Kukosa Usingizi (Insomnia)

 

 

Tatizo la kukosa usingizi (insomnia) linawapata mamilioni ya watu duniani. Kukosa usingizi (insomnia) ni tatizo la kawaida linalomfanya mtu ashindwe kupata usingizi, kuendelea kulala, au kuamka mapema sana alfajiri na kushindwa kupata usingizi tena akirudi kitandani. Unaweza kuamka na kujisikia bado umechoka. Insomnia haikupunguzii nguvu na uchangamfu wako tu, bali afya, ufanisi wa kazi na ubora wa maisha yako.

Ni kiasi gani cha usingizi kinatosha, hutofautiana baina ya mtu na mtu, lakini kwa ujmla mtu mzima anahitaji saa 7 hadi 9 za usingizi mzuri katika saa 24 za siku.

Watu wengi hupata tatizo la kukosa usingizi kwa kipindi kifupi, kinachodumu siku au wiki kadhaa. Mara nyingi hii hutokana na msongo wa mawazo au kuumia sehemu ya mwili. Lakini watu wengine hupata insomnia inayodumu mwezi au zaidi. Insomnia inaweza kuwa ndilo tatizo, au tatizo linaweza kutokana na matatizo mengine ya kiafya.

Mabadiliko madogo katika staili yako ya kuishi yanaweza yakakusaidia.

Dalili Za Tatizo La Kukosa Usingizi

Dalili za kuwa unakosa usingizi ni pamoja na:

. Kushindwa kupata usingizi usiku
. Kuamka usiku
. Kuamka mapema mno asubuhi
. Kusikia kama hujapumzika vizuri baada ya kuamka
. Uchovu na kusinzia mchana
. Hasira, mfadhaiko na wasiwasi
. Shida kutuliza mawazo, kufanya jambo moja ulilokusudia na usahaulifu
. Kufanya makosa mengi au ajali
. Kuwa na wasiwasi kuhusu kulala.

Sababu Za Kukosa Usingizi

Kukosa usingizi kunaweza kuwa ndilo tatizo lenyewe au kukaambatana na hali nyingine.

Tatizo sugu la kukosa usingizi kwa kawaida husababishwa na msongo wa mawazo, matukio ya maisha au tabia zinazokatisha usingizi. Kujua na kudhibiti chanzo cha tatizo kunaweza kuliondoa tatizo hili, lakini wakati mwingine inaweza ikachukua miaka.

Sababu za kawaida za kukosa usingizi ni:

. Msongo wa mawazo: Maswala yanayohusu kazi, shule, afya, pesa aukukosa usingizi kwa msongo wa mawazo familia yanaweza yakaufanya ubongo wako ufanye kazi usiku, na kukufanya ushindwe kulala. Matukio makubwa ya maisha au kuumia – kama kifo au ugonjwa wa mtu umpendaye, kuachika, au kuachishwa kazi nayo yanaweza kusababisha kukosa usingizi.

. Safari au ratiba ya kazi: Mwili hatimaye unapanga utaratibu (circadian rhythms) wa kuufuata na unafanya kazi kama saa, ukikuongoza kuhusu mzunguko wa kulala na kuamka, mpangilio wa shughuli za kimetaboliki na joto la mwili. Kuuvuruga mpango huu kunaweza kusababisha kuukosa usingizi. Sababu ni pamoja na ndege kuchelewa ikiwa inasafiri kutoka time zone moja kwenda nyingine, kufanya kazi hadi usiku wa manane au kwenye shifti, au kubadili shifti mara kwa mara.

. Tabia mbaya za kulala: Tabia mbaya ya kulala ni pamoja na kutokuwa na muda maalumu wa kulala, kupata usingizi mfupi wa mchana (naps), vitu vya kusisimua kabla ya kulala, mazingira ya kulala yasiyo mazuri, kutumia kitanda chako kwa kazi, kula au kuangalia TV, vioo vya kompyuta, video games, smartphones na vinginevyo vinaweza kuuvuruga mzunguko wako wa kulala.

