Mshtuko Wa Moyo Na Kufeli Kwa Moyo. Tofauti Ni Nini?

 

 

Moyo ni kiungo muhimu cha mwili kinachofanya kazi ya kusukuma damu ili izifikie sehemu zote za mwili. Kama mwili hauna uwezo wa kufanya hivyo, matatizo makubwa ya kiafya yatatokea. Watu wengi huchanganya kati ya mshtuko wa moyo na moyo kufeli. Mshtuko wa moyo hutokea wakati ghafla kuna hitilafu katika usambazaji wa damu kutoka kwenye moyo wakati kufeli kwa moyo ni hali ya moyo kushindwa kusukuma damu vizuri.

Mada yetu ya leo ni uchambuzi wa tofauti zilizopo kati ya mshtuko wa moyo na moyo kufeli. Tutaelezea dalili, sababu na tiba zinazotolewa kwa kila moja ya matatizo hayo mawili.

Moyo ni pampu inayoundwa na misuli wenye kazi ya kusambaza damu kwenye tishu zote za mwili. Ni kazi ya lazima kwa uhai kwa sbabu bila mtiririko wa damu wa damu mpya kila wakati, seli hazitafanya kazi vizuri na baadaye zitakufa.

Hivyo, ni lazima kutunza afya ya moyo na kujlinda na magonjwa ambayo yanaweza kuathiri utendaji kazi wa moyo.

Mshtuko wa moyo (heart attack au myocardial infarction) ni hali ambapo ghafla kuna upungufu wa damu inayoelekea kwenye sehemu fulani ya moyo. Mara nyingi hii hutokana na kuzibwa kwa mtirirko wa kawaida wa damu. Endapo mtiririkowa damu hautarudi kwenye hali yake ya kawaida, sehemu fulani ya moyo itaanza kufa.

Kufeli kwa moyo (heart failure au congestive heart failure) ni  hali ya moyo kushindwa kusukuma damu kwa kiwango cha kutosha kusambaa mwilini. Hii inaweza kutokana na moyo kutojaa damu ya kutosha au moyo kuwa dhaifu na kushindwa kusukuma damu vizuri. Ifahamike kuwa kufeli kwa moyo hakumaanishi kusimama kwa moyo.

 

Chanzo Cha Mshtuko Wa Moyo

 

Mshtuko wa moyo au shambulio la moyo linaweza kusababishwa na vitu vingi. Lakini mara nyingi sababu kuu ni ugonjwa wa coronary artery disease. Ugonjwa huu hutokea wakati ateri zilizo juu ya misuli ya moyo (coronary arteries) ambazo husambaza damu yenye uwingi wa oksijeni kwenye moyo hupungua kipenyo au kuziba baada ya kujazana kwa plaque. kipenyo cha mishipa hii kikipungua, damu hupita kwa shida kuelekea kwenye moyo.

Kujikaza kwa ghafla kwa mishipa ya coronary (coronary artery spasm) huweza pia kusababisha shambulio la moyo. Hii ni pale kunapotokea mishipa hiyo iliyopo kwenye misuli ya moyo kujipana ghafla.

 

Chanzo Cha Moyo Kufeli

 

Kuna sababu nyingi pia zinazoweza kuchangia kufeli kwa moyo. Kwa kawaida, moyo hufeli kutoakana na sababu nyingine za kiafya zinazoufanya moyo kufanya kazi zaidi, au kuumia au mashambulizi ya vijidudu yanayoleta uharibifu kwenye moyo. Kufeli kwa moyo kunaweza kuhusisha pande zote, upand wa kushoto au wa kulia. Upande wa kushoto unasukuma damu yenye uwingi wa oksijeni kwenda kwenye mwili, wakati upande wa kulia unakusanya damu yenye oksijeni kidogo na kuisukuma kwenda kwenye mapafu ili ikapate oksijeni.

Ni kawaida sana kufeli kwa moyo kuuhusisha upande wa kushoto. Kuna aina mbili za kufeli kwa moyo zinazotokea upande wa kushoto: reduced ejection fraction na preserved ejection fraction.

Reduced ejection fraction, kwa jina jingine asystolic heart failure, ni wakati moyo haukazi kikamilifu. Hii inaweza ikatokana na:

. ugonjwa wa coronary artery
. genetic cardiomyopathy – ugonjwa wa misuli ya moyo unaotokana na vinasaba kama, dilated cardiomyopathy na hypertrophic cardiomyopathy
. hitilafu katika valvu za moyo
. mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida
. matatizo ya moyo yatokanayo na hitilafu nyingine za mwili
. pombe
. cocaine, methamphetamine, au sumu nyingine.

