Tiba Ya Kisukari

upofu kutokna na kisukari

 

Tumekwisha kuona ni chakula gani apate mgonjwa wa kisukari na kwa mpango upi mgonjwa wa kisukari apate chakula hicho. Pia tulijadili jinsi ya kufanya mazoezi ya mwili na kuona faida za mazoezi hayo kwa mgonjwa huyu. Katika mada yetu ya leo, tutazungumzuia namna ambavyo mgonjwa wa kisukari anavyoweza kupewa au kutumia insulin.

Kimsingi mgonjwa anaweza kupewa insulin ya vidonge, lakini pindi atakapokunywa vidonge hivyo na vikafika tumboni, vitameng’enywa mara moja bila hata kuingia katika mkondo wa damu. Hivyo basi inapasa kumpa mgonjwa insulin ya sindano ambayo itachonmwa kwenye mafuta yaliyo chini tu ya ngozi, ili taratibu dawa hiyo iingie kwenye mkondo wa damu.

Kuna aina zaidi ya 20 za insulin ambazo kila kila moja inafanya kazi tofauti na nyingine, imetengenezwa kwa njia tofauti na nyingine na ina bei tofauti na nyingine. Insulin nyingi hutengenezwa kwenye maabara na nyingine hutokana na wanyama, hasa nguruwe.

 

Tiba Ya Kisukari Kwa Insulin Ya Sindano

 

 

Tiba ya kisukari kwa sindano ya insulin

 

Rapid-acting insulin

Rapid-acting insulin ni aina ya insulin ambayo hufanya kazi kwa haraka sana, dakika 5 tu baada ya mgonjwa kuchomwa sindano hiyo na hufikia kilele cha ufanyaji kazi wake baada ya saa moja. Insulin za aina hii huendelea kuwa na nguvu ya kufanya kazi katika mwili kwa muda wa saa 2 hadi 4. Mifano ya Rapid-acting insulin ni lispro, insulin aspart na insulin glulisine.

Short-acting insulin

Insulin ya aina hii huingia kwenye mkondo wa damu ndani ya dakika 30 tu na hufikia kilelele cha utendaji kazi wake ndani ya saa 2 hadi 3. Insulin hii huendelea kufanya kazi ndani ya damu kwa muda wa saa 3 hadi 6.

Intermediate-acting insulin

Intermediate-acting insulin huchukka muda wa saa 2 hadi 4 kuingia kwenye mfumo wa damu baada ya sindano kuchomwa na hufikia kilele cha ufanyaji wake kazi baada ya saa 4 hadi 12. Inaendelea kufanya kazi mwilini kwa muda wa saa 12 hadi 18.

Long-acting insulin

Insulin ya aina hii huingia ndani ya damu baada ya saa 6 hadi 10 baada ya kuchomwa sindano na zinafanya kazi ndani ya damu kwa muda wa saa 20 hadi 24.

Pre-mixed insulin

Wagonjwa wengine wa kisukari hutakiwa wachanganye insulin za aina mbili. Ili kuwarahisishia, kuna insulin ambazo zinakuja zikiwa zimeshachanganywa tayari. Insulin za aina hii huwasaidia zaidi watu wenye matatizo ya kuona.

 

Tiba Ya Kisukari Kwa Kutumia Insulin Pump

 

Insulin pump ni kifaa maalumu kilichotengenezwa kukuongezea insulin mwilini kwa haraka muda wote unapokuwa unakitumia. Ni kifaa ambacho unaweza kukifunga kwenye mkanda, kukiweka ndani ya mfulo wa nguo yako au kukifunga kwenye mkono au mguu na kukifunika na nguo zako. Usiku unapolala, unaweza kukiweka chini ya mto au po pote unapoona panafaa karibu na kitanda chako.

 

tiba ya kisukari kwa insulin pump

 

Kifaa hiki hutumika zaidi na watu wenye Type 1 Diabetes ingawa taratibu watu wenye Type 2 Diabetes nao wameanza kukitumia. Ni kifaa chenye faida nyingi sana katika kudhibiti kiwango cha sukari katika mwili wa mgonjwa.

Mada hii ya kisukari ni mada ndefu iliyotuchukua toka kujua chanzo cha kisukari na aina zake, ikatupeleka kujua dalili na madhara ya kisukari na vile vile ilizungumzia njia nyingine za kupambana na kisukari kabla ya leo kuzungumzia tiba ya kisukari kwa kutumia insulin.

Tunaomba maoni yako kuhusu mada yetu na usisite kuuliza maswali uliyo nayo. Ni furaha kwetu kukujibu.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0 655 858027 au  0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.