Madhara Ya Unene Wa Kuzidi (Obesity)

madhara ya unene

Watu wengi sana wanatafuta njia za kuweza kupunguza uzito wa miili yao au kwa maneno mengine, watu wengi wanene hutumia njia mbalimbali ili wawe wembamba. Kutokana na hilo, watu wengi wanajitokeza na kujipatia fedha kwa kudai kuwasaidia watu hao katika kupunguza uzito wa miili yao. Kwetu hapa Tanzania, njia zinazotumika ni dawa za asili (hapa namaanisha dawa zilizotengenezwa hapa hapa kienyeji au mitishamba) na dawa zilizoletwa na makampuni mbalimbali ya nje ya nchi, zikiwemo za asili na za kemikali. Kila mmoja aliyetumia dawa hizo amekuwa na maoni tofauti, wapo walioridhika na matokeo na wapo ambao waliona dawa hizo hazikuwafaa.

Katika kutumia dawa hizo yapo mambo ambayo yanapaswa kutazamwa, si tu kupungua au kutopungua uzito bali na matokeo mengine ambayo yanasababishwa na matumizi ya dawa hizo (side effects). Najua hakuna aliyechukua hatua ya kufanya utafiti huo, lakini kitu cho chote unachotumia huwa na matokeo mengine mengi ambayo hayakuwa yamekusudiwa.

Dunia yetu ya sasa inakuwa na idadi kubwa ya watu walio na unene wa kupindukia kuliko wakati mwingine wo wote katika historia yake. Unene wa kupindukia sasa hivi ni tatizo la dunia nzima. Unene wa kupindukia hutokana na kula zaidi (hasa chakula kisichofaa kiafya – fast foods na junk foods) na kutofanya mazoezi ya kutosha.

Dunia yetu ya sasa ina uwingi wa chakula cha bei ya chini, chakula chenye kalori nyingi (fast foods na junk foods), chakula kinachotengenezwa kikiwa na chumvi, sukari na mafuta mengi, maisha yanayozidi kumfanya mtu asiushughulishe mwili wake, kuishi mjini na njia rahisi za usafiri, kwa hiyo tatizo hili si kitu cha ajabu.

Nchi zote zinafanya tafiti ili kuondoa tatizo la unene wa kupidukia kwa watu wazima na watoto. Pamoja na tahadhari zinazotolewa, tatizo linazidi kukua kwa kasi kwenye nchi zote, zilizoendelea na zinazoendelea.

Njia Sahihi Za Kupunguza Uzito

Pamoja na kwamba kuna mambo mengi yanayotajwa na kutumika kama njia za kupunguza uzito, kiutaalamu yote yanalenga kupunguza mafuta (fat) mwilini. Hivyo basi njia sahihi za kupunguza uzito huo ni mbili. Ya kwanza ni kuwa na mpango maalumu kuhusu chakula na namna unavyokula na ya pili ni kufanya mazoezi ili kupunguza mafuta yaliyojazana chini ya ngozi (adipose tissues) na kwenye maeneo mengine ya mwili. Katika kufanya hayo yote, inabidi kuwa na malengo katika kupunguza uzito wako. Kuna kiwango cha chini cha uzito ambacho kila mtu inafaa awe nacho kulingana na umri, jinsia  na urefu alio nao. Kupunguza uzito chini ya kiwango hicho kunaweza kuleta matatizo mengine ya afya baadaye. Inafaa basi kabla ya yote kujua unataka kupunguza uzito kwa kiasi gani.

Body Mass Index – BMI

 

BMi ni njia rahisi na isiyo na gharama ya kujitambua uko kwenye kundi gani kati ya uzito mdogo (underweight), uzito unaofaa (healthy weight), uzito mkubwa (overweight), au uzito mkubwa wa kupindukia (obesity). BMI hupatikana kwa kugawanya uzito wako katika kilo kwa mraba wa urefu wako katika mita.

Kwa kukurahisishia, tumia jedwali lililokwisha andaliwa hapa chini. Kwa hiyo, tazama urefu wako katika mita na kisha ni uzito wa chini na wa juu kabisa ambao unaotakiwa kuwa nao. Hili ni eneo la rangi ya kijani katka jedwali hili. Hapo sasa umejua unatakiwa kupunguza au kuongeza  kilo ngapi.

Eneo la njano linaashiria kuwa una uzito mkubwa kuliko kiasi na eneo la bluu ni ishara ya tatizo la kiafya kutokana na uzito wa kupindukia.

Watu wengi hufikiria kuwa unene wa kupindukia ni suala la mwonekano tu. Ukweli ni kwamba unene wa kupindukia ni tatizo kubwa kwa sababu linaweza kuiathiri afya yako kwa kiwango kikubwa sana.

Waist-to-hip Ratio (WHR)

Utafiti umeonyesha kuwa kipimo kikubwa cha waist-to-hip ratio kinaashiria uwezekano mkubwa zaidi wa unene wa kuzidi unaoitwa central obesity au apple shape abdominal obesity.

madhara ya unene

 

Kuna mamia ya jeni zinazohusika katika unene lakini wanasayansi wamegundua kuwa jeni moja iitwayo SNX10 ndiyo inayohusika na unene uletao magonjwa ikiwa ni pamoja na magonjwa ya moyo. diabetes type 2 na kiharusi.

