Malaria ni ugonjwa unaotishia maisha ya binadamu, unaoenezwa na mbu jike mwenye maambukizo, wa jamii ya anopheles. Ugonjwa wa malaria unazuilika na unatibika.
Katika mwaka 2016 pekee kulikuwa na wagonjwa milioni 216 wa malaria kutoka nchi 91 duniani. Vifo kutokana na malaria vilifikia 445 000 mwaka 2016.
Mgonjwa huambukizwa kwa kuumwa na mbu jike mwenye vimelea vya plasmodium. Mbu akikuuma, vimelea huingia na kusambaa kwenye mfumo wako wa damu. Kuna spishi zaidi ya 400 za plasmodium, wanaoweza kuambukiza aina nyingi za wanyama kama wanyama wa ngeli ya reptilia, ndege, na wengineo. Spishi nne za palsmodium zimetambulika siku nyingi kueneza malaria kwa binadamu. Kuna spishi moja ambayo kwa kawaida huwaambukiza nyani ambayo kwa siku za karibuni imegunduliwa kuwa ni chanzo cha zoonotic malaria kwa binadamu.
Spishi zinazoambukiza binadamu ni:
P.falciparum, anayepatikana dunia nzima kwenye maeneo yenye joto kali na maeneo ya joto kiasi, na hasa Afrika. P.falciparum anaweza kuleta malaria kali kwa sababu anazaliana kwa kasi sana ndani ya damu, na kusababisha upungufu mkubwa wa damu. Pia vimelea hawa wenye maambukizo, huweza kuziba mishipa midogo ya damu. Hali hii ikitokea ndani ya ubongo, celebral malaria hutokea, ugonjwa unaoweza kuua.
P. vivax, anayepatikana hasa Asia, Marekani ya Kusini, na kwenye baadhi ya maeneo ya Afrika. Kwa sababu ya uwingi wa watu , hasa barani Asia, huyu ndiye anayefahamika zaidi. P.vivax (P.ovale) ana vipindi vya kutulia kwa muda (dormant stages) katika maini (hypnozoites) ambapo anaweza kuamka na kushambulia damu miezi au miaka kadhaa baada ya kuumwa na mbu.
P. ovale, anapatikana zaidi Afrika (hasa Afrika Magharibi. Huyu anafanana sana kimaumbile na kibayolojia na P.vivax. Tofauti na P.vivax, huyu Ana uwezo wa kushambulia baadhi ya watu ( individuals who are negative for the Duffy blood group), ambao wengi ni wakazi wa maeneo ya Afrika ya sub-saharan. Hii inaeleza kwa nini P.ovale anajulikana zaidi ya P.vivax barani Afrika.
P. malariae, anayepatikana dunia nzima ndiye kimelea pekee wa malaria mwenye mzunguko wa siku tatu – quartan cycle or three-day cycle. Spishi nyingine za hapo juu zina mzunguko wa siku mbili. Kama tiba haitatolewa, P.malariae husababisha maambukizo sugu ambayo mara nyingine hudumu maisha yote ya mgonjwa. Kwa watu wenye maambukizo sugu, P.malariae anaweza kusababisha nephrotic syndrome (uharibifu wa mishipa midogo ya damu ndani ya figo).
P. knowlesi, anapatikana maeneo yote ya kusini mashariki mwa Asia kama kimelea anayeshambulia aina fulani za nyani. Amebainishwa kuambukiza zoonotic malaria katika maeneo hayo, hasa Malaysia.
Kusambaa Kwa Malaria
Karibu mara zote, malaria husambaa kwa kuumwa na mbu jike wa jamii ya anopheles. Kuna spishi tofauti zaidi ya 400 za mbu huyu, na spishi yapata 30 ni wasambazaji wa malaria wanaojulikana. Mbu hawa wasambazaji huanza kuuma giza linapoingia hadi kunapopambazuka. Kasi ya usambazaji hutegemea aina ya kimelea, aina ya mbu msambazaji, binadamu anayeumwa, na mazingira.
Anopheles hutaga mayai yao kwenye maji, ambayo hujiangua na kuwa larvae, na baadaye kutoka kama mbu kamili. Mbu jike huhitaji mlo wa damu ili kutunza mayai yake. Kila jamii ya mbu ana mazingira anayoyapenda zaidi, kwa mfano, wengine hupenda vidimbwi vidogo visivyo na kina kama alama za nyayo, vinavyopatikana vipindi vya mvua kwenye nchi za tropiki. Katika maeneo mengi, usambaaji ni wa msimu, ukifikia kilele wakati fulani na mara nyingi baada ya msimu wa mvua. Mlipuko wa malaria unaweza kutokea pale hali ya hewa na vitu vingine vitakapochangia usambaaji kwenye maeneo yenye watu wenye kinga za mwili dhaifu au wasio na kinga dhidi ya malaria. Milipuko pia hutokea watu wenye kinga dhaifu wanapoingia maeneo yenye malaria kwa wingi, pale wanapokwenda kutafuta kazi, au kama wakimbizi.
