Sauti Kwenye Masikio, Ni Tatizo Gani?

 

 

Umeshawahi kutokewa na hali ambapo unasikia kelele ndani ya masikio? Kuna tatizo linalowatokea watu wengi ambalo husababisha mtu kusikia sauti ndani ya masikio. Ni tatizo ambalo kitaalamu huitwa tinnitus. Mtu husikia mivumo ndani ya sikio au sauti za kengele kwenye sikio wakati hakuna kitu cha nje kinachotoa kelele. Tatizo hili huweza kumkosesha mtu raha na wakati mwingine linaweza kuvuruga usikivu wake kwa vitu vinavyomzunguka. Unaweza kusikia mivumo au kelele ndani ya sikio moja au wakati mwingine ndani ya masiko yote mawili. Ni tatizo ambalo huwapata asilimia 15 hadi 20 ya watu na hasa wale wenye umri mkubwa.

Mada yetu ya leo itajadili matatizo ya kusikia mivumo au sauti za kengele ndani ya masikio, tukianzia na sababu za sauti hizo na kisha hatua gani za kuzichukua ukiwa tayari umepatwa na shida hiyo.

Dalili

Tinnitus huelezwa kuwa ni mivumo ndani ya sikio, hata kama hakuna sauti za nje. Tinnitus huweza kuleta aina nyingi ya sauti kwenye sikio, kama:

. kuvuma (kama nyuki)
. kunguruma
. sauti ya kugonga kama vile ya kidole
. sauti ya sss kama ya mlio wa nyoka.

Watu wengi wenye tinnitus wana tatizo liitwalo subjective tinnitus kwa maana ya kusikia sauti wewe peke yako. Sauti unayoisikia inaweza kuwa ya juu au ya chini, na unaweza kuisikia ndani ya sikio moja au yote mawili. Wakati mwingine sauti inaweza kuwa ya juu hivi kwamba ukashindwa kutuliza mawazo au kuzikia sauti za nje. Tinnitus inaweza kuwa ya muda mfupi au ya kudumu.

Aghalabu, tinnitus huja kama mdundo wenye mahadhi, mara nyingi ukifuata mapigo ya moyo. Hii huitwa pulsatile tinnitus. Ukiwa na pulsatile tinnitus, daktari anaweza kuzisikia sauti hizo ukiwa kwenye uchunguzi.

Sababu Za Mivumo Ya Sauti Ya Ndani Ya Masikio

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha au kuchochea tatizo la kelele ndani ya masikio. Mara nyingi sababu kamili huwa siyo rahisi kuibaini.

Sababu zinazoonekana mara nyingi kusababisha tinnitus

Kwa walio wengi, tinnitus husababishwa na yafuatayo:

. Kupoteza usikivu. Kuna seli ndogo, dhaifu za nywele kwenye eneo la ndani kabisa la sikio (cochlea) ambazo hucheza wakati sikio likipata mawimbi ya sauti. Kucheza huko husababisha ishara za umeme kwenye neva inayounganisha sikio na ubongo (auditory nerve). Ubongo hutafsiri ishara hizo kuwa sauti.

 

 

Endapo nywele hizi za sehemu ya ndani ya sikio zitapinda au kukatika -hali hii hutokea umri ukiwa mkubwa au unapokuwa kwenye mazingira ya sauti kubwa mara kwa mara – zinaweza kuvujisha misukumo ya umeme isiyo na mpangilio kwenda kwenye ubongo, na kusababisha tinnitus.

. Maambukizo au Kuzibwa kwa mkondo wa sikio. Masikio yako yanaweza kuzibwa kwa kujijenga kwa majimaji, nta za masikio, uchafu au vitu vingine toka nje. Kuziba kunaweza kubadilisha msukumo wa ndani ya sikio, na kusababisha tinnitus.

. Kuumia kwa kichwa au shingo. Kuumia kwa kichwa au shingo kunaweza kuathiri sehemu ya ndani ya sikio, neva za usikivu au utendaji wa ubongo unaohusiana na kusikia. Kuumia kwa namna hii mara nyingi husababisha sauti kwenye masikio.

. Matumizi ya madawa. Kuna madawa ambayo huweza kusababisha au kuongeza tatizo la kelele za masikioni. Kwa kawaida, dozi inavyokuwa kubwa zaidi ya dawa hizi, tatizo ndivyo linakuwa kubwa zaidi. Kwa kawaida, sauti hizi zisizotakiwa hutoweka pale matumizi ya dawa hizi yanapokoma.

Dawa zinazoeleweka kuleta tinnitus ni pamoja na nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) na baadhi ya antibiotics, dawa za kansa, diuretics, dawa za malaria na antidepressants.

