Ugonjwa Wa Bacterial Vaginosis ni Nini?

 

bacterial vaginosis cover

 

Bakteria rafiki na wabaya wote huishi ndani ya uke. Inapotokea uwiano dhalili wa ukeni unabadilika, unaweza kupata ugonjwa huu wa bacterial vaginosis (BV kwa kifupi) au wakati mwingine huitwa vaginal bacteriosis. Ni ugonjwa unaowasumbua wanawake walio katika umri wa kuzaa, miaka 15 hadi 44 ingawa mwanamke wa umri wo wote huweza kuupata. Chanzo halisi bado hakijajulikana, lakini kushiriki ngono mara nyingi bila kinga na kujiosha ukeni kwa maji kumedhihirika kuwa kunaongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huu. BV kwa kawaida haileti madhara mengine ya kiafya. Lakini huweza kuchangia kupatwa na matatizo mengine hasa pale unapokuwa mjamzito au unatarajia kupata mimba.

 

Chanzo Cha Bacterial Vaginosis

 

Bakteria aitwaye lactobacillus hufanya kazi ya kuuweka uke kwenye hali ya utindikali ili bakteria wabaya wasizaliane. Endapo idadi ya lactobacillus itapungua, bakteria wabaya huongezeka na utapata BV.

Mwanamke ye yote anaweza kupata BV, lakini yafutayo yanaongeza yamkini ya maambukizi haya:

. Kuvuta sigara
. Kushiriki ngono na mpenzi mpya au wapenzi wengi
. Kujiosha ukeni kwa maji au vimininika vingine (douching)
. Matumizi ya antibiotics ya siku za karibuni

Ungefikiria kuwa kujiosha mara kwa mara ukeni kungekusaidia kuzuia BV, lakini kujiosha huko kunaharibu uwiano wa asili wa bakteria wa ukeni. Sabuni za manukato na perfume za ukeni nazo zinachangia katika kuharibu uwiano huo wa bakteria.

Kuwa na mpenzi mpya au kuwa na wapenzi wengi kunaongeza uwezekano wa kupata BV. Sababu hazijawa bayana. Unaweza kupata BV kwa kushiriki ngono ya mdomo au ya kinyume na maumbile.

Si kweli kuwa unaweza kupata BV au magonjwa mengine ya ukeni kutoka kwenye mabwawa ya kuogelea au vyoo.

 

Dalili Za Bacterial Vaginosis

 

 

Zaidi ya nusu ya wanawake wenye BV hawaonyeshi dalili zo zote. Pale zinapoonekana huwa pamoja na:

. Uchafu mwembamba mweupe, wa kijivu au kijani hasa baada ya tendo la ndoa
. Kuwaka moto wakati wa haja ndogo
. Harufu ya samaki inayozidi baada ya kujamiiana
. Mara chache kuwa na miwasho sehemu ya nje ya uke

 

bacterial vaginosis harufu

 

 

Kuna utofauti na candidiasis (yeast infection) ambayo huleta mwasho, hutoa uchafu mzito mweupe usio na harufu.

 

Tiba Ya Bacterial Vaginosis

 

Kama huna dalili zo zote na huna ujauzito, hutahitaji tiba. BV inaweza ikaondoka yenyewe.

Pale inapoonyesha dalili, daktari anaweza kukuandikia antibiotics. Vinaweza kuwa ni vidonge au cream utakayopaka ukeni. Utahitaji kuendelea na tiba kwa siku 5-7. Unapaswa kumaliza dozi hata kama dalili zitakuwa zimeondoka. Ukikatisha, maambukizi yanaweza yakarudi upya.

Kwa vile BV inaenezwa kwa ngono, inakubidi kusimama hadi utakapokuwa umepona. Hata kama BV imepona, ni kawaida kurudi tena. Na ikitokea hivyo, unashauriwa kutumia tena antibiotics kwa kipindi kirefu zaidi.

Katika mada nyingine tatajadili tatizo la uchi kulegea au hali ya maumbile ya mwanamke kuwa mapana kuliko kawaida na tatizo la candidiasis.

Tunaomba mchango wako wa mawazo kuhusu mada yetu ya leo na kama una maswali yo yote usisite kutuuliza. Ni faraja kwetu kuona tumekujibu vizuri.

 

 Kwa mawasiliano tumia anuani promota927@gmail.com, au jaza fomu iliyopo chini kwenye ukurasa huu. Unawaewza kuzungumza nasi moja kwa moja kwa simu kwa namba 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.