Katika mada yetu ya leo tatalijadili tatizo linalowapata baadhi ya wanaume linaloitwa kuchelewa kufika kileleni au kuchelewa kuwaga au kuchelewa kukojoa. Tutaona sababu za tatizo hilo na hatua unazoweza kuchuzikua ili kupunguza au kuondoa tatizo hilo.
Kuchelewa kufika kileleni ni hali ya kufika kileleni kwa shida au kushindwa kufika kileleni na kutoa shahawa. Ni plale unapohitaji kusisimuliwa sana na inacchukua muda mrefu sana kwako kufika mshindo na kumwaga mbegu, wakati mwingine ukashindwa kabisa kumwaga mbegu.
Kitaalamu hali huitwa delayed ejaculation au impaired ejaculation au delayed orgasm.
Kushindwa kabisa kumwaga mbegu huitwa anejaculation na kushindwa kufika mshindo huitwa anorgasmia.
Mwanamme akichukua zaidi ya dakika 30 kumwaga mbegu, pamoja na kuwa uume wake ulisimama vyema, tunasema ana tatizo hili la delayed ejaculation.
Asilimia 1-4 ya wanaume wana tatizo hili la kuchelewa kufika kileleni.
Kuchelewa kufika kileleni kunaweza kusababisha huzuni kwa mwanamme na mwenzi wake.
Kunaweza kusababisha wasiwasi kuhusu afya, kukasababisha kukosa hamu ya tendo la ndoa na kutoridhika kimapenzi. Kunaweza pia kuleta matatizo ya mahusiano na wasiwasi baina ya wapenzi wanaotaka kujenga familia.
Wanaume wengi hupata tatizo la kushindwa kufika kileleni kwa wakati fulani, lakini kuna wengine, tatizo hili huwa ni la kudumu.
Sababu Za Kuchelewa Au Kushindwa Kufika Kileleni
Kushindwa kufika kileleni kunaweza kuletwa na sababu za kimaumbile au sababu za kisaikolojia. Wakati mwingine, aina zote mbili zinaweza kuhusika. Tatizo linaweza kuwa la maisha, ambapo mtu atashindwa muda wote kufika kileleni.
Lakini, mara nyingi tatizo huja baada ya kuwa mtu alikuwa akifika kileleni kama kawaida.
Sababu za kimaumbile ni pamoja na:
- . Matokeo mabaya ya matumizi ya madawa yanaweza kuwa ni sababu. Tatizo linaweza kusbabishwa na:
- . antidepressants, na hasa selective serotonin reuptake inhibitord (SSRIs)
- . antianxiety drugs
. dawa za blood pressure
. dawa za kuondoa maumivu
. na dawa zinginezo - . pombe au matumizi ya baadhi ya dawa za kujiburudisha
- . mabadiliko ya homoni, kama hypogonadism (testosterone ndogo)
- . Kuwa na prolactin nyingi mno (hyperprolactinemia)
- . Shida kwenye tezi dume, kama prostatitis
- . Uharibifu wa neva, pamoja na kiharusi, kuumia uti wa mgongo, upasuaji, multiple sclerosis, kisukari cha juu
- . Umri mkubwa unaweza kupunguza usikivu wa uume ukisisimuliwa
Tatizo hili likitokea baadaye hugundulika kama ni la kisaikolojia kama linatoteka kwenye baadhi ya mazingira tu.
Kwa mfano, tatizo linaweza kuwa ni la kisaikolojia iwapo mtu anafika mshindo akipiga punyeto lakini anapata shida kufika mshindo akiwa na mwenzi wake.
Sababu za kisaikolojia zinazoweza kuchangia kuchelewa kufika kileleni ni pamoja na:
. historia ya mwanzo ya maisha, pamoja na kunyanyaswa, kutelekezwa na wazazi au makuzi mabaya kuhusu tendo la ndoa
. hasira inayofichwa
. kushindwa kupata burudani
. imani za kidini, labda kwamba tendo la ndoa ni dhambi
. hofu, kwa mfano, ya shahawa au maumbile ya kike, au hofu ya kumwumiza mpenzi kwa kwa kumwagia shahawa
. hofu ya mimba
. kukosa kujiamini, au wasiwasi wa ufanisi wa tendo -kwa mfano, wasiwasi kuhusu mwonekano wa mwili.
Kuna aina fulani za upigaji punyeto zinazoweza kusababisha tatizo la kuchelewa au kushindwa kufika kileleni.
Mtaalamu mmoja wa somo hili aligundua uhusiano wa tatizo hili na tabia zifuatazo za upigaji punyeto.
. kupiga punyeto mara nyingi, kama zaidi ya mara tatu kwa wiki
. upigaji punyeto usifanana kabisa na tendo la ndoa, hasa wa kasi sana, wa kubana sana uume au unaosababisha mhemko mkubwa sana
. kushindwa kuiga kwa urahisi staili ya mkono ya mwenzzi wako, mdomo au uke
. kuwa na mpenzi afanyaye tofauti kabisa na ubunifu unaoutumia wakati wa kupiga punyeto na kukufikisha kileleni.
Mtaalamu huyu aligundua kuwa watu wengi wenye matatizo ya kufika kileleni walitoa ripoti kuwa hawakusumbuka kufika mshindo au kukojoa wakiwa kwenye punyeto.
Tiba Ya Kuchelewa Kufika Kileleni
Tiba ya taizo la kuchelewa kufika kileleni inategemea chanzo cha tatizo. Endapo aina fulani ya dawa ni chanzo, daktari atakuandikia dawa mbadala.
Kama pombe au madawa mengine yasiyo rasmi ndicho chanzo, kupunguza au kuacha kutasaidia. Kama ni matatizo mengine ya kiafya, kuondoa chanzo kutasaidia, kama ni matatizo ya neva, kuyaondoa kutasaidia.
Katika mada yetu nyingine, tutalizungumzia tatizo la mwanamme kuwahi kufika kileleni. Usisite kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo.
Pata ushauri zaidi kwa kututumia ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au kututumia barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu ndani ya saa za kazi kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.