Kutoka Usaha Sehemu Za Siri. Ujue Ugonjwa Wa Chlamydia

 

 

 

 

Unaweza kuwa umepata ugonjwa wa zinaa na ukaona usaha unatoka kutoka kwenye uume au uchafu kutoka ukeni ukashindwa kujua ni tatizo lipi kati ya gonorrhea na chlamydia linalokusumbua. Katika somo letu la leo tutaujadili ugonjwa wa chlamydia na kutoa tofauti zake na ugonjwa wa gonorrhea.

Chlamydia ni ugonjwa unaowapata watu wengi na unaenezwa kwa ngono. Ni ugonjwa unaoshambulia jinsia zote na mara nyingi hauonyeshi dalili zo zote. Dalili zikionekana, ni baada ya wiki kadhaa kutoka siku ya mambukizo.

 

Chanzo Cha Chlamydia

 

Chlamydia huenezwa na bakteria aitwaye Chlamydia trachomatis. Bakteria huyu hupatikana kwenye shingo ya kizazi (cervix), mrija wa mkojo, uke na/au mkundu. Bakteria huyu pia huishi ndani ya koo. Namna yo yote ya kujamiiana inaweza kumweneza bakteria huyu.

 

chlamydia cervical

 

 

Dalili Za Chlamydia

 

Katika hatua za awali, maambukizo ya bakteria huyu mara nyingi hayaonyeshi dalili zo zote. Dalili zinaweza kuanza kuonekana baada ya wiki moja au mbili kutoka siku ya kupata maambukizo. Dalili za mwanzo huwa si kali hivi kwamba ni rahisi sana kuzipuuzia.

Dalili za chlamydia zinaweza kuwa:

. Maumivu ya sehemu ya chini ya tumbo
. Maumivu wakati wa kukojoa
. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
. Maumivu ya nyonga
. Usaha au uchafu kutoka kwenye uume
. Kutoka damu kwenye mkundu
. Uchafu kutoka kwenye mkundu
. Maumivu kwenye mkundu
. Maumivu kwenye korodani
. Kukojoa mara kwa mara
. Uchafu kutoka ukeni
. Maumivu ukeni
. Kutokwa damu katikati ya hedhi na baada ya tendo la ndoa kwa wanawake.

Unaweza pia kupata maambukizo ya chlamydia kwenye macho (conjunctivitis) kwa kugusana na mtu mwenye chlamydia.

 

chlamydia machoni

 

Kuna Tofauti Gani kati ya Gonorrhea na Chlamydia?

Tofauti Za Chlamydia Na Gonorrhea

Chlamydia na gonorrhea yote ni magonjwa yanayoenezwa kwa ngono na yanayowapata watu wa jinsia zote, wanawake kwa wanaume. Magonjwa yote mawili huenezwa na bakteria ambao wanaleta maambukizo yanayoshambulia utando telezi, ambazo ni tishu zenye unyevu, laini zisizofunikwa na ngozi. Chlamydia husababishwa na bakteria aitwaye chlamydia trachomatis, ambaye anaweza kupatikana kwenye uke, shingo ya uzazi (cervix), mrija wa mkojo (urethra), na rektamu na hata kwenye koo na macho. Gonorrhea husababishwa na bakteria aitwaye Neisseria gonorrhoeae. Bakteria huyu wa gonorrhea anaweza kupatikana kwenye shingo ya kizazi, uterus, mirija ya uzazi na kwa wanaume kwenye mrija wa mkojo. Anaweza pia kuambukiza kwenye mkundu, mdomo na koo.

 

chlamydia mdomoni

 

Magonjwa haya yote mawili yanaweza kumpata kichanga wakati wa kuzaliwa endapo mama atakuwa ni mgonjwa.

Gonorrhea ni ugonjwa wenye dalili za kutoka uchafu ukeni, maumivu eneo la chini ya tumbo na maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa wanawake. Dalili kwa wanaume ni kutoka usaha na maumivu wakati wa kukojoa. Isipotibiwa huweza kuleta maambukizo kwenye korodani (epididymitis), prostatitis na maambukizo kwenye mrija wa mkojo (urethritis). Kwa wanawake huweza kusababisha pelvic inflammatory disease (PID), septic arthritis kwenye vidole, kiwiko, dole gumba na ankle.

Karibu asilimia 50 ya watu wenye gonorrhea wana chlamydia. Wakati gonorrhea huleta maumivu wakati wa kukojoa, chlamydia haileti maumivu. Chlamydia hutoa uchafu tu kutoka kwenye uume.

Hakuna dalili zinazoonekana baada ya maambukizo ya chlamydia na bakteria wanaweza kuendelea kuwemo ndani ya mwili kwa miezi mingi kabla ya kugundulika. Hadi mwisho mwathirika atakapopata maumivu na kuona usaha. Chlamydia hutibika kwa antibiotics, kama, azithromycin, Doxycycline, Tetracycline, na Erythromycin. Gonorrhea hutibiwa na ofloxacin, Cefixine, na Ceftriaxone ambazo ni tiba kali zaidi.

 

Madhara Yatokanayo Na Chlamydia

 

Chlamydia inaweza kusababisha madhara mengi, baadhi yakiwa:

. Kupata maradhi mengine yanayoenezwa kwa ngono. Watu wenye chlamydia wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa magonjwa mengine yanayoenezwa kwa ngono – kama gonorrhea na HIV.

 

chlamydia mdomoni

 

. Pelvic inflammatory disease (PID). PID ni maambukizo kwenye uterus na mirija ya uzazi yanayoleta maumivu ya nyonga na homa. PID huweza kuiharibu mirija ya uzazi, ovari na uterus pamoja na cervix.

. Maambukizo karibu na korodani (epididymitis). Maambukizo ya chlamydia huweza kuleta uvimbe kwenye kijibomba kilichojikunja chini ya korodani (epididymis). Maambukizo haya huweza kuleta homa, kuvimba na maumivu ya pumbu.

. Maambukizo ya tezi dume. Bakteria wa chlamydia wanaweza kusambaa hadi kwenye tezi dume na kusababisha prostatitis, ugonjwa ambao huleta maumivu wakati wa kujamiiana au baada ya kujamiiana, homa, maumivu wakati wa kukojoa, na maumivu sehemu ya chini ya mgongo.

. Maambukizo kwa vichanga. Chlamydia wanaweza kuambukiza kichanga kutoka kwenye mkondo wa uke wakati wa kuzaliwa, na kukisababishia pneumonia na maambukizo mabaya ya macho.

 

 

. Reactive arthritis. Watu wenye chlamydia wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata reactive arthritis ambayo pia huitwa Reiter’s syndrome. Reiter’s syndrome huathiri joints, macho na mrija wa mkojo.

. Ugumba. Chlamydia wanaweza kusababisha makovu na kuziba kwa mirija ya uzazi, hali ambayo inaweza kumsababishia mwanamke ugumba.

 

Katika mada tofauti tutaujadili ugonjwa wa kisonono (Gonorrhea).

 

Usisite kutuma maswali au maoni yako yanayohusiana na mada hii ya leo. Tutakuwa na furaha kubwa kukujibu.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya saa za kazi  kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.