
Mawe ya nyongo ni vipande vya nyongo yenye ukolezi mkubwa iliyoganda na kuwa vigumu vinavyotokea ndani ya mfuko wa nyongo au katika mirija ya nyongo. Neno “Gall” lina maana ya nyongo, kwa hiyo, gallstones ni mawe yaliyomo katika kibofu cha nyongo. Kibofu cha nyongo hukusanya na kutunza nyongo kwa ajili ya matumizi ya baadaye. Maini hutengeneza nyongo na mirija ya nyongo husambaza nyongo kwenye viungo tofauti. Watu wa tiba mara nyingine hutumia neno “cholelithiasis” kuelezea hali ya kuwa na mawe kwenye nyongo. “Chole” ni neno lenye maana ya nyongo, na “lithiasis” maana yake ni kujijenga kwa mawe. Mawe ya nyongo hutokea wakati masimbi ya nyongo yanapojikusanya na kuganda. Masimbi haya kwa kawaida ni uzidifu wa moja ya viambato muhimu katika nyongo.
Mawe katika nyongo (cholelithiasis) si lazima yakusababishie matatizo. Watu wengi wana mawe katika nyongo na hawajui. Lakini mawe katika kibofu cha nyongo yanaweza kuwa hatari pale yakianza kusafiri kupitia mkondo wa nyongo na kukwama sehemu nyingine. Mawe kwenye nyongo yanaweza kuziba mkondo wa nyongo, na kusababisha maumivu na matatizo mengine ya kiafya.
Shida ya mawe ya nyongo ni kwamba yanaongezeka ukubwa-taratibu, lakini kiuhakika-wakati nyongo ikipita juu yao na kuacha tabaka jipya la masimbi. Jiwe linaloanza kama punje ya mchanga linaweza kukua kiasi cha kuziba mtiririko wa nyongo, hasa likipita sehemu nyembamba, kama kwenye mrija wa nyongo au kwenye shingo ya mfuko wa nyongo.
Vitu Vinavyochangia Kupata Mawe Ya Nyongo
. Umri. Mawe ya kwenye nyongo huchukua muda mrefu kukua na kufikia kuanza kuziba njia za nyongo. Wanaume mara nyingi hupata tatizo hili wakiwa na miaka zaidi ya 60. Wanawake wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata tatizo wakiwa kwenye umri wao wa kuzaa yaani miaka 20 hadi 50.
. Homoni. Uwezekano wa kupata mawe katika nyongo kwa wanawake ni mara tatu zaidi ya ule wa wanaume. Uwezekano hupanda na kushuka kulingana na homoni za estrogen na progesterone. Estrogen huongeza viwango vya cholesterol, wakti progesterone hupunguza kasi ya mfuko wa nyongo ya kukamua nyongo.
. Uzito wa mwili. Mafuta ya mwili hutoa estrogen, kwa hiyo kuwa na mafuta mengi hupandisha kiwango cha mwili cha estrogen na kiwango cha cholesterol. Kwa upanade mwingine, kupunguza uzito ghafla, kama kwa upasuaji wa kupunguza mwili, kunaweza kuzalisha mawe katika nyongo. Kupungua mwili ghafla kunatoa kiasi kikubwa cha cholesterol ndani ya kibofu cha nyongo.
. Urithi. Kama kuna historia ya ugonjwa wa mawe katika nyongo katika familia yako, unaweza pia kupata tatizo hili.
