Mzunguko wa hedhi kwa kawaida hujirudia kila baada ya siku 24 hadi 28 kuanzia siku ya kwanza ya hedhi hadi siku ya kwanza ya hedhi ya mwezi unaofuata, na wastani kwa wengi ni siku 28. Katika mzunguko wa hedhi ulio wa kawaida mwanamke hupoteza wastani wa vijiko 2 hadi 3 (kama mililita 35 hadi 40) za damu katika kipindi cha siku 4 hadi 8. Hata hivyo, wanawake wengine hupoteza damu nyingi zaidi.Mwanamke akipoteza damu zaidi ya vijiko 5 hadi 6 (kama mililita 80) wakati wa hedhi, hii huitwa hedhi ndefu au hedhi nzito, kitaalamu menorrhagia-hedhi inayozidi siku saba au kutoka damu nyingi kunakolazimisha kutumia pedi zaidi ya moja kwa saa moja kwa mfululizo wa saa. Asilimia tano ya wanawake wana menorrhagia.
Katika ukurasa huu, tutalijadili tatizo la kutoka damu siku nyingi au kwa lugha nyingine, tatizo la kuwa na period ndefu.
Hedhi ndefu ni dalili ya tatizo la kiafya, kama matatizo ya:
. mabadiliko ya mpangilio wa homoni
. matatizo ya nyumba ya kizazi
. Saratani
Hedhi ndefu huweza kusababisha kukosa raha wakati wa hedhi au hata kuvuruga shughuli za kawaida. Hedhi ndefu yaweza pia kuvuruga usingizi wako. Hedhi ndefu huweza kusababisha upungufu wa madini ya chuma, na hasa hedhi hizo zikiwa nzito.
Dalili Za Kuwa Na Hedhi Nzito Au Hedhi Ndefu
Dalili za kuwa na menorrhagia zinaweza kuwa ni pamoja na:
. Kulowesha pedi moja au zaidi kila saa moja kwa saa kadhaa mfululizo
. Kuhitaji kutumia pedi mbili ili kudhibiti damu inayotoka
. Kuamka usiku kubadilisha pedi
. Kutoka damu kwa zaidi ya siku saba
. Kutoa vibonge vikubwa vya damu
. Kushindwa kuendesha vizuri shughuli zako za kila siku
. Dalili za upungufu wa damu, kama uchovu au kukosa pumzi
Nini Kinasababisha Kuwa Na Period Ndefu?
Hedhi ndefu ni matokeo ya hali nyingi zinazotokana na afya yako, umri wako na staili yako ya maisha. Baadhi zikiwa:
. Hormone imbalance: Katika mzunguko wa kawaida, uwiano mzuri kati ya homoni za estogen na progesterone husimamia ujenzi wa utando wa juu (endometrium) unaofunika nyumba za mimba (uterus), ambao hubanduka wakati wa hedhi. Kama uwiano si mzuri, utando huu hujengwa zaidi ya kiwango cha kawaida na kisha kuondolewa kwa hedhi nzito, maana yake, hedhi inayoambatana na kutoka kwa damu nyingi sana.
Kuna vipengele kadhaa vinavyoweza kusababisha hormone imbalance, ikiwa ni pamoja na polycystic ovary syndrome (PCOS), unene, insulin resistance na uvimbe (fibroids).
. Matatizo ya kiutendaji ya ovari. Kama ovari hazitatoa yai katika mzunguko wa hedhi (anovulation), mwili wako hautatengeneza homoni ya progesterone, kama vile wakati wa mzunguko wa kawaida. Hali husababisha hormone imbalance na kuleta menorrhagia.
Uterine fibroids: Uvimbe wa aina hii, ambao si wa saratani, hutokea kwenye umri wa kuzaa. Fibroids huweza kuleta hedhi nzito kuliko kawaida au hedhi zilizo ndefu kama ifuatavyo:
Fibroids zinaweza kusukuma juu ya ngozi laini ya juu ya mimba ya mimba na kusababisha kuvuja zaidi kwa damu.
Nyumba ya mimba itashindwa kujikamua vizuri na hivyo kusababisha damu kuendelea kuvuja
Fibroids huweza kuanzisha ukuaji wa vishipa vipya vya damu, vinavyochangia hedhi nzito au hedhi ndefu na matone ya damu katikati ya hedhi
Uwepo wa fibroids unaweza kusababisha kupanda kwa kiwango cha homoni ziitwazo prostaglandins na kunaongeza uzito wa hedhi
Hedhi nzito zinazotokana na fibroids zinategemea maeneo zilipo fibroids hizo, uwezo wa kujikamua wa nyumba ya uzazi, uwepo wa prostaglandins, na kuharibika kwa umbo la uterus.
Prostaglandins ni michanganyiko iliyomo ndani ya mwili inayoundwa na mafuta, inayofanya kzai kama za homoni.
