Mshituko wa moyo hutokea pale mtiririko wa damu kuelekea kwenye moyo unapozibwa. Mara nyingi kuziba huku hutokana na kujikusanya kwa mafuta, cholesterol na vitu vingine, ambavyo hufanya utando ndani ya ateri zinazopeleka damu kwenye moyo (coronary arteries). Mara nyingine utando huu hubomoka na kufanya donge la damu linaloziba mtiririko wa damu. Kuziba huku kwa damu kunaweza kuharibu sehemu ya musuli wa moyo. Hapa chini tutaeleza dalili za mshituko wa moyo, chanzo cha mshituko wa moyo na nini ukifanye ili kuzuia mshituko wa moyo. Mshtuko wa moyo, ambao kitaalamu huitwa myocardial infarction, unaweza kuua, lakini siku za karibuni tiba yake imeboreshwa. Ni muhimu kupiga 911 au namba ya dharula endapo unahisi unanyemelewa na mshtuko wa moyo.
Dalili Za Mshituko Wa Moyo
Dalili za kawaida za mshituko wa moyo ni pamoja na:
. Pressure, kubana kifua, maumivu, na kubana au kuwashwa kifuani na mikononi kunakoweza kuenea hadi maeneo ya shingo, taya au mgongoni
. Kichefu, kuvimbiwa, kiungulia au maumivu ya tumbo
. Kuhema kwa shida
. Jasho baridi
. Uchovu
. Kizunguzungu cha ghafla
Dalili Za Mshituko Wa Moyo Hutofautiana
Si watu wote wanaopata mshituko wanapata dalili zile zile au za uzito ule ule. Wengi hupata maumivu ya kiasi, wengine maumivu makali. Wengine hawaoni dalili zo zote. Kwa baadhi yao, dalili ya kwanza ni moyo kusimama kufanya kazi.
Mashituko wa moyo mara nyingine huja ghafla, lakini kwa watu walio wengi, dalili huonekana saa, siku au hata wiki kadhaa kabla. Dalili ya wawali kabisa yaweza kuwa maumivu kifuani yanayojirudia (angina) yanayoanza unapokuwa na shughuli na kuacha ukipumzika. Angina husababishwa na kupungua kwa muda mfupi kwa mtiririko wa damu kwenye moyo.
Nini Cha Kufanya Kama Unaona Mtu Amepatwa na Mshituko Wa Moyo
Kama uamwona mtu amepoteza fahamu na unahisi amepata mshituko wa moyo, kwanza piga simu kuomba msaada wa dharula. Kisha chunguza kama anapumua na ana mapigo ya moyo. Kama hapumui na hana mapigo ya moyo, mpe huduma ya CPR.
Sukuma kwa nguvu na kwa haraka juu ya kifua chake ukitumia misukumo ya haraka inayolingana – kama misukumo 100 hadi 120 kwa dakika.
Chanzo Cha Mshituko Wa Moyo
Mshituko wa moyo unatokea wakati ateri moja au zaidi ya moja ya kupeleka damu kwenye moyo inapoziba. Muda ukienda, mafuta ikiwa ni pamoja na cholesterol, hujijenga na kutengeneza plaque, ambayo itapunguza kipenyo cha ateri (atherosclerosis). Hali hii, iitwayo ugonjwa wa ateri za moyo (coronary artery disease), ndicho chanzo cha mishituko ya moyo iliyo mingi.
Wakati mshituko unapotokea, plaque inaweza kuwa imebomoka na kumwaga cholesterol na vitu vingine ndani ya mkondo wa damu. Donge la damu hutokea eneo plaque ilipobomoka. Endapo donge hilo ni kubwa, linaweza kuziba mtiririko wa damu ndani ya ateri, na kuufanya moyo ukose oksijeni na virutubishi (ischemia).
Unaweza kuwa na tatizo la mishipa kuziba kiasi au kuziba kabisa.
. Ikiziba kabisa una ST elevation myocardial infarction (STEMI).
. Ikiziba kiasi una non-ST elevation myocardial infarction (NSTEMI).
Uchunguzi na tiba hutofautiana kulingana na aina ya tatizo ulilo nalo.
Sababu nyingine ya mshituko wa moyo ni kukaza kwa ghafla kwa mshipa wa damu unaoelekea kwenye moyo (spasm of a coronary artery) ambako kutazuia damu isifike kwenye eneo fulani la musuli wa moyo. Matumizi ya tumbako na madawa ya kulevya, kama cocaine, huweza kusababisha hali hii inayotishia maisha.
Maambukizi ya COVID-19 huweza kuuharibu moyo kufikia hali inayoweza kusababisha mshituko wa moyo.
Katika mada nyingine katika tovuti yetu, tutauona ugonjwa wa kiharusi (stroke). Usisite kutoa maoni yako au kuuliza maswali uliyo nayo kuhusu mada hii ya leo.
Pata ushauri zaidi kwa kututumia ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au kututumia barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.