. Kula usiku kupita kiasi ukiwa umechelewa: Kupata chakula chepesi kabla ya kulala haina shida, lakini kula chakula kingi mno kunaweza kukufanya usijisikie vizuri wakati umelala. Watu wengi wanapatwa na kiungulia, wanacheua tindikali na chakula, hali inayowafanya wawe macho.

Insomnia sugu inaweza pia kuhusishwa na hali ya kiafya au na matumizi ya baadhi ya madawa. Kutibu tatizo la kiafya kunaweza kuboresha usingizi, lakini tatizo la kukosa usingizi linaweza likaendelea hata baada ya kupata ahueni ya tatizo la kiafya.

Sababu nyingine za kukosa usingizi ni pamoja na:

. Matatizo ya afya ya akili: Matatizo ya kuwa na wasiwasi, kama tatizo la kuwa na msongo wa mawazo baada ya kuumwa, yanaweza kuvuruga usingizi wako. Kuamka mapema mno yaweza kuwa ni dalili ya mfadhaiko. Isomnia inaweza kuambatana na matatizo mengine ya afya ya akili.

. Madawa: Kuna dawa nyingi zinazoweza kusababisha ukose usingizi, kama baadhi ya dawa za mfadhaiko na dawa za asthma au blood pressure. Dawa nyingi kama za maumivu, za allergy, za mafua na kupunguza uzito, zina caffeine na vitu vingine ambavyo vinaweza kuvuruga usingizi.

. Hali ya afya: Hali mbaya za kiafya zinazoweza kuvuruga usingizi ni kama maumivu sugu, saratani, kisukari, magonjwa ya moyo, asthma, gastroesophageal reflux disease (GERD), tezi ya thyroid, Parkinson’s disease na ugonjwa wa Alzheimer’s.

. Matatizo yanayohusiana na usingizi: Tatizo la sleep apnea linakufanya usimame pumzi kwa vipindi usiku mzima, na kukuvurugia usingizi. Tatizo la miguu kutokutulia (Restless legs syndrome) hukufanya usijisikie vizuri miguuni na kukuletea kishawishi kinachokushinda cha kuichezesha miguu, hali inayokufanya ushindwe kulala.

 

kukosa usingizi

 

. Kahawa, nicotine na pombe: Kahawa, chai, cola na vinywaji vingine vyenye caffeine husisimua. Kutumia vinywaji hivi alasiri au jioni huweza kukusababishia ukose usingizi usiku. Nicotine iliyomo ndani ya bidhaa za tumbaku ni kitu cha kusisimua na inaweza kuvuruga usingizi. Pombe inaweza kukufanya upate usingizi, lakini inazuia usiingie kwenye hatua za usingizi wa kina na mara nyingi hukufanya uamke katikati ya usiku.

Kukosa Usingizi Na Kuzeeka

Tatizo la kukosa usingizi linakuwa la kawaida zaidi mtu anapokuwa na umri mkubwa. Kadiri unavyokuwa na umri mkubwa, unaweza kuyaona yafuatayo:

. Mabadiliko katika mwenendo wa kulala. Usingizi unakupumzisha kidogo zaidi unapozeeka, hivyo kelele na mabadiliko mengine kwenye mazingira yako yanaweza kukuamsha. Umri ukisogea, saa yako ya mwili inawahi, kwa hiyo unachoka mapema jioni na kuamka mapema zaidi asubuhi. Lakini watu wa umri mkubwa bado wanahitaji saa zile zile za kulala kama watu wa umri mdogo.

. Mabadiliko Ya Shughuli. Unaweza kuwa umepunguza shughuli za kimwili au kijamii. Kukosa shughuli za kufanya kunaweza kuvuruga upatikanaji wa usingizi mnono. Na vile vile, kadiri unavyokosa shughuli za kufanya, ndivyo uwezekano wa kupata vipindi vifupi vya usingizi wa mchana unavyoongezeka.