. Sababu za kiafya kama unene wa kupindukia, Crohn’s disease, cirrhosis na sickle cell anemia
. Maambukizo katika mfuko wa nyongo
. Kula chakula chenye uwingi wa mafuta au cholesterol na kukosa fiber
. Ujauzito
. Matumizi ya madawa yenye estrogen nyingi, kama dawa za uzazi wa mpango

Dalili Za Mawe Kwenye Nyongo
Mawe ya nyongo hayaleti dalili zo zote hadi pale yatakapokwama na kuziba eeno fulani. Kuziba huku kutaleta dalili, na mara nyingi ni maumivu ya sehemu ya juu ya tumbo na kichefuchefu. Ni hali inayoweza kuja na kuondoka, au ikaja na kuendelea. Kama kuziba ni kubaya sana au kukiendelea kwa muda mrefu sana, unaweza kuona dalili zifuatazo:
. Kutoa jasho
. Homa
. Mapigo ya moyo ya haraka
. Kuvimba tumbo na maumivu likiguswa
. Rangi ya njano kwenye macho na ngozi
. Mkojo mweusi na mabadiliko ya rangi ya haja kubwa.
Maumivu Ya Mawe ya Figo Husikika Wapi?
Mfumo wa nyongo unapataikana sehemiu ya juu ya tumbo ya upande wa kulia, sehmu ambayo ni chini ya kizimba cha mmbavu. Watu wengi husikia maumivu ya mawe ya nyongo kwenye eneo hilo. lakini wakati mwingine huweza kusambaa maeneo mengine. Watu wengine huyasikia kwenye mkono wa kulia au bega au mgongoni katikati ya mabega.
Watu wengine husikia maumivu ya mawe katika nyongo katikati ya matumbo au vifua. Hii inaweza kuchanganya kawa sababu itafanana na dalili za magonjwa mengine. Watu wengine huchanganya maumivu ya mawe ya nyongo na kiungulia. Watu wengine huona kama wana heart attack.
Maumivu ya mawe ya kwenye nyongo yana maana kuwa jiwe limekwama katika mkondo wa nyongo na kuziba. Kama ni kuziba kukubwa, utasikia maumivu mara moja. Kama kuziba ni kwa kiasi, hutasikia maumivu hadi pale mfuko wa nyongo utakapojikaza (utakapojiminya), na kuongeza msukumo kwenye mfumo. Kula ndiko kunakosababisha mfuko wa nyongo kujikamua.
Mlo mkubwa, wenye mafuta mengi utasababisha mfuko wa nyongo kujikamua kwa nguvu zaidi. Hii ni kwa sababu utmbo wako mdodgo utagundua uwepo mkubwa wa mafuta katika mlo wako na kuutarifu mfuko wa nyongo kiasi gani cha nyongo kihitajika ili kukivunjavunja chakula hicho. Mfuko wa nyongo huitika kwa kujikamua na kutoa nyongo inayotakiwa.
Madhara Yatokanayo Na Mawe Katika Nyongo
Endapo mawe ya nyongo yataziba mtiririko wa nyongo katika mfumo wa nyongo, viungo vyote vya mfumo huo vinaweza kuathirika. Nyongo inaweza kujazana ndani ya njia za nyongo na viungo vingine, na kusababisha uvimbe na kuruhusu maambukizo ya bakteria. Hali ikizidi, maisha yanaweza kuwa hatarini.
Madhara yafuatayo ynaweza kutokea:
. Cholecystitis (gallbladder inflammation)
. Pancreatitis (pancreas inflammation)
. Cholangitis (bile duct inflammation)
. Hepatitis (liver inflammation)
. Jaundice (bile in your bloodstream)
. Septicemia (an infection in your bloodstream).
Mawe Kwenye Nyongo Husababishwa Na Nini?

Mawe ndani ya kibofu cha nyongo hutokea wakati kuna uzidifu wa moja kati ya viambato muhimu katika nyongo. Viambato vilivyozidi hugeuka kuwa masimbi na kutuama chini kwenye kibofu cha nyongo au mirija ya nyongo, na masimbi haya taratibu huganda na kugeuka kuwa mawe. Mawe ya cholesterol ndiyo huonekana kwa wingi zaidi. Mawe ya bilirubin ni aina nyingine inayoonekana.
