Tatizo La Hormonal Imbalance

Hormonal imbalance ni hali ambapo kuna uzidifu au upungufu wa homoni moja au zaidi katika mwili, hali ambayo inaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya. Ni neno pana ambalo linaweza kuelezea hali tofautitofauti kuhusiana na homoni. Dalili za kawaida ni kama mabadiliko ya uzito, kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa, na chunusi na inategemea ni homoni ipi isiyo na uwiano.

Homoni ni kemikali zinazoratibu matendo mbalimbali ndani ya mwili kwa kusambaza ujumbe kupitia damu hadi kwenye viungo, ngozi, misuli na tishu nyingine. Ishara hizi huviambia viungo vya mwili nini cha kufanya na lini kifanyike. Homoni ni za muhimu kwa maisha na afya yako

Wanasayansi wamezitambua homoni zaidi ya 50 zilizomo ndani ya mwili hadi sasa.

Homoni na tishu nyingi (hasa viungo) vinavyozalisha na kuachia homoni vinaunda endocrine system.

Homoni hudhibiti shughuli nyingi katika mwili ikiwa ni pamoja na:

. Shughuli za ujenzi na uvunjaji wa seli za mwili (metabolism)
. Homeostasis (constant internal balance)
. Ukuaji
. Shughuli za mapenzi
. Uzazi
. Mzunguko wa kuamka na kulala (sleep-wake cycle)
. Hisia.

Hormonal Imbalance Ni Nini?

Hormonal imbalance ni hali inayotokea pale unapokuwa na homoni moja au zaidi nyingi zaidi au pungufu ya kiwango kinachohitajika.

Homoni ni ishara zenye nguvu kubwa. Kwa homoni zilizo nyingi, kuzidi kidogo au kupungua kidogo tu kunaweza kuleta mabadiliko makubwa katika mwili wako na kupelekea hali fulani ambazo zitadai matibabu.

Hormonal imbalance nyingine ni za muda mfupi wakati nyingine zinaweza kuwa sugu (za muda mrefu). Isitoshe, hormonal imbalances nyingine zitahitaji tiba ili kurudia afya yako, wakati nyingine hazitaathiri afya yako bali tu kuzorotesha ubora wa maisha yako.

Hormonal Imbalance Inaweza Kusababisha Hali Zipi?

Hormonal imbalance inaweza kuleta mabadiliko ya kiafya ya aina nyingi sana katika mwili. Nyingi katika homoni, kuwa na uwingi wa kuzidi au kuwa na upungufu huleta dalili na matatizo ya kiafya. Wakati matatizo mengi yanayoletwa huhitaji tiba, mengine huweza kuondoka yenyewe.

Hali zinazoonekana mara nyingi na zinazosababishwa na hormonal imbalance ni:

. Hedhi zisizotabirika (irregula menstrual periods): Homoni kadhaa zinahusika katika mzunguko wa hedhi. Kwa sababu hiyo, kukosekana kwa uwiano katika moja au baadhi ya homoni kunaweza kusababisha hedhi zisizotabirika. Hali ambazo zinahusiana na homoni zinazosababisha hedhi zisizotabirika ni pamoja na polycystic ovary syndrome na amenorrhea.

. Kutopata mimba (infertility): Hormonal imbalance ni sababu inayoongoza ya ugumba kwa wanawake. Matatizo yanayohusiana na homoni kama ya PCOS na kushindwa kupevusha yai (anovulation) huweza kusababisha ugumba. Wanaume nao pia huweza kupata tatizo la hormonal imbalance ambalo litasababisha ugumba, kama kuwa na kiwango cha chini cha testosterone (low testosterone levels – hypogonadism).

. Chunusi: Chunusi husababishwa kimsingi na vijitundu vilivyoziba. Pamoja na kuwa kuna vipengele vingi vinavyosababisha chunusi, mabadiliko ya homoni na hasa wakati wa kubalehe, yana mchango mkubwa. Tezi za mafuta, pamoja na zile za kwenye ngozi ya usoni kwako, husisimuliwa wakati homoni zikianza kufanya kazi ukiwa kwenye  balehe.

