Ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo ni wa hatari sana kwani unaweza kuua katika saa chache tu. Ni ugonjwa unaozuka sehemu mbalimbali ulimwenguni, na katika bara la Afrika umeua watu wapatao 100,000 katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.
Mlipuko wa kwanza wa meningitis ulitokea Geneva mwaka 1805, na katika bara la Afrika, kumbukumbu zinaonyesha mlipuko wa kwanza ulikuwa mwaka 1840. Imani iliyoenea hapo zamani ilikuwa ni ugonjwa uliotokana na hewa mbaya na kwamba haukuwa ni ugonjwa unaoambukiza.
Kupata tiba ya haraka ni muhimu, lakini pamoja na tiba ya haraka, maambukizo bado huweza kutokea na kuua. Kwa hiyo, kinga kwa kupata chanjo ni ndicho kitu bora zaidi.
Shirika la afya duniani – WHO – limepanga kuutokomeza ugonjwa huu ifikapo 2030.
Meningitis ni uvimbe unaotokea kwenye utando laini (meninges) unaozunguka ubongo na uti wa mgongo. Uvimbe ndani ya ubongo huitwa encephalitis ambao huweza kuwa ni mwendelezo wa meningitis au vikatokea vyote kwa wakati mmoja, hali ambayo huitwa meningoencephalitis. Ikitokea ubongo na uti wa mgongo vyote vikaathiriwa kwa wakati mmoja, neno encephalomyelitis hutumika.
Chanzo Cha Meningitis Ni Nini?
Meningitis huweza kutokea kwa sababu ya maambukizo au bila maambukizo. Kuna virusi, bakteria, fungi, na vimelea wa aina nyingi wanaoweza kuleta meningitis. Magonjwa yanayoweza kusababisha uvimbe mwilini bila maambukizo (kama systemic lupus erythematosus na Bahcet’s disease) yanaweza kusababisha aseptic meningitis (meningitis isiyotokana na bakteria.) Baadhi ya madawa huweza kusababisha aseptic meningitis, kama ibuprofen au antibiotic iitwayo trimethoprim-sulfamethoxazole.
Dalili Za Meningitis
Dalili za kawaida za meningitis huwa:
. Kuumwa kichwa
. Homa kali
. Shingo kukamaa
. Maumivu machoni ukiona mwanga (photophobia).
Ishara ambazo tabibu atazitazama wakati wa uchunguzi wa meningitis ni pamoja na ishara za Kernig na Brudzinski. Ishara ya Kernig hutazamwa ifuatavyo: Mgonjwa akiwa amelalia mgongo, mguu unakunjwa nyuzi 90 sehemu ya nyonga na goti kukunjwa nyuzi 90. Ikiwa mgonjwa atapata shida sana wakati wa kunyoosha goti lililokunjwa huku nyonga ikiwa bado imekunjwa nyuzi 90, hiyo ni ishara ya meningitis. Ishara ya Brudzinski hutazamwa ifuatavyo: Mgonjwa akiwa amelalia mgongo na miguu ikiwa imenyooshwa kitandani, tabibu atakinyanyua kichwa mbele sehemu ya shingo. Kama tendo hili litaifanya miguu kunyanyuka na kujikunja kwenye magoti, hii ni ishara ya meningitis.
Dalili za homa ya uti wa mgongo huweza kutokea ghafla na hufanana na mafua (flu.) Kwa mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 2, zinaweza kuwa:
. Homa kali ya ghafla
. Kukakamaa shingo
. Maumivu makali ya kichwa yasiyo ya kawaida
. Maumivu ya kichwa yanayoambatana na kichefuchefu na kutapika
. Kifafa
. Kutopenda mwanga
. Kukosa hamu ya kula au kiu
. Mabadiliko katika tabia, kama kuchanganyikiwa, kukosa usingizi na shida kuamka asubuhi. . . . Ukurutu
Dalili kwa watoto wadogo hazijitambulishi vizuri na zinaweza kuwa:
. Homa kali
. Kulia kila wakati
. Kusinzia muda mrefu zaidi
. Kutocheza
. kuchoka
. kukataa kula
. uvimbe utosini
. Kukakamaa kwa shingo na mwili
Aina Za Meningitis
Meningitis inaweza kuwa kali (acute meningitis) – ambapo ugonjwa unakuja ghafla na kudumu muda mfupi – au sugu (chronic) ambapo ugonjwa huanza taratibu na kudumu muda mrefu. Meningitis inayotokana na maambukizo ni pamoja na bacterial meningitis (kutokana na maambukizo ya bakteria), viral meningitis ( kutokana na maambukizo ya virusi ) na parasitic meningitis (kutokana na maambukizo ya vimelea).