Preserved ejection fraction, au kwa jina jingine diastolic heart failure ni wakati moyo unakuwa mgumu mno ili kukaza inavyotakiwa. Hii ina maana kuwa hauruhusu damu kujaa inavyotakiwa, kwa hiyo unasukuma kiasi kidogo kwenda mwilini. Hii inaweza kusababishwa na:

. high blood pressure
. unene
. kisukari

Kufeli kwa moyo upande wa kulia, ni moyo kushindwa kusukuma damu ya kutosha kwenda kwenye mapafu ili ikapate oksijeni ya kutosha. Mara nyingi hali hii hutokana na kufeli kwa moyo upande wa kushoto. Nayo hutokana na kujikusanya kwa damu, kupanda kwa pressure ya damu ndani ya mishipa ya damu inayosafirisha damu kutoka kwenye moyo kuelekea kwenye mapafu.

 

Dalili Za Mshtuko Wa Moyo

Mshtuko wa moyo hauji kila wakati na dalili zinazojibainisha. Mshtuko huu usio na dalili za waziwazi huitwa silent heart attack. Dalili za shambulio la moyo huwa tofauti kutoka mtu hadi mwingine. Mtu ambaye alishawahi kushikwa kabla huonyesha dalili za tofauti. Dalili zinazoonekana mara nyingi ni:

. maumivu kwenye kifua
. kutojisikia vizuri kwenye mikono, mabega, shingo, taya au tumboni
. matatizo ya upumuaji

Dalili nyingine zaweza kuwa:

. kutokwa jasho
. uchovu
. kichefuchefu na kutapika
. kizunguzungu cha ghafla

 

Dalili Za Kufeli Kwa Moyo

 

. Dalili za kufeli kwa moyo zinategemea aina na hali iliyofikiwa. Kushindwa kupumua vizuri ni dallili ya kawaida ya kufeli kwa moyo kwa upande wa kulia au wa kushoto. Dalili zitaongezeka kadiri moyo utakavyokuwa dhaifu zaidi.

Dalili za kufeli kwa moyo upande wa kushoto zinaweza kuwa ni pamoja na:

. udhaifu kwa ujumla
. shida kupumua
. kukosa usingizi
. kushindwa kutuliza akili
. kukohoa
. uchovu
. rangi ya bluu kwenye vidole na kwenye midomo
. shida kulala chali

Dalili za kufeli kwa moyo upande wa kulia zinaweza kuwa ni pamoja na:

. kuvimba
. kunenepa
. kichefuchefu
. kukosa hamu ya kula
. maumivu ya tumbo
. haja ndogo ya mra kwa mara

 

Tiba Ya Mshtuko Wa Moyo

 

Kuwahi kutoa tiba ya mshtuko wa moyo kunaweza kusaidia kuzuia au kupunguza madhara kwenye misuli ya moyo. Baada ya kuligundua tatizo, daktari anaweza kujaribu kurudisha mtirirko wa damu kwa kuondoa au kupunguza kuzibwa kwa damu. Anaweza kutumia dawa au kufanya coronary angioplasty.

Coronary angioplasty ni utaratibu wa tiba ambao unatumia namna ya kijiputo kufungua ateri na kurudisha mtiririko wa damu. Daktari anaweza pia kijibomba chenye matundu kiitwacho stent ili kuifungua ateri.

 

 

Daktari anaweza pia kutoa dawa za kupunguza kuganga kwa damu, kupunguza pressure, ili kuupunguzia moyo mzigo.

Tiba Ya Moyo Kufeli

 

Tatizo la kufeli kwa moyo halina dawa, lakini mgonjwa anaweza kusaidiwa aishi muda mrefu zaidi bila kusumbuliwa mara kwa mara. Mgonjwa tapewa tiba kulingana na aina ya tatizo, alkini kwa ujumla itahusu mabadiliko ya staili ya kuishi, dawa na mara nyingine upasuaji.

 

Katika ukurasa wetu mwingine tatalijadili tatizo la   chembe ya moyo. Usisite kutoa maoni yako au kutuuliza maswali kuhusiana na mada yetu hii ya leo.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.