Sababu Nyingine Za Tinnitus

Mara chache tinnitus huweza kutokea kwa sababu nyingine kama matatizo ya sikio, kuumwa kwa muda mrefu, na kuumia kulikoathiri neva ndani ya sikio au eneo la ubongo linalohusika na kusikia.

. Meniere’s disease.

. Eustachian tube dysfunction.

. Ear bone changes

. Muscle spasms in the inner ear.

. Matatizo katika Temporomandibular joint (TMJ)

. Acoustic neuroma au uvimbe wa aina nyingine kwenye kichwa au shingo

. Matatizo ya mishipa ya damu

.  Matatizo mengine sugu.

Vitu hatarishi kwa tinnitus

Mtu ye yote anaweza kupatwa na tinnitus, lakini baadhi ya vitu huongeza hatari:

. Sauti kubwa. Sauti kubwa kama za mashine kubwa, baruti, ni vitu ambavyo mara nyingi husababisha matatizo ya kusikia. Vyombo vya muziki vinavyohamishika, kama MP3 players, vinaweza pia kuleta matatizo ya kusikia kama vitachezwa kwa sauti kubwa kwa muda mrefu. Watu wafanyao kazi kwenye mazingira ya kelele – kama viwandani na kwenye ujenzi, wanamuziki, na askari – huwa wapo kwenye hatari kubwa.

. Umri. Umri unavyozidi kuwa mkubwa, idadi ya nyuzi za neva zinazofanya kazi hupungua, na labda kusababisha matatizo ya usikivu ambayo yataambatana na tinnitus.

Jinsia. Wanaume hupata tinitus zaidi kuliko wanawake.

.Tumbaku na vilevi. Watu wanaovuta sigara wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata tinnitus. Kunywa pombe pia kunaongeza yamkini ya kupata tinnitus.

. Matatizo ya kiafya. Unene, magonjwa ya moyo, high blood pressure na kuwa na historia ya magonjwa ya maungio ya mifupa na kuumia kichwa vinaongeza hatari ya kupata tinnitus.

Madhara yatokanayo na tinnitus

Tinnitus huwaathiri watu kwa njia tofauti. Kwa baadhi ya watu, tinnitus huharibu maisha yao. Kama una tinnitus unaweza kuyaona yafuatayo:

. Uchovu
. Msongo wa mawazo
. Matatizo ya usingizi
. Shida kutafakari
. Matatizo ya kumbukumbu
. Mfadhaiko
. Wasiwasi na kukosa amani
. Maumivu ya kichwa.

Tiba Ya Tinnitus

Tiba ya tinnitus inategemea kama ugonjwa ulianzia kwenye tatizo jingine la kiafya. Kama ndivyo, daktari ataweza kukuondolea dalili unazozipata kwa kutibu tatizo sababishi. Mifano ni kama:

. Kuondoa nta ya sikio. Kuondoa nta ya sikio kunaweza kupunguza tatizo la tinnitus.
. Kutibu mshipa wa damu. Matatizo ya mishipa ya damu yanaweza kuhitaji dawa, upasuaji au tiba ya aina nyingine.
. Vifaa vya kusaidia kusikia. Kama tinnitus ilisababishwa na sauti au umri, vifaa vya kukusaidia kusikia vinaweza kutumika.
. Kubadili dawa. Kama dawa unazotumia zimeonekana kusababisha tatizo, daktari anaweza kushauri uziache au kukubadilishia dawa nyingine.

Kupunguza sauti

Mara nyingi tinnitus haitibiki. Lakini kuna dawa za kusaidia kupunguza makali yake. Daktari anaweza kukupa kifaa cha kielektroniki cha kupunguza sauti. Vifaa hivi ni pamoja na:

White noise machines. Vifaa hivi vinatoa sauti kama za kwenye mazingira, kama mvua inayonyesha au mawimbi ya bahari, husaidia kutibu tinnitus. Feni, humidifiers na viyoyozi vikiwa chumbani pia hutoa sauti (white noise) ambayo huweza pia kupunguza makali ya tinnitus.

Masking devices. Vifaa hivi vivaliwavyo kwenye masikio hutoa sauti ya chini mfululizo (low-level white noise) ambayo hupunguza makali ya tinnitus.

Dawa

Dawa hazitibu tinnitus, lakini kuna wakati zinaweza kusaidia katika kupunguza ukali au madhara yanayotokana na tinnitus. Ili kupunguza dalili unazozipata, daktari anaweza kukupa dawa za kutibu chanzo sababishi cha tinnitus au dawa za kukuondolea wasiwasi na mfadhaiko vinavyoambatana na tinnitus.

Katika mada nyingine tutazungumzia kizunguzungu. Usisite kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo au kuuliza maswali uliyo nayo.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya saa za kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.