Meningitis ya kuambukiza mara nyingi hutokana na kuwepo ndani ya jamii. Ni mara chache sana mgonjwa hupata bacterial na fungal meningitis kutokana na shughuli za kwenye mahospitali au za tiba.
Chanzo kikuu cha meningitis ni virusi ikifuatiwa na bakteria. Mara chache sana meningitis husababishwa na fungus. Maambukizo ya bakteria yanaweza kuwa hatarishi sana kwa maisha ya mgonjwa.
Homa Ya Uti Wa Mgongo Kutokana Na Bakteria – Bacterial meningitis
Bakteria wanaoiingia ndani ya mfumo wa damu na kusafiri hadi kwenye ubongo na uti wa mgongo husababisha homa kali ya uti wa mgongo. Lakini ugonjwa unaweza kutokea pale bakteria wanaposhambulia meninges moja kwa moja. Hili linaweza kutokea baada ya maambukizo kwenye sikio au pua, mvunjiko kwenye fuvu, na, mara chache baada ya upasuaji.
Kuna koo za bakteria wanaoweza kuleta meningitis kali, na hasa:
. Streptococcus pneumoniae (pneumococcus). Bakteria huyu ndicho chanzo kikuu cha homa ya uti wa mgongo inayotokana na bakteria kwa vichanga, watoto wadogo na watu wazima. Kwa kawaida huleta pneumonia au maambukizi kwenye masikio au pua. Chanjo yaweza kusaidia kuzuia aina hii ya meningitis.
. Neisseria meningitidis (meningococcus). Bakteria huyu ni moja ya wale wanaoongoza katika kuleta bacterial meningitis. Bakteria huyu huleta maambukizo kwenye sehemu ya juu ya mfumo wa upumuaji lakini pia anaweza kuleta meningococcal meningitis akiingia ndani ya mfumo wa damu. Wanaweza kuambukiza kwa haraka na huathiri zaidi vijana wa umri mdogo na wa kati. Wanaweza kuleta mlipuko kwenye mabweni ya shule na kambi za jeshi. Chanjo husaidia kuzuia ugonjwa huu.
. Haemophilus influenzae (haemophilus). Bakteria aitwaye Haemophilus influenzae type b (Hib) alikuwa ni kiongozi wa bacterial meningitis hapo zamani kwa watoto wadogo. Lakini baadaye sindano za Hib zimepunguza sana ugonjwa wa aina hii.
. Listeria monocytogenes (listeria). Bakteria hawa hupatikana ndani ya chakula ambacho hakikuchukuliwa tahadhari za kutosha kuua bakteria (unpasteurized cheeses, hot dogs and lunchmeats.) Wanawake wenye mimba, vichanga, wazee na watu wenye kinga ndogo za mwili, ndiyo wahanga wakuu.
Homa Ya Uti Wa Mgongo Kutokana Na Virusi – Viral meningitis
Homa ya uti wa mgongo kutokana na virusi kwa kawaida huwa si kali sana na mara nyingi mgonjwa hupona mwenyewe. Virusi kama herpes simplex virus, HIV, mumps, West Nile virus na wengine huweza kusababisha homa ya uti wa mgongo.
Chronic meningitis
Viumbe wakuao taratibu (kama fungi na Mycobacterium tuberculosis) ambao hushambulia ngozi laini na majimaji yanayozunguka ubongo husababisha meningitis sugu. Meningitis sugu hukua katika kipindi cha wiki mbili au zaidi. Dalili za chronic meningitis ni – maumivu ya kichwa, homa, kutapika na kichwa kuwa kizito.
Fungal meningitis
Homa ya uti wa mgongo kutokana na fangasi haionekani mara nyingi na husababisha meningitis sugu. Hufanana sana na meningitis kali ya bakteria. Meningitis ya fangasi haiambukizi kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Aina ya fangasi waitwao Cryptococcal meningitis ndiyo inayoonekana zaidi na huathiri zaidi watu wenye upungufu wa kinga za mwili, kama UKIMWI. Huweza kuwa tishio kwa maisha kama tiba ya fangasi haitatolewa.
