Tatizo La Mwanamke Kukosa Hamu Ya Kufanya Mapenzi

 

kukosa hamu ya tendo la ndoa

 

Tatizo la kukosa hamu ya kufanya mapenzi au kukosa nyege kwa lugha ya mitaani huwatokea zaidi wanawake kuliko wanaume, lakini ni wanaume wanaokerwa zaidi na tatizo hili kuliko wanawake. Wakati ambapo ni asilimia 15 hadi 16 ya wanaume wenye tatizo hili, idadi ya wanawake ni mara mbili ya hii ya wanaume. Lakini wakati ni asilimia 23 ya wanaume wanaonyesha kuridhika kuishi na tatizo hili, asilimia 46 ya wanawake wapo radhi kabisa kuendelea kuishi na tatizo hili.

Si lazima kuendelea kuishi na tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa sababu kuna mambo mengi unayoweza kuyafanya ili kuondokana na hili tatizo.

Hali ya kupenda kufanya mapenzi au tendo la ndoa kwa mwanamke inabadilikabadilika sana ikipanda na kushuka kulingana na matukio mbalibali yanayomtokea katika maisha yake. Baadhi ya matukio yanayoathiri hamu ya mwanamke ya kufanya mapenzi ni pamoja na kuanza na kwisha kwa mahusiano ya kimapenzi na mwanamme, kupata ujauzito, na magonjwa. Kama wewe mwanamke umepatwa na hali hii unaweza kukabiliana nayo kwa kubalisha jinsi unavyoishi, kufanya mambo kadhaa yatakayobadilisha hali hii au kutumia baadhi ya dawa zinazosaidia kuondoa tatizo hili.

 

Jee, Utajuaje kama Una Tatizo?

 

Kuna vitu vingi ukiviona vinakutokea, ujue una tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya mapenzi. Tulivijadili viashiria hivi kwa kina tulipozungumzia tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa wanaume. Unaweza kusoma tulivyojadili kwa kusoma ukurasa huu “Mwanamme Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa.”

 

 

 

kukosa hamu ya kujamiiana

 

 

Sababu Za Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa

 

Sababu zinazoweza kupelekea mwanamke kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa ni nyingi lakini kwa ujumla karibu zote tunaweza kuzigawanya katika makundi manne:

 

1. Mahusiano Baina Ya Mwanamke Na Mwanamme

Kwa wanawake walio wengi ukaribu wa kihisia ndicho kitu cha kwanza katika kujenga mapenzi kati yake na mwanamme. Hivyo, mahusiano mabovu yaweza kuwa ndicho chanzo cha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanamke. Mwanamke atakosa hamu ya kufanya mapenzi endapo hakutokuwa na mawasiliano baina yake na mumewe, kutakuwa na migogoro kati yake na mumewe isiyokwisha, kutakuwa na ukosefu wa mawasiliano kuhusu mahitaji yake ya kufanya mapenzi na jinsi ambavyo yeye angependa kufanyiwa kimapenzi na kama atahisi kuna ukosefu wa uaminifu katika ndoa au mahusiano yao.

 

2. Matatizo Katika Maisha Yako

Matatizo mbalimbali katika maisha ya mwanamke humsababishia kukosa hamu ya kufanya mapenzi. Baadhi ya matatizo ambayo huweza kusababisha mwanamke kukosa hamu ya kufanya mapenzi ni pamoja na magonjwa, mabadiliko katika mwili wake na hata matumizi ya baadhi ya madawa:

 

Matatizo Katika Kufanya Tendo La ndoa.

Kama mwanamke anapata maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa au kama mwanamke anakosa kufika kileleni, hali hii inaweza kusababisha akakosa kabisa hamu ya kufanya mapenzi.

Matatizo ya afya

Magonjwa mengi husababisha mwanamke akose hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baadhi ya magonjwa ni maumivu ya viungo vya mifupa (arthritis)kansa, ugonjwa wa kisukari, high blood pressure, matatizo katika mishipa ya damu ya arteri na matatizo ya akili.

Matumizi ya madawa

Baadhi ya madawa yakitumiwa, huondoa kabisa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Mfano wa dawa hizo ni madawa ya kukabiliana na msongo wa mawazo.

Mtindo wa maisha

Matumizi ya pombe kuzidi kiwango, uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya huathiri hamu ya kufanya mapenzi.

