutokea kama mwitiko wa aina zote za tabia za kufanya mapenzi, ikiwa ni pamoja na kujichua, kutumia mdomo n.k., na ni kwa jinsia zote ingawa watu tofauti watapata mwitiko tofauti kutokana na kichocheo cha mapenzi kimoja kutegemeana na viungo vyake vya uzazi.

Hatua 1: Excitement

Msisimko (sexual excitement or sexual arousal) ni hatua ya kwanza katika mzunguko wa mwitiko wa kimapenzi. Hatua hii ni mwili kuitika baada ya mawazo, kushituliwa, au matukio ambayo yanamfanya mtu kuamshwa kimapenzi.

Mifano ya vitu vinavyoweza kuamsha msisimko wa kimapenzi (sexual stimulation ) ni kutazama picha za ngono, kuwazia mapenzi, au kubusiana.

Katiaka hatua hii ya msisimko mtu anaweza kuona yafuatayo:

. mapigo ya moyo kupanda, kupumua kwa haraka, na pressure ya damu
. misuli kukaza
. kuongezeka kwa mtiririko wa damu kuelekea viungo vya uzazi
. kuongezeka kwa usikvu wa kuguswa
. chuchu kuwa ngumu
. uume kusimama
. uke kuanza kulowana
. korodani kuwa kubwa na mfuko wa korodani kukaza.

Hatua 2: Plateau

Kama mtu atazidi kupata kichocheo cha mapenzi baada ya hatua ya kusisimuliwa, ataingia kwenye hatua ya pili: plateau.

Katika hatua hii ya pili, mwitiko ulianzisha msisimko wa kimapenzi huongezeka. Mtiririko wa damu, kasi ya moyo, misuli kukaza, upumuaji, na usikivu wa ngozi vyote huongezeka.

Mwanamke ataona:

. kuta za uke kuwa nyeusi, uke kutanuka
. Usikivu wa kinembe kuongezeka
. uke kuzidi kuwa laini

Mwanamme anaweza kutoa majimaji ya mwanzo (pre-seminal fluid), hali amabayo pia huitwa pre-ejaculate au pre-cum. na pia anaweza kuona mfuko wa korodani kupanda zaidi.

Hatua hii huishia pale hatua ya tatu, orgasm, inapoanza.

Hatua 3: Orgasm

Hatua hii ya orgasm hufikiwa mtu anapokuwa kwenye kilele cha msisimko. Hatua hii huitwa pia “climax.”

Hatua hii hufikiwa endapo mtu ataendelea kupata kichocheo cha mapenzi baada ya hatua ya plateau. Vichocheo vinavyoweza kusababisha kufika mshindo (orgasm) ni pamoja na kujishika kwenye viungo vya uzazi, matiti, chuchu, na sehemu nyingine za mwili.

Lakini, si lazima kwamba watu wote wanafikia hatua hii.

Dalili za kufika mshindo ni pamoja na kukaza kwa misuli, kusikia wingi wa raha, na kujisikia kama kuna mzigo umeutua.

Mwanamme anaweza kusikia kukaza kwa misuli ya uume na kukojoa shahawa, ambay=ko ni kutoa manii kupitia njia ya mkojo.

Mwanamke atasikia kukaza kwa misuli kwenye uvungu wa mifupanyongana misuli kulegea.

Pamoja na mabadiliko haya katika kwenye maumbile, ubongo hutoa kemikali iitwayo oxytocin, ambayo hukufanya ujisike vizuri na kukufanya uongeze ukaribu na mwenza.

Ubongo pia hutoa dopamine ambayo huufanya mwili kulegea baada ya tendo la ndoa.

Jee, Mwanamke hukojoa?

Wanawake wanaweza kukojoa kupitia njia ya mkojo (urethra). Wanasayansi wanaamini kuwa majimaji (ejaculate) huweza kutunzwa ndani ya kibofu cha mkojo na wanawake wengine huweza kuyatoa (kukojoa) wakati wakisisimuliwa kimapenzi au wakifika mshindo.

Si wanawake wote wanaokojoa. Wakati mwingine majimaji hayo hubaki ndani ya kibofu cha mkojo na kutolewa nje pamoja na mkojo.

Kuna aina mbili za majimaji yanayotolewa na mwanamke:

Ejaculate fluid

Aina hii inafanana na manii ya mwanamme. Ni nzito na yenye rangi ya maziwa. Tezi za paraurethral hutengeneza majimaji haya. Majina mengine ya tezi hizi ni Skene’s glands, Garter’s duct, na female prostate.

Uchunguzi umebaini kuwa majimaji haya yana prostatic acid phosphate (PSA). PSA ni kimeng’enya kilichomo ndani ya manii ya mwAnamme na husaidia utembeaji wa mbegu za kiume.

Squirting fluid

Majimaji haya kwa kawaida hayana rangi wala harufu. Hutengenezwa ndani ya kibofu cha mkojo na hufananA na mkojo. Wakati mwingine majimaji haya yana PSA, na mwanamke huyatoa majimaji haya kwa wingi zaidi kuliko ejaculate.

Hatua 4: Resolution

Hatua ya resolution huurudisha mwili kwenye hali yake ya kabla ya kusisimuliwa kimapenzi. Mtu anaondokana na tendo la ndoa na mshindo.

Mapigo ua moyo na kuhema kunapungua, pressure na damu na kukaza kwa misuli kunarudi kuwa kawaida, maumbile ya uzazi yananywea. Mtu anaweza kujisikia ametosheka na mchovu.

Baada ya mshindo (orgasm), mtu anaingia kwenye refractory period.

Refractory period ni nini?

Refractory period ni kipindi baada ya kufika mshindo ambapo mwili hauna mwitiko tena wa vichocheo vya mapenzi.

Uume wa mwanamme husinyaa na mwanamme huyu hasikii tena msisimko wa kimapenzi.

Urefu wa kipindi cha refractory kinategemeana na umri, ni mara ngapi anafanya mapenzi, jinsi mwenzi alivyo mbele ya mwanamme, na upya wa mapenzi.Utafiti unasema wanawake hawana refractory period, hivi kwamba wanaweza kufika mshindo mfululizo.

Hata hivyo, uchovu baada ya mshindo unaweza kumfanya mwanamke kupoteza hamu ya mapenzi.

Mada yetu ijayo itazungumzia faida za kufanya mapenzi. Usisite kuuliza maswali kuhusu na mada yetu ya leo, ni furaha kwetu kukujibu.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini, au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya muda wa kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.