Ujue Ugonjwa Wa Candidiasis

 

candidiasis

 

Kuna aina nyingi sana za fungus wanaoishi ndani ya mwili wa binadamu. Moja ya aina hizo ni fungus aitwaye candida. Huyu ni aina ya yeast apatikanaye kwa kiwango kidogo na ambaye kwa kawaida anaishi kwenye midomo, tumboni au juu ya ngozi bila kuleta madhara. Lakini mazingira yanaweza yakabadilika na kusababisha akaongezeka idadi na kuanza kuleta madhara. Maambukizi haya huitwa candidiasis.

Candida yeast huyu akisambaa kwenye mdomo na koo, anaweza kusababisha maambukizi yanayoitwa thrush (oropharyngeal candidiasis). Hali ni inaonekana sana kwa watoto wachanga na watu wa umri mkubwa ambao wana upungufu wa kinga za mwili. Watu walio kwenye hatari ya kumpata yeast huyu ni:

. Watu walio kwenye tiba ya kansa
. Watu wanaotumia antibiotics
. Watu wenye meno bandia
. Watu wenye kisukari

Dalili Za Thrush:

. Vijidoa vyeupe au vya njano juu ya ulimi, lips, fizi, kuta za ndani za mdomo, kuta za ndani za  ya mashavu
. Wekundu kwenye midomo na kooni
. Kuchanika kwenye kingo za mdomo
. Maumivu wakati wa kumeza, kama imesambaa kooni

 

THRUSH IMAGE

 

 

Vaginal Candidiasis au Vulvovaginal Candidiasis (VVC)

 

Maambukizi ya yeast ukeni huitwa vaginal candidiasis. Wanawake 3 katika 4 hupata maambukizi haya katika maisha yao. Wanawake wengi hupata maambukizi haya angalau mara mbili. Maambukizi haya hutokea wakati aina hii ya fungus wanapoongezeka na kuzidi idadi. Kuongezeka huku kunatokana na mabadiliko katika uwiano wa uke yanayoweza kusababishwa na ujauzito, kisukari, matumizi ya dawa, vilainishi au kushuka kwa kinga za mwili. Mara chache maambukizi haya hutokana na kujamiiana.

Chanzo Cha Vaginal Candidiasis

Maambikizi ya ugonjwa huu yanasababishwa na yeast wa jamii ya Candida albicans, ingawa jamii nyingine za candida pia zinaweza kuleta maambukizi.

Bakteria na fungus aina ya yeast huishi kwa uwiano fulani katika uke, lakini mvurugiko wa uwiano huu dhalili unaweza kuleta mambukizi.

Kwa kawaida bakteria aitwaye Lactobacillus huweka mazingira ambayo huzuia mwongezeko wa yeast, lakini yeast akiweza kuyavuruga, anaweza kuongezeka na kuleta maambukizi. Maambukizi haya huonekana zaidi kwa wanawake wanaoshiriki sana ngono.

Mazingira yanayosababisha kuongezeka kwa yeast ni:

. Matumizi ya antibiotics
. Ujauzito
. Kisukari kisichodhibitiwa
. Upugufu wa kinga za mwili

Shughuli yo yote inayoleta mabadiliko kwenye mazingira ya uke, pamoja na kujiosha (douching), yanaweza kuchangia maambukizi ya yeast. Lishe duni na kukosa usingizi wa kutosha pia vinaweza kuwa na mchango.

Dalili Za Candidiasis

. Kuwashwa ukeni
. Wekundu au kuvimba ukeni na nje ya uke (vulva)
. Maumivu wakati wa haja ndogo
. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
. Uchafu mweupe, mzito kama jibini

 

Tiba Ya Candidiasis

 

Maambukizi ya yeast yanaweza kutibiwa kwa kutumia antifungal creams au vidonge.

Unaweza vile vile kujitibu kwa njia za kiasili. Njia ambazo zimetumika sana ni pamoja na:

. Mafuta ya nazi

 

Garlic Oil Softgel
DAWA KWA TATIZO LA FUNGUS UKENI

. Garlic (kitunguu saumu)
. Kunywa maziwa ya mgando au kuyaingiza ukeni

Katika mada nyingine ndani ya tovuti yetu tutazungumzia matatizo ya cytolitic vaginosis, trichomoniasis na bacterial vaginosis ambayo yanafanana na yote husababisha uchafu ukeni.

Usisite kuuliza maswali au kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo. Itakuwa furaha kubwa sana kwetu kukujibu.

 

Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.