Upasuaji

Upasuaji uliofanyika katika maeneo ya maziwa au katika maeneo ya viungo vya uzazi humbadilishia mwanamke mwonekano wake, huathiri ufanyaji kazi wa viungo hivyo na mwisho kuathiri hamu yake ya kufanya mapenzi.

Uchovu: 

Unaotokana na kulea watoto wadogo au vikongwe huweza kuathiri hamu ya mwanamke ya kufanya mapenzi.

 

3. Mabadiliko Katika Mfumo Wa Homoni.

Kukoma hedhi:  Mabadilko ya viwango vya homoni katika mwili wa mwanamke yanaweza kusababisha kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Kupungua kwa Estrogen katika mwili wa mwanamke katika kipindi cha kuelekea kukoma hedhi kunaweza kusababisha ukosefu wa hamu ya kufanya mapenzi. Upungufu wa homoni hiyo husababisha uyabisi wa viungo vya sehemu nyeti na kusababisha maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Mwanamke pia huweza kuwa na upungufu wa homoni ya testosterone, homoni ambayo husaidia kuongeza hamu ya kufanya mapenzi kwa wanaume na wanawake, hivyo mwanamke huyo akapungukiwa na hamu ya kufanya mapenzi.

Pamoja na kuwa wanawake wengi huendelea kupata hamu ya kufanya mapenzi baada ya kukoma hedhi, baadhi kupungukiwa na hamu hiyo baada ya mabadiliko haya ya viwango vya homoni katika miili yao.

Ujauzito na kunyonyesha. Mabadiliko katika mfumo wa homoni wakati wa ujauzito, baada ya kujifungua na wakati wa kunyonyesha huweza kusababisha mwanamke kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

 

4. Matatizo Ya Kisaikolojia

Matatizo ya kisaikolojia yana mchango katika kumfanya mwanamke akose hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baadhi ya mtatatizo hayo ni:

  •  Wasiwasi na kuwa na msongo wa mawazo
  •  Kuwa na mawazo mengi kuhusu matatizo ya kifedha au kikazi
  •  Kuhisi kutothaminiwa katika jamii
  •  Kuwa na historia ya kunyanyaswa kimwili au kijinsia kama kupigwa  au kubakwa
  •  Kuwa na historia mbaya ya kimapenzi

 

 

 

kukosa hamu ya mapenzi

 

 

Njia Za Kuondoa Tatizo La Kukosa Hamu Ya kufanya Tendo La Ndoa

 

Hakuna dawa ya moja kwa moja toka hospitalini kwa sasa hivi kwa ajili ya kuondoa tatizo hili, hata hivyo wanawake wengi wanaweza kurudi kwenye hali zao za kawaida kwa kushirikiana na waume zao waelewa. Jaribu kufanya mambo tuliyoyadokeza katika mada yetu ya “Mwanamme Kukosa hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa” ukisaidiana na mumeo. Unahitaji kuchunguza taratibu na kwa kina chanzo cha tatizo lako, na taratibu lifanyie kazi kwa msaada wa mume wako.

Katika nchi zilizoendelea, kila siku wamekuwa wakija na dawa na vifaa vipya vya kuondoa tatizo hili na vingi bado ni vya bei kubwa na/au vinapatikana kwa shida. Vipo ambavyo vimeonyesha mafanikio makubwa, mifano ya vitu hivyo ni Suction Vibrators, Desire Creams na Erection Drugs.

Unaweza kupata mafanikio makubwa  (wasomaji wangu wengi wamefanikiwa na kunishukuru) kwa kutumia chakula kinachosaidia kuongeza hamu au kwa kutengeneza na kutumia viagra asilia. Hivi nimevielezea hapa chini. Kama hivi bado havijakusaidia, nashauri utumie virutubishi vya mwili ambavyo husamabazwa na makampuni mbalimbali. Vipo vinavyofanya kazi kwa haraka na kutibu kabisa tatizo hili. Endapo umepata tatizo kutambua virutubishi vizuri vya kutumia, wasiliana nasi kwa kutumia njia yo yote iliyo rahisi kwako kati  ya  hizi nilizoziorodhesha chini ya ukurasa huu.