Waist-to-hip ratio ni kipimo cha kuonyesha uwiano wa mzingo wa kiumo na mzingo wa nyonga. WHR inaashiria uwingi wa mafuta yanaypzunguka viungo vya maeneo ya tumbo sehemu ya ndani kabisa ya tumbo (visceral fat) na hutengeneza kemikali na homoni ambazo zinanweza kuwa sumu kwa mwili. Visceral fat huzunguka viungo vya ndani ya tumbo wakati subcutaneous fat hujenga chini ya ngozi.

Kiwango cha chini ya 0.99 kwa wanaume na 0.90 kwa wanawake huchukuliwa kuwa ni salama.

Baadhi ya matatizo ya kiafya yatokanayo na unene ni kama:

Upumuaji kusimama wakati umelala – Sleep apnea

Kusimama upumuaji kwa vipindi vifupi ukiwa umelela ni kitu cha kawaida. Lakini kusimama kwa upumuaji kukitokea mara kwa mara au kwa vipindi virefu, huwa ni tatizo ambalo huitwa sleep apnea. Mtu akiwa na sleep apnea kiwango cha oksijeni katika mwili hupungua na usingizi hukatishwakatishwa.

Sleep apnea ni tatizo haswa la watu wanene. Inasadikika kuwa njia ya hewa ya watu wanene hupunguzwa na tonsils kubwa, ulimi mkubwa na kuongezeka kwa mafuta katika eneo la shingo, vyote vikisukuma njia ya hewa wakati misuli ya koo ikiwa imelegea kwa usingizi. Mzingo wa shingo ndicho kipimo cha sleep apnea. Mzingo (circumference) wa shingo ya mwanamme mnene unaozidi nchi 17, na wanawake wenye mzingo wa shingo unaozidi nchi 16, wapo kwenye hatari kubwa ya kupatwa na sleep apnea.

Sleep apnea husababisha mtu asinzie mchana, hupunguza kiwango cha oksijeni ndani ya damu na kuifanya damu kuwa ya mnato, hali inayoongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo na kiharusi.

Kisukari

Utafiti zimeonyesha kuwa mafuta katika tumbo husababisha seli za mafuta kutoa kemikali “pro-inflammatory chemicals”, ambazo zinaweza kuufanya mwili usiisikie insulin kwa kuvuruga utendaji kazi na uwezo wa seli za kuipokea insulin. Hali hii huitwa insulin resistance – chanzo cha kisukari – type 2 diabetes. Kuwa na mafuta mengi kwenye tumbo (kuwa na kiuno kikubwa) huitwa central au abdominal obesity, aina ya unene wenye hatari kubwa.

Mafuta mengi na Maini yenye mafuta – high blood lipids & fatty liver

Kuwa na unene mkubwa kunakuweka kwenye hatari ya kuwa na viwango vikubwa vya cholesterol. Ukiwa na unene wa kupindukia, viwango vya triglycerides na LDL (bad cholesterol) huwa juu na HDL (good cholesterol) huwa chini.

Mwili wako ukiitunza sukari, hugeuka na kuwa triglycerides ambayo hutunzwa kama LDL katika maini.

Magonjwa ya moyo

Kuwa na BMI kubwa kunachangia tatizo la high blood pressure kwa asilimia 30. Tafiti zimeonyesha kuwa watu wenye BMI kubwa zaidi ya 30 wanaishi maisha mafupi zaidi ukilinganisha na wale wenye BMI za viwango vizuri. Unene wa kupindukia, na hasa wa matumbo (central au abdominal obesity) unaongeza yamkini ya kupatwa na  magonjwa ya moyo.

Osteoarthritis na gout

Osteoarthritis ni tatizo la kawaida la joint ambalo hushambulia zaidi magoti, nyonga, au mgongo. Kubeba uzito wa ziada huogeza msukumo kwenye viungo hivi na kufanya gegedu (cartilage) isagike. Kwa namna ambavyo joint ya goti inavyofanya kazi, madhara ya uzito wa ziada yanaweza kuwa mara nne au mara tano ya yale yatokanayo na uzito wa kawaida.

Gout ni ugonjwa unaoathiri joints. Gout inatokea pale kunapokuwa na uric acid nyingi zaidi katika damu. Tindikali ya ziada hutengeneza chembechembe ambazo hutuama kwenye joints. Gout huonekana zaidi baina ya watu waenye unene wa kuzidi. Unavyozidi kuwa mnene ziadi ndivyo hatari ya gout inavyoongezeka.

Unene wa kupindukia huongeza uwezekano wa kupata gout mara mbili. Na kuwa na unene zaidi – na hasa maeneo ya kati – huleta tatizo la mwili kutoisikia insulin – insulin resistance. Insulin ikizunguka mwilini kwa wingi huzuia figo zisiitoe uric acid.

Usisite kutoa maoni yako au kuuliza maswali kuhusiana na mada yetu ya leo.

Katika mada yetu ifuatayo, tutazungumzia kuhusu njia sahihi za kupunguza unene.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya muda wa kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.