Lijue Tatizo La Fibroids – Uvimbe Ndani Ya Kizazi

Fibroids Ni Kitu Gani? Ni Nini Tiba Ya Fibroids?

Fibroids au uvimbe ndani ya kizazi cha mwanamke, ni uvimbe wa misuli laini wenye mizizi ya kuiunganisha, unaoota na kukua kwenye nyumba ya uzazi (uterus). Majina mengine ya uvimbe huu ni uterine fibroids, myomas, au fibromyomas. Fibroids ni aina ya uvimbe unaoonekana kwa wingi zaidi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Fibroids ni uvimbe ambao mara nyingi  (asilimia 99) hauna madhara kiafya na wala kuhusiana na ugonjwa wa kansa.

Fibroids huweza kuota kama kijinundu kimoja au kama kikundi. Kikundi cha fibroids kinaweza kuwa na ukubwa kuanzia kipenyo cha milimita moja hadi sentimeta 20 (inchi 8) au zaidi. Kwa kupata picha zaidi, fibroids ziinaweza kuwa na ukubwa wa punje au zikafikia ukubwa wa tikitimaji. Uvimbe huu unaweza kuota juu ya ukuta wa nyumba ya mimba, ndani kwenye uwazi wa nyumba ya mimba au katikati ya ukuta huo.

aina ya fibroids

Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 20 hadi 50 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa, miaka 30 hadi 50, wana uvimbe katika kizazi (fibroids), ingawa wengi wao hawahangaiki kuchukua vipimo.  Watu ambao bado hawajaona hedhi zao za kwanza hawawezi kuwa na fibroids. Fibroids ni nadra kuonekana kwa watu wailiokoma hedhi.

Chanzo Cha Fibroids

Sababu hasa za kuota kwa fibroids katika viungo vya uzazi vya mwanamke bado hazieleweki vizuri ingawa inaamika kwamba kila uvimbe wa fibroid unatokana na seli ya musuli wa uterus ambayo imeamua kuwa na tabia ya tofauti na nyingine na ikaanza kukua kwa haraka ikichangiwa na uwepo wa homoni ya estrogen.

Wanawake wanaokaribia kufikia ukomo wa kupata siku zao za mwezi wanaonekana kuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata fibroids kwa sababu ya kuwa wameishi na homoni ya estrogen kwa muda mrefu zaidi. Wanawake wenye asili ya mchanganyiko wa wamarekani na waafrika (wamarekani weusi) nao wanaonekana kupatwa na fibroids zaidi ya wanawake wengine ingawa sababu bado haijajulikana.

Baadhi Ya Sababu Zaweza Kuwa

. Mabadiliko ya jeni (genes). Jeni ni sehemu ya DNA inayorithisha tabia au umbile fulani. Fibroids nyingi zina mabadiliko katika jeni yaliyo tofauti na seli za kawaida za misuli ya nyumba ya mimba.

. Homoni. Homoni za estrogen na progesterone husababisha tishu zinazotanda kuta za ndani za nyumba ya kizazi kuvimba kwenye kila mzunguko wa hedhi ili kujiandaa kwa ujauzito. Homoni hizi ainaonekana kuwa zinasaidia ukuaji wa fibroids. Fibroids huwa na seli nyingi zaidi ambako estrogen na progesterone huweza kunata kuliko misuli ya kawaida ya nyumba ya mimba. Fibroids husinyaa baada ya kukoma hedhi kwa sababu ya kushuka kwa viwango vya homoni.

. Sababu nyingine. Vitu ambavyo huusaidia mwili kulinda tishu, kama insulin-like growth factor, husaidia ukuaji wa fibroid.

. Exracellular matrix (ECM). Hivi ni vitu ambavyo hufanya seli kunatana, kama sementi kati ya tofali. ECM huongezeka ndani ya fibroid na huzifanya kuwa za nyuzinyuzi. ECM pia hutunza growth factors na kuanzisha mabadiliko ya kibayolojia ndani ya seli zenyewe.

Madaktari wanaamini kuwa fibroids huanza kukua kutokana na stem cell kutoka ndani ya tishu laini za misuli ya nyumba ya mimba. Seli moja hujigawa tena na tena. Baada ya muda huwa kitu kigumu kinachotereza tofauti na tishu za karibu yake.

Ukuaji wa fibroids huwa tofauti. Unaweza kuwa wa taratibu au haraka. Au ukabakia katika ukubwa ule ule. Fibroids nyingine zinakua haraka na nyingine zinanywea zenyewe.

Fibroids zinazotokea wakati wa ujauzito,  zinaweza kunywea au kutoweka baada ya ujauzito, wakati nyumba ya mimba inaporudi kwenye hali yake ya kawaida.

Sababu Zinazochangia Kutokea Kwa Fibroids

. Unene. Unene wa kupindukia na kuwa na BMI kubwa

. Asili (mbari). Watu wote walozaliwa na jinsia ya kike wanaweza kupata fibroids. Lakini wenye rangi nyeusi wana hatari zaidi ya kupata fibroids kuliko wengine. Watu weusi hupata fibroids kwenye umri mdogo zaidi kuliko watu weupe. Vile vile hupata fibroids kubwa zaidi, na dalili mbaya zaidi, kuliko watu weupe.

