Ulishakwenda hospitali ukaambiwa kuwa mifupa imesagika au ute umekwisha? Maneno haya yanaelezea tatizo la kiafya ambalo kitaalamu huitwa osteoarthritis. Osteoarthritis ni ugonjwa wa maungio ya mifupa (joints). Ugonjwa wa osteoarthritis huonekana zaidi umri wa mtu unapokuwa mkubwa. Kabla ya umri wa miaka 45, ugonjwa huu unaonekana zaidi kwa wanaume. Baada ya 55, ugonjwa huonekana zaidi kwa wanawake. Osteoarthritis hufupishwa OA na majina mengine ni degenerative arthritis au degenerative joint disease.Tofauti na aina nyingine za arthritis, kama rheumatoid arthritis na systemic lupus, osteoarthritis haishambulii sehemu nyingine za mwili.
Osteoarthritis hushambulia zaidi mikono, miguu, uti wa mgongo, na maungio yanayobeba uzito mkubwa kama nyonga na magoti. Primary osteoarthritis ni pale chanzo cha ugonjwa hakifahamiki na kama chanzo kinaeleweka ugonjwa huu huitwa secondary osteoarthritis.
Chanzo Cha Osteoarthritis
Primary osteoarthritis, osteoarthritis ambayo haitokani na kuumia au magonjwa, kwa kiasi fulani ni sehemu ya kuzeeka kwa maungio ya mifupa (joint.) Umri ukiwa mkubwa, uwiano wa maji katika gegedu (cartilage) huongezeka, na protini inayojenga cartilage hupoteza ubora wake. Hatimaye gegedu hupoteza muundo wake wa asili na uiamara wake. Kwenye hatua za mbali za osteoarthritis, gegedu inayofunika mifupa ya pande mbili kwenye maungio hupotea kabisa. Matumizi endelevu ya maungio haya yenye dosari husababisha mifupa kusuguana na kuleta maumivu na uvimbe. Uvimbe huu kwenye gegedu huweza kusababisha vijifupa vipya kuota (osteophytes) kuzunguka eneo la joint.
Secondary osteoarthritis ni namna ya osteoarthritis iliyotokana na ugonjwa mwingine au sababu nyingine. Hali ambazo zinaweza kuleta secondary osteoarthritis ni pamoja na unene, kuumia kwa mara kwa mara au upasuaji kwenye joint, dosari za kwenye maungio wakati wa kuzaliwa (congenital abnormalities), gout, kisukari na dosari nyingine za homoni.
Unene husababisha osteoarthritis kwa kuongeza mgandamizo kwenye joint na kwa hiyo kwenye gegedu. Baada ya kuzeeka, unene ndiyo chanzo kikubwa cha osteoarthritis ya kwenye magoti. Kujitokeza mapema kwa osteoarthritis baina ya wanyanyua vitu vizito kunaaminika kuchangiwa na miili yao mikubwa. Kuumia kwa mara kwa mara kwenye tishu za joint (ligamenti, mifupa , na gegedu) kunasadikika kuwa ni sababu ya osteoarthritis ya mapema baina ya wachezaji mpira na wanajeshi. Cha kushangaza, watu wa tiba wameshindwa kubainisha mwongezeko wa tatizo hili baina ya watu wanaokimbia mbio ndefu.
Kutuama kwa chembechembe (crystal deposits) kwenye gegedu kunaweza kusababaisha kuharibika kwa gegedu na kisha osteoarthritis. Chembechembe za tindikali ya uric huleta gout, wakati chembechembe za calcium pyrophosphate husababisha pseudogout.
Dalili Za Osteoarthritis
Dalili kubwa ya osteoarthritis ni maumivu kwenye eneo lililoathirika baada ya matumizi ya maeneo hayo. Maumivu huzidi baada ya shughuli za siku. Kunaweza kukatokea uvimbe, joto na sauti ya mifupa kugongana kwenye maeneo ya joint. Maumivu na kukakamaa kunaweza kutokea baada ya muda mrefu wa kutotumia viungo, kama vile kukaa kwenye ukumbi. Hali ikiwa mbaya sana, kukosekana kabisa kwa gegedu husababisha msuguano wa mifupa, na kuleta maumivu wakati mtu amepumzika au akifanya shughuli nyepesi.
Dalili hutofautiana kutoka mtu hadi mtu mwingine. Watu wengine watapata maumivu kidogo pamoja na kuwa vipimo vya X-ray vitaonyesha uharibifu mkubwa. Wakati mwingine dalili hutokea na kupotea. Si ajabu sana kwa mtu mwenye osteoarthrits ya mikono na magoti kutopata maumivu kwa miaka kadhaa na kisha yakamrudia tena.