Tofauti na homoni, prostaglandins hazitolewi na tezi fulani mahsusi badala yake mwili una tishu za aina tofauti zinazotengeneza prostaglandins.
Prostaglanding zina tabia za kuvutia kwa sababu zinaweza kuleta matokeo tofauti kulingana na vipokezi tofauti ambako zitajiambatanisha.
Baadhi ya matokeo ya uwepo wa prostaglandins ni kujikamua kwa misuli ya nyumba ya uzazi na usikivu wa maumivu n.k.
Utafiti wa kisayansi umetuwezesha hata kutengeneza prostaglandins bandia kwa ajili ya kutia uchungu (induce labor).
Polyps: Vitu vyenye maumbo madogo, visivyo na madhara, vinavyoota juu ya utando wa uterus vinaweza kusababisha hedhi nzito au hedhi inayokwenda siku nyingi.
Kama homoni zako haziko kwenye viwango vizuri au kama mwili wako hauachii yai katika mzunguko wako wa hedhi, ngozi laini (uterine lining) inayotanda juu ya nyumba ya uzazi huwa nene sana. Mwili wako baadaye unapoondoa utando huu, unaweza ukaona unapata siku nyingi zaidi za hedhi.
Madawa:Unaweza ukaingia period kwa siku nyingi kwa sababu ya dawa unazozitumia. Dawa hizi ni pamoja na:
. dawa za kuzuia mimba
. aspirin na blood thinners
. Anti-inflammatories.
Ujauzito: Kutoka damu kwa muda mrefu kunaweza pia kuwa ni ishara ya matatizo ya mimba, kama mimba iliyotungwa nje ya kizazi (ectopic pregancy) au kuharibika kwa mimba (miscarriage).
Unaweza kuwa na hedhi ndefu kwa sababu ya tatizo la placenta previa, placenta ya mtoto kuziba kwa kiasi fulani au kuziba kabisa cervix. Placenta previa inaweza kusababisha kutoka damu kwa wingi wakati wa ujauzito au wakati wakati wa kuzaa. Ukiwa na placenta previa unaweza kutoka damu mfululizo kipindi chote cha ujauzito.
Adenomyosis: Hii ni aina nyingine ya kujijenga kwa tishu. Hali hii hutokea pale endemetrium, au ngozi laini ya juu ya nyumba ya mimba, inapoungana na misuli ya uterus. Hii huweza kusababisha kupata hedhi ya muda mrefu.
Tezi ya Thyroid: Unaweza kupata hedhi kwa muda mrefu kama tezi yako ya thyroid inatenda kazi chini ya kiwango chake. Hali hii huitwa hypothyroidism.
Kutokwa damu: Unaweza kuwa na hali ambayo imeathiri uwezo wa mwili wako kuifanya damu yako igande, na kukusababishia hedhi ndefu. Mbili katika hali hizi ni hemophilia na von Willebrand’s disease.
Unene: Unene uliozidi unaweza kukusababisha kuingia period kwa muda mrefu. Hapa ni kwa sababu tishu za mafuta zinaweza kusababisha mwili kutengeneza estrogen nyingi zaidi. Estrogen hii ya ziada inaweza kukuletea mabadiliko ya hedhi yako.
. Kuwa na kiwango kidogo cha platelets. Platelets au thrombocytes ni vipande vidogo visivyo na rangi vilivyomo ndani ya damu ambavyo hufanya damu kuganda na kuzuia kutiririka kwa damu. Platelets hutengenezwa ndani ya bone marrow pamoja na chembechembe nyekundu na chembechembe nyeupe za damu.
Ugonjwa wa PID: Pelvic inflammatory disease (PID) hutokea pale bakteria wanaposhambulia viungo vyako vya uzazi. Pamoja na kubadilisha mzunguko wako wa hedhi, PID inaweza kusababisha kutoka uchafu usio wa kawaida pamoja na dalili nyingine.
Saratani: Kutoka damu kwa muda mrefu wakati wa hedhi inaweza kuwa ni ishara ya saratani katika nyumba ya uzazi au shingo ya kizazi. Kwa baadhi ya wanawake, hii inaweza kuwa ndiyo dalili ya kwanza ya saratani hizi.
Jee, Unaweza Kufupisha Siku Zako Za Hedhi?
Ni kitu cha kawaida kutokea kuwa utasafiri nje ya nyumbani kwako, ukataka kwenda beach, ukawa na shughuli fulani muhimu, na tarehe zikagongana na siku zako za hedhi. Kuliko kuahirisha plani zako, unaweza kuzipunguza siku za hedhi katika mzunguko wako.
Kuna mbinu unazoweza kuzijaribu ili hedhi yako iishe mapema zaidi. Baadhi ya mbinu hizi unaweza kuzifanya kila mwezi bila madhara, lakini nyingine zinahitaji ushauri wa daktari.