Baada ya kuumwa na mbu, kuna siku 7 hadi 30 ndipo dalili zitakapoanza kujionyesha (incubation period). Incubation period ya P.vivax ni siku 10-17 ingawa inaweza kuwa ndefu zaidi (kama mwaka mmoja, au mara chache hadi miaka 30). P.falciparum kwa kawaida ana incubation period fupi zaidi (siku 10-14). Spishi nyingine za plasmodium zinazoleta malaria zina incubation period sawa na ile ya P.vivax.
Vimelea wa malaria wakiisha ingia ndani ya mwili wako, husafiri hadi kwenye maini, ambako watakua na kukomaa. Baada ya siku chache, vimelea wataingia ndani ya mfumo wa damu na kuanza kuambukiza chembechembe nyekundu za damu. Katika muda wa saa 48 hadi 72, vimelea ndani chembechembe nyekundu za damu huzaliana na kusababisha chembechembe hizo kupasuka.
Vimelea huendelea kushambulia chembechembe nyekundu za damu, na kuleta dalili zinazojirudia kwenye vipindi vya siku mbili hadi tatu.
Mama mjamzito anaweza kumwambukiza kichanga wakati wa kuzaa. Hii huitwa congenital malaria. Malaria husamabazwa kupitia damu, kwa hiyo mtu anaweza kuambukizwa kupitia:
. Kuwekewa kiungo kipya
. Kuwekewa damu
. Kuchangia sindano au vitu vingine vinavyotoboa ngozi.
Dalili Za Malaria
Dalili za malaria kwa kawaida huanza kuonekana siku 10 hadi wiki nne baada ya kuambukizwa. Wakati mwingine dalili zinaweza zisionekane kwa miezi kadhaa. Jamii zingine za vimelea huweza kuingia mwilini na zikatulia kwa muda mrefu. Dalili za kawaida za malaria ni pamoja na:
. Kutetemeka kwa baridi
. Homa kali
. Kutoka jasho jingi
. Kichwa kuuma
. Kichefuchefu
. Kutapika
. Maumivu ya tumbo
. Kuharisha
. Kupungukiwa damu
. Maumivu ya misuli
. Degedege
. Kupoteza fahamu
. Damu katika kinyesi.
Madhara ya Malaria
Malaria inaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya ya binadamu. Yafuatayo yanaweza kutokea:
. Kuvimba kwa mishipa ya damu ya kwenye ubongo, au malaria ya ubongo
. Kujaa maji kwenye mapafu au pulmonary edema
. Kushindwa kufanya kazi kwa figo, maini, au bandama
. Upungufu wa damu (anemia) kutokana na kuharibiwa kwa seli za damu
. Upungufu wa sukari mwilini.
Tiba Ya Malaria
Tiba ya malaria inalenga kuondoa vimelea wa plasmodium kutoka kwenye mfumo wa damu wa mgonjwa.
Mchanganyiko wa Artemisinin – Artemisinin-based combination therapy (ACT) – ndiyo tiba inayoshauriwa na WHO kutiba malaria za kawaida. ACT inatolewa pamoja na dawa nyingine. Kazi ya artemisinin ni kupunguza idadi ya vimelea katika siku 3 baada ya maambukizi, wakati dawa mwenza huwamalizia vimelea hao.
Matumizi ya artemisinin kona zote za dunia yamesaidia sana kupunguza malaria, lakini ugonjwa huo unazidi kuwa sugu kwa dawa hii. Sehemu ambazo vimelea wameshajijengea usugu kwa dawa hii, inashauriwa kutoa dawa nyingine yenye nguvu.
Lakini wakati mwingine daktari anaweza kutoa dawa nyinine kulingana na aina ya kimelea uliye naye. Vimelea wa malaria huweza hujenga usugu kwa dawa za aina fulani. Hali hiyo ikibainika, daktari anaweza kukuandikia zaidi ya aina moja ya dawa.
Baadhi ya vimelea, kama P.vivax na P.ovale, wana hatua ya kukaa ndani ya maini ambapo vimelea huishi humo kwa muda mrefu na kuzinduka baadaye. Ukibainika kuwa aina hizi za vimelea, daktari atakupa dawa ya kuzuia mashambulio ya malaria ya baadaye.
Tunakuomba ndugu msomaji kutoa maoni yako kuhusu uandishi wa mada yetu ya leo. Vilevile, jisikie huru kuuliza maswali pale ambapo hujaelewa. Katika mada nyingine tutajadili kuhusu magonjwa kisukari na high blood pressure.
Kwa maswali na msaada wa ziada wa kukabiliana na ugonjwa huu wa pumu, wasiliana nasi kwa kupitia anuani yetu promota927@gmail.com au unaweza kutupigia simu moja kwa moja kutumia nambari 0655 858027 au 0756 181651 au jaza fomu chini ya ukurasa huu.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.