. Hormonal acne (adult acne: Hormonal acne (adult acne) ni aina aya chunusi zinazotokea wakati mabadiliko ya homoni yanaongeza kiwango cha mafuta yanayotengenezwa na ngozi. Hii hutokea hasa wakati wa ujauzito, kukoma hedhi na watu walio kwenye tiba ya homoni (testosterone therapy).

Kisukari: Hali inayoonekana mara nyingni zaidi inayotokana na homoni ni kisukari. Kisukari maana yake kongosho halitengenezi au linatengeneza homoni ya insulin kwa kiwango kidogo au mwili wako hauitumii insulin ipasavyo. Kuna aina kadhaa za kisukari. Aina zilizozoeleka zaidi ni Type 2 diabetes, Type 1 diabetes na gestational diabetes. Kisukari huhitaji tiba.

Thyroid disease: Kuna aina mbili za maagonjwa ya tezi dundumio nayo ni hypothyroidism (viwango vya chini vya homoni ya thyroid) na hyperthyroidism (viwango vya juu vya homoni ya thyroid). Kila moja ina sababu kadhaa. Magonjwa ya thyroid yanahitaji tiba.

Unene: Kuna homoni nyingi zinazohusika katika kuuambia mwili wako kuwa unahitaji chakula na namna mwili wako unavyotumia nishati, hivi kwamba kukosekana kwa uwiano wa baadhi ya homoni kunaweza kusababisha kuongezeka kwa uzito wa mwili (unene) kama namna ya kuhifadhi ya mafuta. Kwa mfano, kuwa na ziada ya homoni ya cortisol na kiwango cha chini cha homoni ya thyroid kunaweza kuchangia unene wa mwili.

Dalili Na Chanzo Cha Hormonal Imbalance

Ni Dalili Zipi Za Hormonal Imbalance

Kwa sababu mwili wako hutengeneza homoni tofauti yapata 50 – zote zikiwa na mchango mkubwa katika utendaji kazi wa mwili wako – unaweza kuona dalili tofauti kutegemeana na ukosefu wa uwiano wa homoni husika.

Yafaa kujua kuwa nyingi ya dalili hizi zinaweza kiusababishwa na vitu vingine, na si lazima kuwa ni tatizo la hormonal imbalance.

Hormonal Imbalance Inayoathiri Shughuli Za Kimetaboliki

Hormpnal imbalance zinazoonekana kwa wingi ni pamoja na zile zinazoathiri shughuli za kimetaboliki ndani ya mwili wako. Shughuli za kimetaboliki ni mabadiliko ya kikemikali yanayotokea katika seli za mwili wako na kukibadilisha chakula kuwa nishati. Kuna homoni nyingi zinazohusika katika shughuli hizi.

Dalili za Hormonal Imbalances Zinazoathiri Shughuli Za Kimetaboliki

. Mapigo ya moyo kuwa chini au juu (tachycardia)
. Kupungua au Kuongezeka unene bila maelezo
. Uchovu
. Kufunga choo
. Kuharisha au kwenda haja kubwa mara kwa mara
. Ganzi au vitu kucheza kwenye mikono
. Viwango vikubwa mno vya cholesterol
. Mfadhaiko au wasiwasi
. Kushindwa kuhimili joto la juu au la chini
. Ngozi au nywele kavu vinavyokwaruza
. Ngozi nyembamba, ya joto na yenye unyevu
. Mafuta ya mwili kujipanga bila mpangilio
. Weusi wa ngozi kwenye makwapa au nyuma na upande wa kulia na wa kushoto wa shingo (acanthosis nigricans)
. Vitu vidogo kuota juu ya ngozi (skin tags)
. Kiu kali na kukojoa mara kwa mara.

