Jee, Kisukari huleta Upofu? Ujue Ugonjwa Wa Diabetic Retinopathy

 

upofu wa kisukari, dalili katika kuona

Kisukari ni ugonjwa ambao unasababisha uwepo wa sukari kwa wingi ndani ya damu ya mwathirika. Hali ya kuwa na sukari kwa wingi ndani ya mishipa ya damu husababisha matatizo mengi. Leo tutajadili tatizo ambalo kitaalamu huitwa diabetic retinopathy, tatizo ambalo huweza kusababisha upofu. Diabetic retinopathy ni hali inayotokana na kisukari na inayoathiri macho. Diabetic retinopathy inatokana na kuharibiwa kwa mishipa ya damu ya tishu nyepesi zenye uwezo wa kuhisi mwanga zilizopo sehemu ya nyuma ya jicho iitwayo retina. Mwanzoni diabetic retinopathy haionyeshi dalili zo zote au inaweza kutoa matatizo madogo madogo ya kuona. Lakini mwishowe, huweza kusababisha upofu.

upofu na kisukari

Diabetic retinopathy huweza kumpata mtu ye yote mwenye kisukari –  type 1 au type 2 diabetes. Kadiri unavyokaa na kisukari kwa muda mrefu zaidi na kadiri unavyopuuzia kuchukua hatua stahiki za kudhibiti sukari ndani ya mwili wako, ndivyo uwezekano wa kupata tatizo hili unavyoongezeka.

Dalili Za Diabetic Retinopathy

Unaweza usione dalili zo zote kwenye hatua za mwanzo za diabetic retinopathy. Kadiri ugonjwa unavyoongezeka, dalili zifuatazo zinaweza kuanza kujitokeza:

. Vijidoa au vijikamba kuelea mbele ya macho yako (floaters)
. Kutoona vitu vizuri
. Kutopambanua rangi vizuri
. Maeneo meusi au matupu kwenye vitu unavyoviona
. Kushindwa kuona

Chanzo Cha Diabetic Retinopathy

Sukari ikikaa kwa muda mrefu ndani ya damu huweza kusababisha kuziba kwa mishipa midogo ya damu inayopeleka damu kwenye retina, na mwisho kukatisha usambazaji wa damu kwenye eneo hilo. Hali hiyo hupelekea jicho kufanya jitihada za kuotesha mishipa mipya ya damu. Lakini mishipa hiyo  mipya ya damu haikui kufikia kiwango kipaswacho na huweza kuanza kuvuja kirahisi.

Kuna aina mbili za diabetic retinopathy

. Early diabetic retinopathy.

Kwenye aina hii ambayo huonekana zaidi – ambayo pia huitwa nonproliferative diabetic retinopathy (NPDR) — mishipa mipya ya damu haijengwi.

Unapokuwa na NPDR, kuta za mishipa ya damu ndani ya retina hudhoofika. Vijinundu vidogo (tiny bulges) viitwavyo microaneurysms hujitokeza kutoka kwenye kuta za mishipa midogo ya damu, wakati mwingine vikivujishia majimaji au damu kwenye retina. Mishipa mikubwa ya damu ya retina itaanza kupanuka na kuwa na vipenyo visivyo vya kawaida, na NPDR inaweza kukua kutoka ndogo ya kawaida hadi ya hatari, kadiri mishipa ya damu inavyozidi kuzibwa.

Nyuzinyuzi ndogo za neva ndani ya retina zinaweza kuanza kuvimba. Wakati mwingine eneo la kati la retina (macula) litaaanza kuvimba pia (macula edema), hali ambayo itahitaji tiba.

.  Advanced diabetic retinopathy.

Wakati mwingine diabetic retinopathy huweza kukua hadi kuwa hali mbaya zaidi iitwayo, proliferative diabetic retinopathy. Kwenye aina hii, mishipa ya damu iliyoharibiwa huziba, na kusababisha mishipa mingine mipya isiyo ya kawaida kuota ndani ya retina, na kuvujia damu ndani ya eneo lililo kama jeli linalojaza eneo la kati la jicho (vitreous.)