. Mabadiliko Ya Kiafya. Maumivu sugu yanayotokana na hali kama za arthritis au maumivu ya mgongo na hata mfadhaiko au wasiwasi yanaweza kuvuruga usingizi. Hali zinazodai kupata haja ndogo usiku – kama tezi dume au matatizo ya kibofu cha mkojo – vinaweza kuvuruga usingizi. Sleep apnea na restless legs syndrome vinakuwa vya kawaida umri ukiwa mkubwa, ambavyo vinaweza kukuvurugia usingizi.

. Dawa zaidi. Watu wa umri mkubwa kwa kawaida hutumia madawa mengi zaidi kuliko vijana, jambo linalowaongezea uwezekano wa kupata tatizo la kukosa usingizi linalotokana na dawa.

Kukosa Usingizi Kwa Watoto Na Vijana

Tatizo la kukosa usingizi huwagusa pia watoto na vijana. Lakini, baadhi ya watoto hupata shida ya kwenda kulala kwa sababu mpangilio wa muda wa kulala (saa za miili yao) umesogezwa mbele. Wanataka walale baadaye na kisha wachelewe kuamka kesho yake asubuhi.

 

kukosa kulala

 

Madhara Yatokanayo Na Kukosa Usingizi

Usingizi ni muhimu kwa afya yako kama kilivyo chakula chenye afya na mazoezi ya kila wakati. Bila kujali sababu yake, kukosa usingizi kutakuathiri kiakili na kimwili. Watu wanaokosa usingizi wameonekana kuwa na maisha duni ukilinganisha na wale wanaolala vyema. Unaweza kujifahamisha vizuri zaidi kuhusu faida za kupata usingizi mzuri kwenye ukurasa mwingine unaelezea faida za kupata usingizi wa kutosha.

Madhara yatokanayo na kukosa usingizi ni pamoja na:

. Ubongo kushindwa kutoa mabaki na kusababisha:
– mtu kufikia viwango akiwa kazini au shuleni
– kushindwa kuchukua hatua za haraka unapoendesha gari na kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kufanya ajali
. Matatizo ya kiakili kama mfadhaiko , wasiwasi na kutumia pombe na madawa ya kulevya
. Uwezekano wa kupata magonjwa ya muda mrefu kama pressure na magonjwa ya moyo        . Kuvurugika kwa homoni mbalimbali katika mwili
. Kuongeza kwa uwezekano wa mifupa kuvunjika
. Kudhoofika kwa kinga za mwili.

Namna Ya Kuondoa Tatizo La Kukosa Usingizi

Tabia za kwenda kulala zinaweza kuzuia insomnia na kukupa usingizi mzito:

.1 Uwe na muda wa kulala na kuamka unaoeleweka siku hadi siku, pamoja na wikiendi.
2. Uwe na shughuli muda wote – kufanya kazi kila wakati kunachangia kupata usingizi.
3. Chuguza dawa unazotumia kama zinasababisha kukosa usingizi
4. Kwepa au acha kupata vipindi vidogo vya usingizi (naps) wa mchana
5. Acha au punguza matumizi ya caffeine na pombe, usitumie nicotine.

6.  Usipate milo mikubwa au vinywaji kabla ya kulala.
7. Kitengeneze chumba chako kiwe cha kustarehesha na kitumie kwa kulala na kufanya mapenzi tu. Hakikisha hakina mwanga mkali, kuna utulivu na hakuna kelele kubwa.
8. Jitengenezee kitu cha kufanya kabla ya kulala kama kuoga maji ya vuguvugu, kujisomea au kusikiliza muziki myororo.

Katika mada yetu nyingine, tutazungumzia faida ya kupata usingizi wa kutosha. Usisite kuuliza maswali uliyo nayo kuhusu uandishi wa mada hii yetu ya leo.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu  ndani ya saa za kazi  kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.