Dalili Za Hormonal Imbalance Za Viungo Vya Uzazi Kwa Wanawake

Wanawake wanaweza kukosa uwiano wa homoni za uzazi ambazo ni estrogen na progesterone, ambazo huzalizwa na ovari. Wanaweza kuwa na estrogen na androgenskupita kiwango. Kukosekana kwa uwiano wa homoni kunaweza kuleta dalili zifuatazo kwa wanawake:

. Chunusi usoni, kifuani na/au sehemu ya juu ya mgongo
. Kukosa nywele
. Hedhi nzito
. Nywele kupita kiasi (Hirsutism)
. Vipindi vya joto kali (Hot flashes)
. Ugumba
. Hedhi zisizotabirika
. Kukosa hamu ya mapenzi
. Ukavu ukeni
. Uke kupungua ukubwa

Dalili Za Hormonal Imbalance Za Viungo Vya Uzazi Kwa Wanaume

Wanaume wanaweza kukosa uwiano wa testosterone, inayotengenezwa na korodani, na homoni nyingine, hali inayoweza kuleta dalili zifuatazo:

. Kupungua au kukosa nywele
. Jogoo kushindwa kuwika (ED)
. Matiti kuwa makubwa (Gynecomastia)
. Ugumba
. Kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi
. Kukosa musuli.

Nini Husababisha Hormonal Imbalance?

Katika maisha yako yote – na hata katika saa zote za siku – viwango vyako vya homoni hupanda na kushuka.

Vipindi fulani katika maisha huleta mabadiliko makubwa zaidi na homoni kupanda na kushuka, navyo ni:

. Kubalehe
. Ujauzito
. Kukoma hedhi

Hata hivyo, kuna sababu nyingine zinazofanya viwango vya homoni kutokuwa sawa wakati usiotegemewa. Baadhi ya sababu za kubadilika kwa viwango vya homoni au uwiano wa homoni kutokuwa sawa ni:

. Msongo wa mawazo
. Baadhi ya dawa
. Matumizi ya steroid

Hormonal imbalance zinazotokana na hali hizi zinaweza kuwa za muda mfupi au zinazotibika kwa kubadili dawa ua kudhibiti msongo wa mawazo.Hali sugu za mabadiliko ya homoni zinaweza kuletwa na sababu kadhaa. Kwa kawaida, mazingira yanayosababisha hormone imbalance inayohitaji tiba ni pamoaja na:

. Uvimbe, adenomas au vitu vingine vinavyoota kwenye mwili
. Kuharibika au kuumia kwa tezi za homoni
. Autoimmune conditions.

Uvimbe, Adenomas Na Vitu Vinavyoota Katika Mwili

Uoto wo wote juu ya tezi au kiungo kinachotoa homoni, kama uvimbe, adenoma au kinundu (nodule),unaweza kuathiri uwezo wa kutenda kazi.

Uvimbe

Uvimbe ambao mara chache sana huota kwenye viungo au seli zinazozalisha homoni huweza kuleta hormonal imbalance. Uvimbe huu unaweza kuwa ni:

. Adrenocortical carcinoma: Huu ni uvimbe wa saratani unajenga kwenye adrenal cortex. Kansa hii huweza kusababisha uzalishwaji wa homoni zaidi ya kiwango.

. Carcinoid tumors: Carcinoid tumorsnni aina ya neuroendocrine tumor (NET) inayoota kutokana na seli za neuroendocrine. Seli za neuroendocrine hupokea na kupeleka ujumbe kupitia homoni kuusaidia mwili kufanya kazi zake.

. Medullary thyroid cancer: Medullary thyroid cancer (MTC) ni saratani inayojijenga ndani ya thyroid (the medulla). Medulla huwa seli maalumu ziitwazo parafollicular C cells ambazo hutengeneza na kutoa homoni.

. Pheochromocytoma: Pheochromocytoma ni uvimbe utokeao mara chache katikati ya tezi moja au zote za adrenal (adrenal medulla). Uvimbe huu hujengwa na aina fulani ya seli ziitwazo chromaffin cells, ambazo hutengeneza na kutoa homoni. Kwa kawaida hazina madhara ingawa zaweza kuwa ni za saratani.

. Paraganglioma: Paraganglioma (ambayo pia hujulikana kama extra-adrenal pheochromocytoma) ni uvimbe wa neuroendocrine ambao hujenga karibu na ateri ya carotid, sambamba kwenye njia ya neva ndani ya kichwa na kwenye shingo na sehemu nyingine za mwili. Uvimbe huu hujengwa na seli za chromaffin ambazo hutengeneza na kutoa aina fulani za homoni.