. Historia ya familia. Kama mama yako au dada yako wana fibroids, utakuwa kwenye hatari ya kupata fibroids.

. Kutozaa watoto

. Kuchelewa kukoma hedhi

. Sababu nyingine. Kuanza kupata hedhi kabla ya umri wa miaka 10; kuwa na upungufu wa vitamini D; kula chakula chenye nyama nyekundu nyingi na mboga za majani, matunda na maziwa kidogo; na kunywa pombe vinaonekana kuongeza uwezekano wa kupata fibroids.

Fibroids Na Kupata Mimba

Kwa kawaida fibroids hazizuii kupata mimba. lakini baadhi ya fibroids – hasa submucosal fibroids – huweza kusababisha ugumba au kupoteza ujauzito.

Fibroids huweza kusababisha matatizo ya ujauzito. Ikiwa ni pamoja na:

. Placental abruption, hali ambapo kiungo kinacholeta oksijeni na virutubishi kwa mtoto, kiitwacho placenta, kinapojibandua kutoka kwenye ukuta wa ndani wa uterus.

. Fetal growth restriction, hali ambapo mtoto wa tumboni hakui kama inavyotegemewa.

. Preterm delivery, mtoto kuzaliwa mapema mno, kabla ya wiki ya 37 ya ujauzito.

 

Utafiti umeonyesha pia kuwa idadi ya wanawake wanaopatwa na fibroids katika kundi la wanawake ambao wamezaa watoto angalau wawili wakiwa hai huwa ni nusu ukilinganisha na wale ambao hawajazaa hata mara moja. Hapa haieleweki kama kuzaa kulizuia wanawake hawa wasipate fibroids au fibroids ndizo zilizozuia wanawake wa kundi la pili wasizae. Utafiti kuhusu hilli bado unaendelea.

Dalili Za Fibroids

Akina mama wengine wenye uvimbe wa fibroids huwa hawaoni dalili zo zote zile (wengi hawajui kama wana fibroids) au kuona dalili kidogo na kwa wengine dalili hizi hujitokeza sana na kuwasumbua hadi kufikia kutafuta tiba. Baadhi ya dalili za fibroids ni:

– Kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku au kutokwa na damu  kwa muda mrefu

– Kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku au kutokwa na damu kwa muda mrefu

– Kutokawa na damu kusiko kwa kawaida katikati ya siku za mwezi

– Mauvimu ya nyonga (uvimbe kugandamiza kwenye viungo vya nyonga)

– Kupata haja ndogo mara kwa mara

– Maumivu ya mgongo

– Maumivu wakati wa tendo la ndoa

– Upungufu wa damu kwa sababu ya kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku

– Maumivu ya kichwa

– Maumivu kwenye miguu

– Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo (Fibroids kubwa)

– Uzazi wa shida

– Mimba za shida

– Kutopata mimba

– Kutoka kwa mimba mara kwa mara.

Mara chache inaweza kutokea fibroid ikasababisha maumivu makali ya ghafla wakati fibroid imekuwa kubwa kuliko uwezo wa mwili wa kuilisha damu na hivyo kuanza kufa yenyewe.

Fibroids huweza kusababisha hedhi kuwa nzito au hata kupata hedhi za katikati ya mzunguko. Kwa sababu hiyo, watu wenye fibroids wanaweza wakapata tatizo la upungufu wa damu (anemia). Anemai ni hali inayotokea wakati mwili wako una upungufu wa seli za chembechembe nyekundu za damu zenye afya ili kupeleka oksijeni kwenye viungo vyako.

Dalili za fibroids kwa kawaida huondoka baada ya kukoma hedhi kwa sababu ya kupungua kwa homoni ndani ya mwili.

Aina Ya Fibroids

Kuna aina nne za Fibroids

  • Intramural: Fibroids aina hii hukua ndani ya musuli wa  ukuta wa nyumba ya mimba  (uterus). Hii ndiyo aina ya fibroids inayowapata wanawake wengi.
  • Subserosal fibroids: Fibroids aina hii hukua nje ya kuta za uterus na huweza kuwa na shina. Subserosal fibroids  fibroids huweza  shina kukua na kuwa kubwa sana.
  • Submucosal fibroids: Fibrioids aina hii huota na kukua kwenye misuli chini ya ngozi laini ya kuta za uterus na huvimba kuelekea ndani kwenye uwazi wa nyumba ya mimba.
  • Cervical fibroids: Fibroids aina hii hujenga kwenye shingo ya uzazi (cervix).

Fibroid ni nini

Tiba Ya Fibroids

Kama mwanamke hapati usumbufu wa namna yo yote katika shughuli zake za kawaida, anaweza asipewe tiba ya aina yo yote hata kama imegundulika kuwa ana uvimbe wa fibroid kwa sababu mwanamke anapokaribia kukoma hedhi fibroids hunyauka zenyewe na mara nyingine kutoweka kabisa.

