Hepatitis D Ni Nini?
Hepatitis D, ambayo pia hujulikana kama delta virus, ni maambukizi yanayosababisha ini kuvimba. Kuvimba huku kunaweza kusababisha ini kushindwa kufanya kazi yake na kusababisha matatizo ya muda mrefu, kama makovu na saratani. Hali hii husababishwa na kirusi, hepatitis D virus (HDV). Kirusi huyu huonekana sana kwenye maeneo ya:
. Marekani Ya Kusini
. Afrika Magharibi
. Urusi
. Visiwa Vya Pacifiki
. Asia Ya Kati
. Eneo La Mediterranean
Hepatits D ni moja ya aina nyingi za hepatitis au homa ya ini. Aina nyingine ni:
. Hepatitis A, ambayo inaenezwa kwa kugusa kinyesi moja kwa moja au kwa kula chakula au maji yaliyochafuliwa na kinyesi
. Hepatitis B, inayoenezwa na majimaji yaliyomo mwilini kama damu, mkojo, au shahawa.
. Hepatitis C, inayoenezwa na damu yenye wadudu au sindano
. Hepatitis E, ambalo ni tatizo la muda mfupi na ambalo huondoka lenyewe, linalotokana na maji au chakula kilichochafuliwa na kinyesi.
Hepatitis D inatofautiana na aina nyingine za hepatitis kwa kuwa mgonjwa hawezi kuupata ugonjwa huu kwa wenyewe. Ni mtu ambaye aliwahi kupata hepatitis B tu, ndiye anayeweza kuupata ugonjwa huu.
Homa ya ini ya Hepatitis D inaweza kuwa kali au ya muda mrefu. Homa kali ya hepatitis D huja ghafla na huonyesha dalili kali zaidi.
Inaweza ikaondoka yenyewe. Kama maambukizi yatadumu kwa miezi sita au zaidi, tunasema hii ni homa ya ini ya kudumu (Chronic Hepatitis). Aina hii ya homa ya ini – homa ya kudumu – hujijenga taratibu kadiri muda unavyokwenda. Wadudu wa hepatitis wanaweza kuwemo ndani ya mwili kwa miezi kadhaa kabla ya kutoa dalili. Kadiri homa ya hepatitis itakavyokua, ndivyo uwezekano wa kupata madhara ya kudumu utakavyoongezeka. Watu wengi wa hali hii huishia kupata makovu ndani ya maini yao (cirrrhosis).
Hakuna dawa wala chanjo kwa hepatitis D, lakini kinga inaweza kutolewa kwa wale ambao hawajawahi kupata hepatitis B. Tiba inaweza kuzuia kuharibika kwa ini pale ugonjwa utapogundulika mapema.
Ni Zipi Dalili Za Hepatitis D?
Homa ya ini ya hepatitis D mara nyingi haioyeshi dalili. Pale zitakapojitokeza zaweza kuwa:
. Kugeuka rangi kwa ngozi na macho kuwa njano, hali iitwayo jaundice
. Maumivu kwenye maungio ya mifupa
. Maumivu ya tumbo
. Kutapika
. Kukosa hamu ya kula
. Mkojo mweusi
. Uchovu
Dalili za hepatitis B na D zinafanana, hivyo inaweza kuwa vigumu sana kutofautisha ni ugonjwa upi unaokusumbua. Wakati mwingine, hepatitis D hukuza dalili za hepatitis B. Inaweza vile vile kusababisha dalili kwa mgonjwa wa hepatitis B ambaye hakuwahi kuwa na dalili.
Mtu Anapataje Hepatitis D?
Kama tulivyosema, homa ya ini ya hepatitis D husababishwa na kirusi, HDV. Ni kirusi anayeambukiza kwa kugusa moja kwa moja majimaji ya mwili wa mtu mwenye ugonjwa huo. Inaweza kuambukiza kupitia:
. Mkojo
. Majimaji ya ukeni
. Shahawa
. Damu
. Wakati wa kuzaliwa (kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto)
Ukiwa na hepatitis D unaweza kuwaambukiza wengine hata kabla ya dalili kukutokea. Hata hivyo, unaweza kupata hepatitis D iwapo tu ulishawahi kuugua hepatitis B. Inaaminika kuwa asilimia 5 ya watu wenye hepatitis B huendelea kupata hepatitis D.
Mazingira hatarishi kwa ugonjwa huu ni:
. Kuwa na hepatitis B
. Wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja
. Kuongezewa damu mara kwa mara
. Matumizi mabaya ya dawa za sindano, pamoja na heroin
Ni Nini Tiba Ya Hepatitis D?
Hakuna tiba inayoeleweka kwa ugonjwa wa homa ya ini wa hepatitis D ambao ni mkali au uliokwisha fikia kuwa sugu. Tofauti na aina nyingine za hepatitis, madawa ya kuangamiza virusi hayaonyeshi kufanya kazi kwa ugonjwa huu.
Kama tulivyokwisaha sema, hepatitis D haina tiba. Kwa hiyo uchunguzi wa mapema ni muhimu ili kulingika ini. Inatakiwa kumwona daktari mara unapohisi kuwa na hepatitis. Hepatitis D isipodhibitiwa mapema inaweza kuleta madhara ya kudumu kama:
. Makovu kwenye ini (cirrhosis)
. Ugonjwa wa ini
. Kansa ya ini
Watu wenye hepatitis D sugu wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata madhara haya ya kudumu.
Ukiwa na cirrhosis au aina nyingine ya madhara ya kudumu, unaweza kulazimika kufanyiwa upasuaji wa kubadilishiwa ini. Upasuaji huu ni mkubwa ambapo ini lako lililoharibika litaondolewa na utawekewa ini zuri kutoka kwa mtu mwingine. Ikiwa upasuaji huu wa kubadilisha ini umekuwa ni wa lazima, karibu asilimia 78 ya wahanga huishi miaka 5 au zaidi baada ya upasuaji.
Tunakukaribisha msomaji wetu kutoa maoni yako au kuuliza maswali uliyo nayo kuhusu mada yetu ya leo. Tutafurahi sana kukujibu na kwa wakati mwafaka. Katika mada yetu nyingine tutaujadili ugonjwa wa kifafa.
Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.