Adenomas

Adenoma ni uvimbe usio wa saratani (benign tumor). Adenoma nyingi hazizalishi homoni. Lakini baadhi zinaweza kuzalisha homoni. Hizi huitwa functioning adenomas. Adenoma ambazo zinaweza kusababisha hormonal imbalance ni pamoja na:

. Pituitary adenomas: Pituitary adenomas zinaweza kusababisha hormonal imbalance kwenye homoni yo yote inayozalishwa na tezi ya pituitary. Kwa mfano, pituitary adenomas ni chanzo kikuu cha acromegaly -kuwa na uwingi wa ziada wa homoni ya ukuaji.

. Adrenal adenomas:  Chanzo kikuu cha Cushing’s syndrome (excess cortisol) ni adrenal adenoma kwenye adrenal cortex.

. Parathyroid adenomas: Parathyroid adenoma inaweza kusababisha primary hyperparathyroidism (excess parathyroid hormone).

Uvimbe Wa Aina Nyingine

Uoto mwingine zaidi ya uvimbe na adenomas kwenye tezi za homoni unaweza kusababisha hormonal imbalance. kwa mfano, thyroid nodules, uoto usio wa kawaida wa seli ndani ya tezi ya thyroid , unaweza kusababisha hyperthyroidism au hypothyroidism.

Uharibifu Au Kuumia kwa Tezi Za Kuzalisha Homoni

Namna yo yote ya uharibifu au kuumia kwa tezi ya kuzalisha homoni kunaweza kusababisha kukosekana kwa uwiano wa homoni – mara nyigni ni ukosefu (upungufu) wa homoni. Uharibifu unaweza kutokana na:

. Uharibifu wa bahati mbaya kutokana na upasuaji: Kwa mfano, karibu asilimia 75 ya hypothyroidism (viwango vidogo vya thyroid) ni kutokana na kuharibiwa kwa bahati mbaya kwa tezi za parathyroid wakati wa upasuaji wa shingo au thyroid.

. Kupoteza damu nyingi mno au kukosekana kwa mtiririko wa damu kwenda kwenye tezi ya homoni: Kukosekana kwa mtiririko wa damu kunaweza kusababisha tishu kufa (necrosis). Kwa mfano, Sheehan’s syndrome, chanzo cha hypopituitarism, inaweza kutokea kutokana na kupoteza damu nyingi mno baada ya kuzaa.

. Magonjwa ya bakteria au virusi: Kwa mfano, hypopituitarism iinaweza kuwa ni matokeo ya bacterial meningitis, ingawa ni mara chache.

. Tiba ya Mionzi: Tiba ya mionzi kwa saratani inaweza kuziharibu tezi za homoni. Kwa mfano, asilimia 50 ya watu wanaptibiwa saratani ya shingo na kichwa kwa kutumia mionzi hupata hypothyroidism.

. Kuuumia kwa kichwa au ubongo: Ajali za magari, kuanguka au kugongana kwenye michezo kunaweza kusababisha kuumia kwa kichwa au ubongo, na kuweza kusababisha uharibifu wa tezi ya pituitary au 0

..hypothalamus.

Matatizo Ya Kinga Za Mwili (Autoimmune conditions)

Autoimmune diseases ni Magonjwa ya kinga ya mwili ambapo mfumo wako wa kinga za mwili kwa bahati mbaya unashambulia sehemu ya mwili wako badala ya kuilinda. Haijajulikana ni kwa nini hii hutokea. Ikiwa mfumo wako wa kinga za mwili utashambulia tezi au kiungo kinachozalisha homoni, hormonal imbalance itatokea. Matatizo ya homoni yanayotokana na kinga za mwili ni kama:

. Hashimoto’s disease
. Graves’ disease
. Type 1 diabetes
. Addison’s disease
. Polyglandular syndromes.

Katika mada nyingine, tutalizungumzia tatizo la mzio (allergy). Usisite kuuliza maswali uliyo nayo kuhusu mada yetu ya leo. Tutafurahi sana kukujibu.

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu NDANI YA MUDA WA KAZI kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.