Mazoezi ya Kegel ni mazozezi ambayo mtu huweza kuyafanya wakati wowote ule yakiwa na lengo la kuimarisha misuli inayotanda kuanzia kwenye kinena hadi kunako mwisho wa uti wa mgongo, ikiwa katikati ya miguu. Hii ndiyo misuli inayoshikilia kibofu cha mkojo, utumbo mwembamba, nyumba ya uzazi (uterus) na sehemu ya kutolea haja kubwa. Mazoezi hawa yanafanana kabisa na mazoezi ya misuli ya Pelvic foor ambayo nimeyaelezea katika ukurasa tofauti. Mara nyingi majina ya mazoezi haya huchanganywa hivyo mazoezi ya kegel yakaitwa mazoezi misuli ya pelvic floor.
Faida Za Mazoezi Ya Kegel
Faida za kufanya mazoezi haya ni zile zile nilizozielezea kwenye mazoezi ya misuli ya pelvic floor. Kwa kifupi ni kuzuia mkojo usitoke bila wewe mwenyewe kukusudia hasa wakati ukikohoa, kucheka au kupiga chafya, kuzuia haja kubwa isitoke yenyewe na kuzuia hali ya kutaka kukojoa tena mara tu baada ya kukojoa kiasi kikubwa cha mkojo (urinary incontinence). Mazoezi haya husaidia pia afya ya uzazi kwa kuwasaidia wanawake wanaoshindwa kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa na huzisaidia jinsia zote kupata raha zaidi wakati wa kufika kileleni (increase the intensity of orgasm). Mazoezi ya Kegel yana faida nyingine ya kukaza misuli ya uke iliyolegea kwa sababu ya tendo la uzazi na kuufanya uke kuwa mdogo na unaobana.
Namna Ya Kufanya Mazoezi Ya Kegel
Kuijua misuli ya pelvic floor ambayo tunataka kuiimarisha au kuipa nguvu, jaribu kuuzuia mkojo ukiwa katikati ya tendo la kukojoa. Ukifanikiwa, chunguza misuli iliyokaza na kuachia – hiyo ndiyo misuli ya pelvic floor tunayoizungumzia hapa na tunayotaka kuipa nguvu. Hakikisha huna mkojo kabisa kisha fuata maelekezo ya mkanda (video) huu hapa chini. Tazama mkanda kwa kubofya juu ya eneo lenye picha.
Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: +255 655 858027 au +255 756 181651.