Chakula Cha Kuongeza Hamu Ya Mapenzi

 

Utafiti umeonyesha pasi shaka kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya chakula tunachokula na afya ya viungo vya uzazi. Baadhi ya chakula na virutubishi vimehusishwa na hamu ya kufanya mapenzi (nyege). Virutubishi ndani ya chakula ambavyo vinasaidia hali hiyo ni antioxidants, vitamin C, vitamin E, potassium na zinc. Kirutubishi cha zinc ambacho hupatikana ndani ya  vitunguu swaumu, mbegu za maboga, ufuta na mbegu za matikitimaji, kinaongeza mbegu kwa mwanamme (sperm count) hivyo humsaidia kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa. Chakula cho chote chenye virutubishi hivi kikiliwa, humfanya mlaji asikie hamu ya kufanya mapenzi au kwa maneno ya mtaani, chakula hiki kinasaidia kuongeza nyege. Baadhi ya chakula cha kuongeza nyege ni:

Tikitimaji-Hili linachukuliwa kuwa ndilo tunda bora katika kuboresha afya ya mapenzi. Tunda hili lina asilimia 92 ya maji na asilimia 8 zinazobakia zina phytonutrient citrulline ambayo hugeuzwa kuwa arginine. Arginine ni amino acid ambayo hufanya mishipa ya damu kuwa kwenye hali ya ubora wake na kusadia damu kupita vizuri zaidi. Tikitimaji kwa hiyo husaidia damu ifike kwa kiwango kizuri zaidi kwenye sehemu ambazo hutakiwa kutanuka wakati mtu akipata hisia za kufanya tendo la ndoa ambazo ni viungo vya ndani ya kisimi cha mwanamke na ndani ya uume wa mwanamme.

 

chakula cha kuongeza nyege

 

Strawberries– matunda haya yana antioxidants kwa kusaidia afya ya moyo na mishipa ya damu (arteri) na vitamin C ambayo huongeza kiwango cha mbegu kwa mwanamme.

 

matunda ya kuleta nyege

 

Pombe-glasi moja ya mvinyo hukufanya uwe na akili tulivu. Pombe kwa kiwango kikubwa huleta kinyume cha matarajio na kuondoa kabisa hamu ya mapenzi.

Avocadro-tunda hili lina vitamini E ambayo ni antioxidant. Ndani ya tunda hili kuna potassium na vitamini B6 ambavyo huboresha afya ya moyo na kusaidia mzunguko wa damu.

 

matunda ya kusidia hamu ya mapenzi

 

Viazi vitamu-hivi vina potassium ambayo husaidia kuondoa tatizo la high-blood pressure.

 

viazi huleta nyege

 

Chakula kingine katika kundi hili ni broccoli (picha hapa chini), karafuu, mayai na tangawizi.

 

mboga kwa kusaidia kuleta nyege

 

Kuna mchanganyiko wa matunda ukisagwa pamoja na kunywewa umeonyesha kuongeza hamu ya kufanya mapenzi au kuongeza nyege. Nilionyesha namna mbili za kutengeneneza mchanganyiko huo na nikauita “Viagra asilia.” Nitaongeza mchanganyiko wa tatu wenye matunda mengi zaidi ili uweze kuchagua ule utakaoona ni rahisi zaidi kuutengeneza.

Jinsi Ya Kutengeneza Viagra Ya Asili

Kusanya matunda kama yanavyoonyeshwa kwenye video hii hapa chini, saga kwa pamoja katika blender na kisha kunywa glasi moja ya mchanganyiko huo. Hakuna kipimo kamili cha kutumia, lakini ukipata glasi tatu kwa siku utapata mabadiliko ya kutosha kabisa. Wapo watu wengi waliofuata ushauri huu, wakanipigia simu kuwa hali zao zimekuwa nzuri sana baada ya kutumia kinywaji hiki. Jaribu kisha nipe matokeo.

Kama umeshindwa kupata matunda yote kwa kutengeneza viagra hii asilia, nenda ukurasa wa “Mwanamme Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa” ambamo nimeelezea viagra asilia ya matunda mawili tu, tikiti maji na limau.

 

 

 

viagra ya asili ya matunda

 

 

Kama una swali lolote au maoni yako kuhusiana na mada hiyo hapo juu, usisite kutuandikia. Pia usisite kuomba ushauri zaidi pale ulipojaribu njia hizi ukakwama mahali.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wetu wa Facebook wa LINDA AFYA YAKO kupata mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya mwanadamu na tiba mbalimbali. Usikose kuweka LIKE endapo utafurahishwa na mada hizo.

 

JEE, UNA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA MAPENZI?

 

Kama una tatizo hili na umeshindwa kulipatia ufumbuzi, wasiliana nasi.

Kwa mawasiliano nasi tuma tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: +255 655 858027 au +255 756 181651.

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.