1. Tumia vidonge vya uzazi wa mpango (hormonal birth control pills)
Vidonge vya uzazi wa mpango (Oral birth control pills) na sindano (birth control injections) vinaweza kutumika kuidhibiti hedhi yako. Vidonge vinaweza pia kupunguza maumivu ya tumbo na kupunguza siku za hedhi kila mwezi. Ukianza kutumia vidonge hivi sasa, itakuchukua miezi kadhaa kabla hedhi yako haijapungua siku zake.
Yafaa kupata ushauri wa daktari kuhusu vidonge vitakavyokufaa.
2. Fanya tendo la ndoa
Kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa, kunaweza kupunguza maumivu ya tumbo na utokwaji wa damu. Hii ni kwa sababu kufika kileleni kunasababisha kukaza kwa misuli ya nyumba ya uzazi, tendo ambalo litasaidia kuiondoa damu kwenye nyumba ya uzazi.
Kukaza huku kwa misuli kunasaidia nyumba ya uzazi kumwaga damu haraka.
3. Fanya mazoezi mara kwa mara
Kuwa na ratiba ya kufanya mazoezi ya kuhema haraka (cardiovascular exercise routine) hakusaidii kuboresha afya tuu, lakini pia husaidia kupunguza uzito wa hedhi. Kunaweza pia kusaidia kupunguza idadi ya siku za hedhi unazopata. Mazoezi pia hupunguza maji mwilini, na kuzuia tumbo kujaa na maumivu ya hedhi.
Yafaa kujua mazoezi mazuri ya kuyafanya. Mazoezi ya kuzidi kipimo yanaweza kukufanya ukonde sana hadi chini ya kiwango kinachofaa, kitu ambacho kinaweza kuvuruga afya yako ya homoni na kukufanya usimame hedhi.
4. Linda uzito wako wa mwili
Mabadiliko katika uzito wako huathiri hedhi zako na kuzifanya kuwa zisizoeleweka. Kwa kawaida, wanawake wenye uzito mkubwa wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata hedhi nzito. Wanawake wengine wanaweza kupata hedhi nzito, zenye maumivu kwa wiki kadhaa. Hii hutokana na kuzalishwa kwa estrogen kwa wingi kutoka seli za mafuta, ambako kunaweza kuleta hedhi ndefu na nzito.
5. Pata virutubishi
Baadhi ya virutubishi, kama vitamini B, ni muhimu kwa afya yako ya jumla. Baadhi vinaweza kukulegezea hedhi zako na kukuondolea maumivu ya wakati wa hedhi.
Vitamini B6 ni moja ya virutubishi vyenye mchango kwenye hedhi yako. Vitamini hii hupatikana ndani ya baadhi ya chakula kama mayai, samaki, na kuku. Vitamini B6 imebainika kuongeza homoni ya progesterone wakati ikipunguza estrogen ndani ya mwili. Hii inaweza kuisaidia tezi ya pituitary kuweka vizuri homoni za hedhi.
Utafiti mwingine ulionyesha kuwa zinc inasaidia kupunguza maumivu ya hedhi.
Magnesium ni madini mengine yenye uwezo wa kuondoa hedhi ndefu, zenye maumivu. Mchanganyiko wa magnesium na B6 umeonyesha kutoa msaada wa kupunguza maumivu ya hedhi.
6. Jaribu mimea ifuatayo
Baadhi ya mimea huweza kupunguza hedhi ndefu na zenye maumivu. Mimea ambayo imeonyesha matumaini ni pamoja na:
. fennel (shamari-kiungo jamii ya karoti), mmea wenye tabia ya kutuliza maumivu na kuzuia uvimbe unaoweza kupunguza maumivu ya hedhi na urefu wa hedhi
. Tangawizi, inayoweza kupunguza hedhi nzito
. raspberry leaf, yenye tabia ya kulegeza misuli itakayopunguza kukaza kwa misuli ya nyumba ya uzazi
7. Kunywa maji mengi.
Linapokuja swala la kupunguza makali ya hedhi, kunywa maji mengi ndiyo msingi.
Kama unywaji wako wa maji ni chini ya glasi 8 kwa siku, jaribu kuongeza kiwango ukiwa ndani ya hedhi – hii itakusaidia kupata maumivu kidogo zaidi na kupunguza maumivu ya kichwa. Inaweza kukusaidia kuongeza kasi ya mzunguko wako wa hedhi. Unywaji wa maji huzuia damu isiwe nzito.
Katika ukurasa wetu mwingine tutauzungumzia mzunguko wa hedhi ya mwanamke. Usisite kutuuliza maswali uliyo nayo au kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo.
Pata ushauri zaidi kwa kututumia ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au kututumia barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu ndani ya saa za kazi kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.