Kisukari Husababisha Miguu Kuvimba? Ujue Ugonjwa Wa Diabetic Nephropathy

 

nephropathy dialysis

 

 

Hadi asilimia 40 ya watu wanaougua kisukari hupata matatizo ya figo. Diabetic nephropathy ni ugonjwa hatari wa figo unaotokana na kisukari (type I na type II diabetes). Diabetic nephropathy huathiri utendaji wa kawaida wa figo wa kutoa mabaki na majimaji ya ziada nje ya mwili. Ugonjwa huu ukiendelea huweza kusababsha kufeli kwa figo (kidney end-stage disease) hali ambayo hutishia maisha. Kuna njia mbili tu baada ya figo kufeli ambazo ni tiba ya dialysis au kubadilishiwa figo (kidney transplant).

 

Dalili Za Diabetic Nephropathy

 

Unaweza usione dalili zo zote mwanzoni. Lakini baadaye dalili zifuatazo huanza kuonekana:

. Hali ya pressure ya damu kuzidi kuwa mabaya zaidi
. Protini ndani ya mkojo
. Kuvimba kwa miguu, ankle, mikono au macho
. Mwongezeko wa kujisikia kwenda haja ndogo
. Kupungua kwa uhitaji wa insulin au dawa za kisukari
. Kuchanganyikiwa au kushindwa kutuliza mawazo
. Kupungua kwa hamu ya chakula
. Kichefuchefu au kutapika
. Miwasho isiyoachia
. Uchovu wa mwili

 

Chanzo Cha Diabetic Nephropathy

 

Diabetic nephropathy inatokea wakati kisukari kinapoiharibu mishipa ya damu na seli nyingine ndani ya figo.

 

 chanzo cha nephropathy

 

Jinsi figo inavyofanya kazi

Figo yako ina mamilioni ya mikisanyiko ya vijishipa vidogo vya damu (glomeruli) vyenye kazi ya kuchuja mabaki nje ya damu. Uharibifu mkubwa kwenye vijishipa hivi husababisha diabetic nephropathy, kupungua kwa utendaji kazi wa figo na kufeli kwa figo.

Sababu za diabetic nephropathy

Diabetic nephropathy ni ugonjwa unaotokana hasa na kisukari, type 1 na type 2. Baada ya muda, uwingi wa sukari ndani ya damu unaotokana na kisukari ambayo haikutibiwa husababisha pressure kupanda, nayo huharibu figo kwa kuongeza pressure kwenye mfumo wa uchuchaji ulio muororo.

 

Madhara Yatokanayo Na Diabetic Nephropathy

 

Madhara yanayotokana na diabetic nephropathy yanaweza kujijenga tarartibu katika kipindi cha miezi au miaka kadhaa. Yafuatayo yanaweza kutokea:

 

nephropathy kubonyea miguu

 

. Kuzuiwa kwa maji, ambako kunaweza kusababisha kuvimba kwa mikono na miguu, pressure kupanda, maji ndani ya mapafu (pulmonary edema).
. Kupanda kwa ghafla kwa kiwango cha potassium katika mwili (hyperkalemia)
. Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu (cardiovascular diseases), na pengine kusababisha stroke
. Kuharibika kwa mishipa ya damu ndani ya macho (diabetic retinopathy)
. Upungufu wa chembechembe nyekundu za damu mwilini
. Madonda miguuni, uume kushindwa kusimama, kuharisha
. Matatizo ya mimba yanayohatarisha maisha ya mama na kichanga tumboni
. Matatizo yasiyotibika ya figo ambayo yatahitaji dialysis au kubadilishiwa figo.

Tiba ya Diabetic Nephropathy

Hatua ya kwanza katika tiba ya diabetic nephropathy ni kukitibu kisukari, na kama itabidi pressure.Kwa kudhibiti sukari katika damu yako na pressure yako, unaweza kuzuia au kupunguza kasi ya diabetic nephropathy.

Katika mada nyingine tumezungumzia madhara ya kisukari kwenye neva na kusababisha diabetic neuropathy na madhara ya kisukari kwenye macho na kusababisha diabetic retinopathy.

 

Kwa ushauri zaidi kuhusu somo hili, tupigie kupitia 0655 858027 au 0756 181651.