Vyanzo Vingine Vya Homa Ya Uti Wa Mgongo
Homa ya uti wa mgongo huweza kusababishwa na vyanzo vingine ambavyo si vya maambukizo, kama kudhurika kutokana na dawa, mzio wa madawa, aina fulani za saratani na magonjwa kama sarcoidosis.
Mazingira Hatarishi Kwa Meningitis
Mazingira hatari kwa homa ya uti wa mgongo ni pamoja na:
. Kuruka sindano. Hatari hutokea pale mtu ye yote anapokosa kukamilisha sindano za utotoni au ukubwani alizoandikiwa. Mara nyingi viral meningitis hutokea kwa watoto wenye umri wa pungufu ya miaka 5. Bacterial meningitis ni kwa wale wenye umri chini ya miaka 20.
. Kuishi kwenye jumuia. Watoto wa shule waishio kwenye mabweni, wanajeshi, watoto kwenye maeneo ya kulelea watoto wapo kwenye hatari kubwa ya kupata meningococcal meningitis. Hii huenda ni kwa sababu bakteria huyu huenezwa kwa njia ya upumuaji, na kuenea kwa haraka kwenye makundi makubwa.
. Ujauzito. Ujauzito huongeza hatari ya listeriosis – maambukizi ya bakteria wa listeria, ambao wanaweza kasababisha meningitis. Listeriosis huongeza uwezekano wa mimba kutoka, kuzaa mtoto aliyefariki na kuzaa kabla ya muda.
. Upugufu wa kinga za mwili. UKIMWI, unywaji wa pombe, kisukari na vitu vingine vinavyochangia kupungua kwa kinga za mwili hukuweka kwenye hatari ya homa ya uti wa mgongo. Kuondolewa bandama pia kunachangia.
Madhara Ya Kudumu Ya Homa Ya Uti Wa Mgongo
Madhara huweza kuwa makubwa. Kadiri wewe au mtoto wako anavyokaa muda mrefu zaidi bila tiba, ndivyo uwezekano wa kupata kifafa na uharibifu wa kudumu wa neva unavyoongezeka, ikiwa ni pamoja na:
. Kupoteza uwezo wa kusikia
. Kupoteza kumbukumbu
. Kupoteza uwezo wa kujifunza
. Uharibifu wa ubongo
. Kifafa
. Figo kushindwa kufanya kazi
. Kifo
Namna Ya Kujikinga
Bakteria na virusi waletao homa ya uti wa mgongo wanaweza kuenezwa kupitia kukohoa, kupiga chafya, kubusiana na kushirikiana vyombo, mswaki au sigara.
Hatua zifuatazo zinaweza kusaidia:
. Kuosha mikono. Osha mikono yako kwa makini kuzuia kuenea kwa vijidudu. Wafundishe watoto wako kuosha mikono ipaswavyo kila wakati, hasa kabla ya kula, baada ya kujisaidia, baada ya kuwa kwenye makundi ya watu na baada ya kuchezea wanyama.
. Usafi. Usishiriki vinywaji, chakula, mirija, miswaki na mtu mwingine. Wafundishe watoto kutoshiriki vitu hivi.
. Kutunza afya. Linda kinga za mwili wako kwa kupata muda wa kutosha wa kujipumzisha, kufanya mazoezi mara kwa mara, na kula chakula bora chenye matunda mengi, mboga na nafaka nzima.
. Kuziba mdomo. Unapokohoa au kupiga chafya ziba mdomo wako na pua.
. Kama ni mjamzito, kuwa mwangalifu na chakula. Jilinde kwa kupika nyama kwa moto mkali (74C). Kuwa makini na jibini.
Katika mada yetu nyingine tutauzungumzia ugonjwa wa malaria. Usisite kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo au kuuliza maswali uliyo nayo.
Kwa maswali na msaada wa ziada wa kukabiliana na ugonjwa huu wa pumu, wasiliana nasi kwa kupitia anuani yetu promota927@gmail.com au unaweza kutupigia simu moja kwa moja kutumia nambari 0655 858027 au 0756 181651 au jaza fomu chini ya ukurasa huu.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.