Osteoarthritis ya uti wa mgongo huleta maumivu maeneo ya shingo na chini ya mgongo. Vijifupa vyenye ncha vinavyoota kufuata uti wa mgongo huchoma neva na kusababisha maumivu makali, ganzi na vitu kuchomachoma kwenye maeneo yaliyoathiriwa.
Aina Za Osteoarthritis
Cervical Osteoarthritis (Cervical Spondylosis)
Cervical spondylosis inahusu mabadiliko kwenye mifupa, discs, na joints za shingo. Mabadiliko haya hutokana na uchakavu wa kawaida kwa sababu ya umri. Umri ukiwa mkubwa, discs za uti wa mgongo eneo la shingoni hupoteza uimara, hupoteza ute,na kuwa kavu.
Discs na gegedu nyingine vikianza kupoteza ubora wao, vijifupa (spurs called ostephytes) huota kwenye mifupa ya shingo. Kuota huku huweza kusababisha kupungua kwa kipenyoa cha uti wa mgongo hali iitwayo spinal stenosis.
Cervical spondylosisi huanza kwenye umri wa kati au kwa watu wa umri mkubwa.
Hand Osteoarthritis
Hii ni osteoarhtritis ya kwenye mikono. Kwa mfano, ukipata maumivu wakati unajaribu kufunua gudulia, uwezekano mkubwa ni kwamba una tatizo la osteoarthritis ya mikono.
Shoulder Osteoarthritis (Degenerative Arthritis of the Shoulder)
Hii ni osteoarthritis ya bega. Bega hujengwa na joints mbili, acromioclavicular (AC) joint na glenohumeral joint. Joint ya AC ni plae clavicle inapokutana na acromion. Osreoarthritis mara nyingi hutokea kwenye joint hii.
Osteoarthritis of the Knee (Degenerative Arthritis of the Knee)
Hii ni osteoarthritis ya goti ambayo kwa kawaida hutokana na umri. Inaweza pia kutokana na sababu za kiurthi. Kuumia, maambukizi na uzito wa mwili ni sababu nyingine za kupata tatizo hili.
Tiba Ya Osteoarthritis
Tiba ya osteoarthritis inazingatia zaidi kupambana na dalili zilizokwishajitokeza. Tiba itakayokusaidia itategemea zaidi uzito wa dalili na sehemu ya mwili. Mara nyingi kubadili namna unavyoishi, dawa na mambo utakayoyofanya mwenyewe nyumbani vitakusaidia kuondokana na maumivu, uvimbe na kukakamaa kwa viungo.
Mambo Ya Kuyafanya Nyumbani Na mtindo Wa Maisha
Mazoezi
Mazoezi huivuta misuli inayofunika maungio ya mifupa na kupunguza kukakamaa. Jitahidi kutembeza viungo vyako kwa angalau dakika 20 hadi 30 kila siku kwa kutembea, kuogelea au shughuli nyingine. Mazoezi ya mnyumbuliko yatakuongezea uwezo wako wa kuvitumia viungo vyako kwa muda mrefu zaidi.
Kupunguza Uzito
Kuwa na uzito mkubwa kunachangia kuweka uzito juu ya maungio ya mifupa na kusababisha maumivu. Kupunguza uzito kutakusaidia vile vile kupunguza matatizo mengine ya kiafya, kama kisukari na magonjwa ya moyo.
Usingizi Wa Kutosha
Kuipumzisha misuli yako kutasaidia kupunguza uvimbe na maumivu.
Virutubishi
Tiba mbadala na virutubishi vinaweza kukupunguzia uvimbe na maumivu. Baadhi ya virutubishi na mimea vinavyosaidia ni pamoja na:
. mafuta ya samaki
. green tea
. tangawizi
. glucosamine
Chakula chenye ubora husaidia kupunguza dalili za osteoarthritis ikiwa ni pamoja na uvimbe. Kula chakula kifuatacho kutakusadida:
. vitamin C
. vitamin D
. beta-carotene
. omega -3 fatty acids
Katika kurasa nyingine tutazungumzia matatizo mengine yanayoshambulia maungio ya mifupa ya miili yetu. Tutapata nafasi ya kuzungumzia matatizo ya mifupa kukosa uimara (osteoporosis), rheumatoid arthritis na gout.
Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya saa za kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.