Ugonjwa Wa Figo Unaosababishwa Na Kisukari (Diabetic Nephropathy)

 

 

Kisukari (diabetes type 1 au diabetes type 2) kinaweza kusababisha ugonjwa wa figo ambao kitaalamu huitwa diabetic nephropathy. Diabetic nephropathy huathiri uwezo wa figo wa kutoa mabaki na maji ya ziada kutoka katika mwili. Njia kuu ya kuuzuia ugonjwa huu wa figo unaotokana na kisukari ni kufuata mtindo mzuri wa maisha na kudhibiti sukari ya mwili na pressure.

Miaka ikipita, taratibu hali hii huharibu kabisa mfumo wa uchuchaji wa figo. Ugonjwa huu huweza kufikia hatua ya kufeli kwa figo (end -stage kidney disease), hali ambayo ni hatarishi kwa maisha. Hatua hii ikifikiwa, tiba pekee ni dialysis au kupandikizwa figo nyingine.

Dalili Za Figo Kuharibika Kwa Kisukari

Katika hatua za mwanzo, hutaona dalili zo zote. Baadaye utaanza kuona dalili zifuatazo:

. Shida zaidi katika kudhibiti pressure ya mwili
. Protini katika mkojo
. Kuvimba miguu, fundo za miguu, mikono au macho
. Kapata haja ya kukojoa mara kwa mara
. Uhitaji wa insulin au dawa za kisukari kupungua
. Kuchanganyikiwa au shida kutafakari
. Shida katika upumuaji
. Kukosa hamu ya kula
. kichefuchefu au kutapika
. Miwasho isiyoisha
. Uchovu

Sababu Ya Ugonjwa Wa Figo Utokanao Na Kisukari

Diabetic nephropathy hutokea wakati kisukari kinaharibu vishipa vya damu na seli nyingine ndani ya figo.

Namna Figo Zinavyofanya Kazi

 

 

Figo zako zanajengwa na mamilioni ya vikundi vya mishipa midogo ya damu viitwavyo glomeruli vinavyofanya kazi ya kuchuja mabaki na maji ya ziada na kutoa nje ya mwili kupitia mkojo. Pressure ya juu na kisukari vinaweza kuviharibu vitengo hivi vya uchuchaji na kusababisha makovu. Utendaji kazi wa figo zako hupungua na hatimaye figo zinaweza kufeli.

Madhara Yatokanayo Na Diabetic Nephropathy

Madhara yanaweza kuanza kuonekana baada ya miezi au miaka kadhaa. Madhara yanaweza kuwa ni pamoja na:

. Kutunzwa kwa majimaji, kunakoweza kusababisha kuvimba kwa mikono na miguu, high blood pressure, au maji ndani ya mapafu (pulmonary edema)
. Kupanda kwa viwango vya potassium ndani ya damu (hyperkalemia)
. Magonjwa ya moyo na mishipa ya moyo ambayo yanaweza kusababisha kiharusi
. Uharibishu wa mishipa ya damu ya tishu zinazoweza kuhisi mwanga zilizopo sehemu ya nyuma ya macho (diabetic retinopathy)
. Kupungua kwa chembechembe nyekundu za damu zinazosafirisha oksijeni (anemia)
. Madonda miguuni, jogoo kushindwa kuwika (erectile dysfunction), kuharisha na matatizo mengine yanayotokana na kuharibika kwa neva na mishipa ya damu
. Matatizo ya mifupa na madini ya mwili kutokana na figo kushindwa kutunza kiwango kizuri cha calcium ndani ya mwili na phosphorus ndani ya damu
. Matatizo wakati wa ujauzito yanayoweza kuhatarisha maisha ya mama na kichanga tumboni
. Kuharibika moja kwa moja kwa figo (end-stage kidney disease), mwishowe kuhitaji dialysis au kupandikiziwa figo

Tiba Ya Figo Zilizofeli Kwa Kisukari

Hatua ya kwanza ya kutibu figo zilizofeli kwa sababu ya kisukari ni kuhakikisha sukari ndani ya mwili na pressure vimedhibitiwa. Hii ni pamoja na ulaji, mtindo wa maisha, mazoezi na dawa. Ukidhibiti kisukari na pressure, unaweza ukazuia au ukasogeza mbele tatizo la figo zako na madhara yatokanayo.

Dawa

Katika hatua za mwanzo za uharibifu wa figo kutokana na kisukari, tiba itakuwa ni dawa kwa ajili ya:

. Dawa za pressure. Dawa ziitwazo angiotensin-converting enzyme (ACE) inhibitors na angiotensin 2 receptor blockers (ARBs) hutumika kutibu tatizo la high blood pressure.

. Kudhibiti sukari. Dawa zinaweza kusaidia kuweka vizuri viwango vya sukari. Metformin (Fortamet, Glumetza, n.k.) huboresha usikivu wa insulin na kupunguza uzalishwaji wa sukari katika ini. Glucagon-like peptide 1 (GLP-1) receptor agonists husaidia kupunguza sukari kwa kupunguza kasi ya mmeng’enyo na kusisimua utolewaji wa insulin kutokana na kupanda kwa sukari. SGLT2 inhibitors
hupunguza kiasi cha sukari inayorudi ndani ya damu, na kufanya sukari nyingi itolewe na mkojo.

. High cholesterol. Dawa za kupunguza cholesterol ziitwazo statins hutumika kupunguza cholesterol na protini ndani ya mkojo.

. Kidney scarring. Finerenone (Kerendia) hupunguza makovu.

Tiba Kwa Hatua Za Juu Za Diabetic Nephropathy

Kama ugonjwa utafikia kusababisha figo kufeli (end-stage kidney disease), daktari ataamua hatua nyingine kuchukuliwa, kama:

. Kidney dialysis. Tiba hii ni ya kutoa mabaki na maji ya ziada nje ya mwili wako. Aina kuu mbili za tiba hii ni hemodialysis na peritoneal dialysis. Katika aina ya kwanza, ambayo ndiyo inayotumia ziadi, utafika kwenye kituo cha huduma hii na kuunganishwa kwenye mashine wastani wa mara tatu kwa wiki au unaweza kufanyiwa nyumbani kwako na mtaalamu maalumu. Kila zoezi litachukua saa 3 hadi 5. Aina ya pili inaweza kufanywa nyumbani pia.

. Transplant. Mazingira mengine yatataka kupandikizwa figo nyingine (kidney transplant) au kidney-pancreas transplant.

Katika mada nyignie tutazungumza kuhusu  kufeli kwa figo. Usisite kutoaa maoni yako yako au kuuliza maswali kuhusiana na mada hii.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya muda wa kazi  kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.