Hatimaye, tishu za makovu zinazozalishwa wakati wa ujenzi wa mishipa mipya ya damu zinaweza kusababisha retina ijibandue kutoka sehemu ya nyuma ya jicho. Mishipa hii mipya ya damu ikileta ukinzani katika kutoa majimaji nje ya jicho, mgandamizo mkubwa huweza kutokea ndani ya jicho. Hali ambayo inaweza kuleta uharibifu kwenye neva inayosafirisha picha kutoka kwenye jicho hadi kwenye ubongo (optic nerve), na kusababisha glaucoma – ugonjwa unaotokana na kuharibiwa kwa optic nerve, unaoweza kusababisha upofu.

Hali Zinazoweza Kusababisha Diabetic Retinopathy

Mtu ye yote mwenye kisukari anaweza kupata diabetic retinopathy. Hali ambazo zinaongeza uwezekano wa kutokea ugonjwa huu ni:

. Muda wa ugonjwa wa kisukari – unapokuwa na kisukari kwa muda mrefu zaidi, ndivyo uwezekano wa kupata diabetic retinopathy unavyoongezeka.

. Udhibiti hafifu wa kiwango cha sukari

. Mgandamizo mkubwa wa damu – high blood pressure

. Kiwango kikubwa cha cholesterol

. Uja uzito

. Matumizi ya tumbaku

. Kuzaliwa kwenye jamii ya wamarekani weusi, wahispania au wamarekani asilia.

Madhara Ya Diabetic Retinopathy

Diabetic retinopathy inahusishwa na kujengeka kwa mishipa mipya ya damu isiyo ya kawaida ndani ya retina. Hali hiyo huweza kusababisha madhara kadhaa katika uonaji:

. Vitreous hemorrhage. Mishipa hii mipya ya damu inaweza kuvujisha damu ndani ya eneo angavu , lililo kama jeli linalojaza eneo la kati la jicho. Kama damu iliyovujia ni ndogo, unaweza kuona vijidoa vyeusi (floaters) vichache vikicheza machoni. Kama hali ni mbaya zaidi, damu inaweza kulijaza eneo la vitreous na kuliziba kabisa jicho lisione.

upofu kutokana na kisulari

Vitreous hemorrhage peke yake haileti upofu wa kudumu. Kwa kawaida damu huondoka na jicho kujisafisha katika wiki au miezi michache. Kama retina haikuharibiwa, uonaji wako unaweza kurudi kwenye hali ya kawaida.

. Retinal detachment. Mishipa ya damu isiyo ya kawaida inayohusiana na diabetic retinopathy huanzisha kukua kwa tishu za mabaka, ambazo zinaweza kuibandua retina kutoka sehemu ya nyuma ya jicho. Hii inaweza kusababisha vijidoa vinavyoelea wakati ukiwa unatazama (floaters), miale ya mwanga au kutoona.

. Glaucoma. Mishipa mipya ya damu inaweza kuota kwenye eneo la mbele la jicho na kuleta ukinzani kwenye mtiririko wa kawaida wa majimaji nje ya jicho, na kusababisha msukumo mkubwa kutokea ndani ya jicho (glaucoma). Msukumo huu huweza kuiharibu neva inayosafirisha picha kutoka kwenye jicho kwenda kwenye ubongo (optic nerve.)

. Upofu. Hatimaye, diabetic retinopathy, glaucoma au vyote vinaweza kuleta upofu.

 

Kwenye mada zetu nyingine tutazungumzia chanzo na tiba ya kisukari, dalili za kisukari, chakula na mazoezi kwa mgonjwa wa kisukari na tiba ya ugonjwa wa kisukari.

Una Tatizo la kutoona vizuri linalitokana na kisukari? Usisite kupata ushauri zaidi.

DAWA YA UPOFU WA KISUKARI

Pata ushauri zaidi kwa kututumia ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au kututumia barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.