Sababu nyingi zinachangia katika kutokea kwa mawe ya nyongo:
. Kuzidi kwa cholesterol. Kwa kawaida nyongo ina kemikali za kutosha kuiyeyusha cholesterol inayotolewa na maini. Lakini ikiwa cholesterol inayotolewa na maini inakuwa nyingi kuliko uwezo wa kuyeyushwa na nyongo, ile cholesterol
ya nyongeza huganda na baadaye kuwa mawe.
. Kuzidi kwa bilirubin. Bilirubin ni kemikali inayotokea pale mwili unapovunjavunja chembechembe nyekundu za damu zilizozeeka. Kuna hali ambazo husababisha maini kutengeneza bilirubin kupita kiasi, pamoja na liver cirrhosis, maambukizo kwenye mkondo wa nyongo na baadhi ya magonjwa ya damu. Bilirubin hii ya ziada huchangia katika kujenga mawe katika nyongo.
. Upungufu wa bile acids (bile salts). Baadhi ya magonjwa husababisha bile acid malabsorption, maana yake unapoteza bile acids kupitia haja kubwa. Ikiwa unapoteza nyingi sana, maini hayatakuwa na bile acids ya kutosha kutengeneza nyongo. Upungufu wa bile acids hutengeneza uzidifu wa lipids (cholesterol) katika nyongo.
. Cholestasis or gallbladder stasis. “Stasis” maana yake kutokufanya kitu (inactivity). Kama mirija ya nyongo au mfuko wa nyongo haupitishi nyongo kama inavyotakiwa, kuna uwezekano mkubwa wa nyongo kutengeneza masimbi. Hali hii inaweza kutokan na misuli au ishara za kikemikali za kuiamuru kufanya kazi.
. Mfuko wa nyongo haumwagi nyongo inavyotakiwa. Kama mfuko wa nyongo hautoi nyongo yote au haautoi mara nyingi, nyongo inaweza kuwa na ukolezi mkubwa na kuchangia katika ujenzi wa mawe ya nyongo.
Aina Za Mawe ya Nyongo
Mawe yanayoweza kutengenezwa katika kibofu cha nyongo ni ya aina mbili:

. Cholesterol gallstones
. Pigment gallstones
Katika mada yetu nyingine tutazungumzia ugonjwa wa homa ya ini. Usisite kutoa maoni yako kuhusu uandishi wa mada hii ya leo. Tutafurahi kusikia toka kwako.
Tiba Ya Mawe Ya Nyongo
Kama mawe ya nyongo hayakuletei shida, huhitaji kupata tiba. Lakini kama mawe ya kwenye nyongo yataziba, daktari atashauri kuyaondoa.
Watu wengi wenye shida ya mawe kwenye nyongo hufanyiwa upasuaji. Upasuaji ndiyo njia pekee ya kuhakikisha kuwa mawe kwenye nyongo hayatakusumbua tena. Lakini huhitaji kufanyiwa upasuaji, kuna njia nyingine za kukusaidia, ikiwa ni pamoja na dawa.
Upasuaji wa kuondoa kibofu cha nyongo (cholecystectomy) ndiyo njia ya uhakika ya tatizo la mawe kwenye nyongo. Ni njia itumikayo duania nzima, na mara nyingi kama laparoscopic surgery. Unaweza kuishi vizuri bila kifuko cha nyongo. Kuanzia sasa, nyongo itatiririka moja kwa moja kutoka kwenye maini hadi utumbo mwembamba.
Mara chache hutokea kuwa watu wanaotakiwa kufanyiwa upasuaji wa kuondoa kibofu cha nyongo hawapo katika hali nzuri ya kufanyiwa upasuaji huu. Hapa sasa, cholecystostomy hufanyika ambao ni upasuaji mdogo wa kuweka catheter ndani yamfuko wa nyongo ili kutiririsha nyongo.

Upasuaji huu unaweza kuondoa mawe yaliyomo ndani ya kibofu cha nyongo.
Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya saa za kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.