Endapo tiba imekuwa ni ya lazima, anaweza kupewa dawa au kufanyiwa upasuaji kutokana na hali iliyopo.

Epuka Chakula Kinachochangia Kukua Kwa Fibroids

Chakula ambacho unaweza kula ili kupunguza uwezekano wa kupata fibroids ni pamoja na nyama ya kusindikwa yenye mafuta mengi. Nyama ya kusindikwa yenye mafuta mengi ni moja ya chakula kibaya sana kwa wanawake kuhusiana na fibroids. Chakula chenye mafuta mabaya, kama mafuta yasiyo ya mimea au trans-fats (pamoja na hamburgers, sausages), vinaweza kuongeza viwango vya uvimbeuchungu (inflammation).

Chakula kilichosindikwa huongezwa kemikali na viambato ambavyo huchangia kuongezeka kwa uvimbeuchungu. Punguza kiwango cha nyama na ongeza ulaji wa protini inayotokana na mimea.

Virutubishi Vinavyosaidia Kupunguza Fibroids

-Vitex (400mg mara mbili kwa siku). Vitex au Chasteberry hupunguza viwango vya estrogen na kusisimua uzalishaji wa progesterone. Kwa matokea mazuri, vitex itumiwe angalau kwa miezi sita.

-Fish Oil (1000mg kila siku) au flaxseed Oil (kijiko kimoja kila siku). Essential fatty acids zilizomo ndani ya fish oil na flaxseed yamaweza kusaidia kupunguza uvimbeuchumgu katika mwili na hivyo kusaidia kuzuia ukuaji wa fibroids.

-B-complex (50mg kila siku). Vitamini za B husaidia ini kufanya shughuli zake za kimetaboliki na kudhibiti viwango vya estrogen.

-Progesterone Cream (1/4 kijiko, mzunguko wa siku 6-26). Kupaka progersterone juu ya ngozi kunaweza kuweka sawa viwango vya progesterone vilivyo chini.

-Milk Thistle (150mg mara mbili kila siku). Husaidia katika kutoa sumu katika ini, hali ambayo itaweka sawa viwango vya homoni.

Tiba Ya Fibroids Kwa Kutumia Dawa

Tiba kubwa ya fibroids ni kwa kutumia dawa aina ya GnRHA (gonadotropin released hormone agonist)  ambayo hutolewa kama sindano. Dawa hii huufanya mwili wa mwanamke upunguze utengenezaji wa estrogen hivyo kusababisha fibroids kunyauka.

Tiba nyingine ni Tranexamic acid, vidonge vya kuzuia maumivu, vidonge vya kuzuia mimba (kuzuia mwanamke asipate siku) na LNG-IUS (Levonorgestrel intrauterine system) ambacho ni kifaaa cha plastiki kinachowekwa kwenye uterus.

Tiba Ya Fibroids Kwa Upasuaji

Kama dawa zimeshindwa kufanya kazi, mgonjwa hufanyiwa upasuaji kwa moja ya njia zifuatazo:

Hysterectomy– Kuondoa uterus. Hii hufanywa pale fibroids zinapokuwa kubwa sana au pale ambapo mgonjwa anatokwa na damu nyingi sana. Upasuaji huu una madhara ya aina mbili: 1. Kupunguza hamu ya kufanya mapenzi 2. Kukoma hedhi mapema

Myomectomy– Fibroids kuondolewa kutoka wenye ukuta wa uterus. Hii hufanyika pale ambapo mgonjwa anapenda kuendelea kuzaa. Tiba hii haoifanywi kwa fibroids kubwa au zile ambazo kwenye maeneo nyeti ya uterus.

tiba ya fibroids

Endometrial ablation: Kuondoa wa ngozi laini ya ndani ya uterus.

UAE (Uterine Artery Embolization): Hii ni kuzuia fibroids zisipate damu na hivyo kunyauka. UAE hufanywa kwa fibroids kubwa.

Magnetic-resonance-guided percutaneous laser ablation: Sindano nyembamba hupenyezwa kupitia ngozi hadi kulifikia fibroid. Fibroid humulikwa na mionzi ya laser kupitia waya fiber-optic uliopitishwa kwenye sindano na kulinyausha Fibroid.

Magnetic-resonance-guided focused ultrasound surgery: Kifaa maalumu hutumika kugundua eneo la fibroid, kisha mawimbi ya sauti huelekezwa kwenye fibroid. Mawimbi hayo hulinyausha fibroid.

Katika mada ya leo tumeona fibroids ni nini, chanzo cha fibroids, dalili zake, aina za fibroids na tiba zinazotumika kuondoa fibroids. Mategemeo yetu ni kwamba umeielewa vizuri mada hii, lakini endapo bado una swali lo lote kuhusu somo letu la leo, usisite kutuuliza. Katika mada nyingine tutazungumzia tatizo la mwanamke kutoa uchafu ukeni.

Una Tatizo la Fibroids?

Kwa maelezo zaidi na ya kina au kupata msaada, tuma ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au tutumie  barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu ndani ya saa za kazi kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.