Parkinson’s disease ni ugonjwa wa neva unaoanza na kukua taratibu na kuathiri matumizi ya maungo ya mwili. Dalili huanza taratibu kwa mkono mmoja kuanza kutetemeka kwa mbali. Parkinson’s disease ni ugonjwa unaoweza kusababisha kukakamaa kwa misuli au kupunguza kasi ya mwendo.
Katika hatua zake za mwanzo, mgonjwa anaweza akaonyesha kwa mbali au akashindwa kabisa kuonyesha hisia zake usoni. Mikono inaweza ikashindwa kucheza wakati akitembea. Kuzungumza kukawa kwa shida na hali ya ugonjwa ikawa inazidi kuwa mbaya zaidi siku zikisogea.
Pamoja na kuwa ugonjwa huu hauna tiba, matumizi ya dawa yanaweza kupunguza baadhi ya dalili. Mara nyingine daktari anaweza kushauri upasuaji ili kurekebisha baadhi ya sehemu za ubongo.
Dalili Za Parkinson’s Disease
Dalili na viashiria vya ugonjwa huu huweza kuwa tofauti kwa watu tofauti. Dalili za mwanzo huweza kuchukua muda mrefu bila kutambulika. Kwa kawaida, matatizo huanzia upande mmoja na huendelea kuwa mabaya zaidi upande huo huo mmoja, hata baada ya kuwa upande wa pili umeanza kuathirika.
Dalili za parkinson’s ni pamoja na:
Kutetemeka. Kutetemeka huanzia kwenye mkono au vidole. Unaweza kujikuta unavisugua dole gumba na kidole cha shahada (pill-rolling.) Mkono wako unaweza kutetemeka ukiwa umetulia.
. Kupungua uwezo wa kuvimudu viungo (bradykinesia). Baada ya muda utajikuta umepungukiwa kasi ya vitendo vya mwili na kufanya shughuli ndogo tu ikachukua muda mwingi sana. Hatua zako zinaweza kuwa fupi ukitembea. Utapata shida kunyanyuka kwenye kiti. Unaweza kuburuza miguu wakati ukitembea.
. Kukakamaa kwa misuli. Kukakamaa kwa misuli kunaweza kujitokeza kwenye sehemu yo yote ya mwili. Kukakamaa kunaweza kuambatana na maumivu na kukufanya ushindwe kukamilisha vitendo vya mbali.
. Mkao na kuyumba. Unaweza kupinda mgongo kuanzia kiunoni ukainamia mbele, au ukawa na matatizo ya kuyumbayumba.
. Kusimama vitendo vinavyojiendesha. Vitendo vinavyojiendesha kama kukonyeza, kutabasamu, kutupa mikono utembeapo vitapungua.
. Mabadiliko ya uzungumzaji. Unaweza kuanza kuzungumza taratibu, haraka haraka au kwa kusitasita. Zungumza yako inaweza kuwa ya sauti moja bila vionjo.
. Mabadiliko ya uandishi. Unaweza kupata ugumu katika kuandika na maandishi yako yakawa madogo.
Chanzo Cha Parkinson’s
Kwenye hali ya ugonjwa wa Parkinson’s, seli fulani za neva (neurons) katika ubongo huvunjika au kufa. Dalili nyingi zinatokana na upungufu wa neurons ambazo hutengeneza kemikali ya utoaji taarifa iitwayo dopamine. Kiwango cha dopamine kikiwa chini, utendaji kazi wa ubongo huwa si wa kawaida, hali ambayo husababisha ugonjwa wa Parkinson’s.
Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakieleweki, lakini kuna baadhi ya vipengele vinavyochangia, ambavyo ni pamoja na:
. Sababu za kijenetiki
. Sababu za mazingira
Utafiti umeonyesha pia kuwa kuna mabadiliko mengi ndani ya ubongo wa mtu mwenye ugonjwa wa Parkinson’s, ingawa bado hawajaweza kujua sababu za mabadiliko hayo. Mabadiliko hayo ni pamoja na:
Vitu Vinavyochangia Parkinson’s
. Umri. Watu wazima ndiyo wanaopata ugonjwa huu. Unaanzia kwa watu wa umri wa kati au baadaye kwenye maisha. Watu huupata ugonjwa huu wanapokuwa na umri wa miaka kama 60 au zaidi.
. Urithi. Kuwa na ndugu wa karibu mwenye ugonjwa huu kunaongeza uwezekano wa wewe pia kuupata. Lakini yamkini ni ndogo hadi uwe na ndugu wengi wenye tatizo hili kwenye familia yako.
. Jinsia. Wanaume wanapata ugonjwa huu zaidi ya wanawake.
. Sumu. Kuwa kwenye mazingira ya madawa ya kuulia majani na wadudu kwa muda mrefu kunaweza kukuongezea uwezekano wa kuugua.
Madhara Yatokanayo na Parkinson’s
Ugonjwa wa parkinson’s huambatana na matatizo mengine, ambayo hutibika:
. Ugumu wa kufikiri. Unaweza kupata matatizo ya kutambua na kufikiri. Matatizo haya mara nyingi hujitokeza kwenye hatua za mwisho za ugonjwa. Matatizo haya ya utambuzi huwa hayasikii dawa.
. Mfadhaiko na mabadiliko ya hisia. Unaweza kusikia mfadhaiko, wakati mwingine kwenye hatua za mwanzo za ugonjwa. Tiba ya mfadhaiko inaweza kurahisisha uondoaji wa changamoto nyingine za parkinson’s.
Unaweza kupata mabadiliko mengine ya hisia, kama woga, wasiwasi, au kukosa motisha. Madaktari wanaweza kukusaidia kukupatia tiba ya matatizo haya.
. Matatizo ya kumeza. Unaweza kupata matatizo ya kumeza kadiri ugonjwa unavyozidi. Mate yanaweza kujazana mdomoni kwa sababu ya kupungua kwa kasi ya kuyameza na kusababisha kuchuruzika.
. Matatizo ya kutafuna na kula. Hatua za mwisho za parkinson’s huathiri misuli ya kwenye mdomo, na kufanya utafunaji kuwa mgumu. Hali hii huweza kusababisha lishe duni.
. Matatizo ya kulala. Watu wenye parkinson’s mara nyingi hupata matatizo ya kulala, ikiwa ni pamoja na kuamka mara nyingi usiku, kuamka mapema sana asubuhi au kulala mchana.
. Matatizo ya kibofu. Ugonjwa wa parkinson’s huweza kuleta matatizo ya kibofu, ikiwa ni pamoja na kushindwa kuudhibiti mkojo au shida kupata haja ndogo.
. Tumbo kujaa. Watu wengi wenye parkinson’s hupata matatizo ya choo kigumu kwa sababu ya kupungua kwa uyeyushwaji wa chakula.
Unaweza kuona pia :
. Mabadiliko ya Pressure.
. Matatizo kusikia harufu.
. Uchovu.
. Maumivu.
. Shida ya tendo la ndoa.
Katika mada yetu nyingine tutauzungumzia ugonjwa wa kifafa. Uwe huru kuuliza maswali uliyo nayo au kutoa ushauri ulio nao kuhusu uandishi wa mada zetu.
Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya muda wa kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.