Nyama Za Pua (Nasal Polyps)

Nyama za pua ni vitu visivyo na maumivu vilivyoota ndani ya pua au sehemu za uwazi ndani ya mifupa ya uso au kitaalamu sinuses. Nyama za pua si saratani. Nyama za pua huota juu ya mucosa, ngozi laini na nyembamba inayotanda juu ya njia za pua na sehemu za wazi katika mifupa (hasa ndani ya fuvu) zinaowasiliana na mianzi ya pua. Kwa kawaida huonekana pande zote mbili za pua yako. Nyama za pua huweza kuvimba na kufanya upate shida katika kupumua. Nyama za pua ndogo huwa na umbo la tone linakaribia kudondoka. Lakini zikikua zinaweza kufanana na zabibu zilizomenywa zenye rangi ya pinki, njano au kijivu. Nyama za pua huwapata asilimia 40 ya watu na mtu ye yote anaweza kupata, lakini huonekana mara mbili zaidi kwa wanaume. Umri unavyozidi kuwa mkubwa, uwezekano wa kupata nyama za pua hupungua.  Nyama za pua zinaweza kumpata mtu ye yote, lakini huonekana zaidi baina ya watoto na watu wa umri wa kati. Madawa huweza kufanya nyama za pua kunywea au kuondoka. Lakini wakati mwingine upasuaji hulazimika kufanyika. Hata baada ya tiba hizi, nyama za pua mara nyingi hurudi tena.

Dalili Za Nyama za Pua

Nyama za pua ndogo zinaweza zisitoe dalili yo yote. lakini zikikua unaweza kuona:

. Kuziba kwa pua
. Kuchirizika kwa kamasi
. Kuumwa kichwa
. Kupoteza ladha na harufu
. Damu puani
. Kukoroma

Nyama za pua zikikua na kuwa kubwa sana, zinaweza kuziba njia ya pua na sehemu za wazi katika mifupa, na kusababisha:

. Pumu ya mara kwa mara (kwa watu wenye pumu)
. Maambukizo ya mara kwa mara
. Sleep apnea (kuziba pumzi ukilala)
. Shida kupumua

Chanzo Cha Nyama za Pua

Wataalamu wanajua kuwa namna yo yote ya uvimbeuchungu huleta nyama za pua, lakini wanashindwa kujua ni kwa nini uvimbeuchungu husababisha nyama za pua kwa baadhi tu ya watu.

Uvimbeuchungu sugu kutokana na mzio, maambukizo au pumu – unaonekana kuwa ndiyo sababu kubwa ya kuota nyama za pua. Uvimbeuchungu sugu maana yake matatizo ya uvimbeuchungu yaliyodumu kwa miezi mitatu au zaidi.

Vichocheo vya kuota nyama za pua ni pamoja na:

. Pumu
. Allergic rhinitis
. Maambukizo sugu ya njia za pua
. Cystic fibrosis
. Baadhi ya dawa – NSAIDs (nonsteroidal anti-inflammatory drugs)

Urithi inaweza kuwa ni moja ya sababu ya kuota nyama za pua.

Shida Za Ziada

Maambukizo ya kujirudiarudia ya ya njia za pua yatokanayo na uwepo wa nyama za pua yanaweza kuleta shida kubwa baadaye kama:

. Maambukizo kwenye mifupa (osteomyelitis) na kupoteza mfupa
. Majipu yanayoweza kuenea kwenye mashimo ya macho na ubongo
. Meningitis (Kushambuliwa kwa tishu za ubongo na uti wa mgongo)

Tiba Ya Nyama za Pua

Tiba ya nyama za pua hutegemea hatua iliyofikiwa. Madawa na upasuaji ndizo njia mbili zinazotumika.

Pamoja na kuondolewa kwa upasuaji, nyama za pua zinaweza kuota tena baada ya muda.

Dawa

Dawa mara nyingi haziondoi nyama za pua bali kupunguza makali ya dalili zake. Tiba za kawaida ni:

. Steroid nasal sprays – dawa za kupulizia zinazofanya nyama za pua kusinyaa na kupunguza dalili
. Oral steroids – vidonge vya kunywa kama prednisone
. Biological medications, kama sindano za dupilumab

Daktari anaweza vile vile akakupatia antibiotics kama una maambukizo.

Upasuaji

Kama dawa hazifanyi kazi – au kama nyama za pua ni kubwa sana – upasuaji unaweza kuhitajika ili kuziondoa. Tabibu anaweza kutumia nasal endoscopy ili kufanya moja ya haya:

. Polypectomy. Daktari anatumia vyombo vidogo – kama mikasi ya upasuaji – kushika na kuziondoa nyama za pua kutoka kwenye pua yako.

. Balloon sinuplasty. Daktari anaingia vijiputo vidogo kupitia tundu za pua hadi ndani kwenye uwazi. Taratibu anajaza upepo kwenye viputo ili kuziba njia ya pua. Wakati mwingine, huondoa nyama za pua sambamaba na zoezi hili.

. Functional endoscopic sinus surgery (FESS).  Daktari anatumia vyombo vidogo kuondoa nyama za pua, eneo lenye ugonjwa, mfupa ulioharibiwa na vitu vingine vinavyoziba njia ya pua.

Katika ukurasa mwingine, tutajadili tatizo la kuziba pumzi usingizini. Usisiste kutoa maoni uliyo nayo kuhusu uandishi wetu wa mada hii.

Pata ushauri zaidi kwa kututumia ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini kwa kujaza fomu, au kututumia barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu ndani ya saa za kazi kwenye namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.