Pelvic Infalammatory Disease (PID) ni maambukizo kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke. PID hutokea pale bakteria waenezwao kwa ngono wanaposambaa kutoka kwenye uke (vagina) hadi kwenye nyumba ya uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na ovari.
Dalili za PID huweza kuwa ni ngumu kueleweka. Baadhi ya wanawake hawaoni dalili zo zote. Kwa maana hiyo, unaweza usihisi cho chote hadi pale utakaposhindwa kupata ujauzito au hadi utakapoanza kupata maumivu ya kiuno.
Dalili Za PID
PID inaweza isilete dalili zo zote mbaya na ndogo zikitokea zinaweza kuwa ngumu kuzigundua. Baadhi ya wanawake hawapati dalili zo zote. Pale zinapojitokeza, zinaweza kuwa:
. Maumivu – yanayoweza kuwa madogo au makali – maeneo ya chini ya tumbo au nyonga
. Uchafu usio wa kawaida au mzito ambao unaweza kuwa na harufu mbaya
. Kutokwa damu kusiko kwa kawaida, hasa wakati wa tendo la ndoa, au katikati ya siku za hedhi
. Maumivu wakati wa kujamiiana
. Homa, wakati mwingine kusikia baridi
. Maumivu wakati wa haja ndogo, haja ndogo ya mara kwa mara au haja ndogo kutoka kwa shida.
Chanzo Cha PID
Kuna bakteria wa aina nyingi wanaoweza kusababisha PID, lakini maambukizo ya gonorrhea na chlamydia ndiyo yanayoonekana zaidi. Bakteria hao huambukiza wakati tendo la ndoa linapofanyika bila ya kutumia kinga.
Aghalabu, bakteria hawa huingia kwenye viungo ya uzazi vya mwanamke pale ulinzi wa kwenye shingo ya kizazi (cervix) unapovurugwa. Hii inaweza kutokea mathalani, wakati wa hedhi na baada ya kuzaa, mimba kuharibika au kutoa mimba. Mara chache bakteria huweza kujipenyeza wakati kifaa cho chote cha tiba kinapoingizwa kwenye nyumba ya uzazi.
Mazingira Hatarishi
Kuna vipengele ambavyo huweza kukuweka kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata PID, navyo ni:
. Kuwa mwanamke uliye chini ya miaka 25 unayeshiriki ngono
. Kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja
. Kuwa na mahusiano na mpenzi mwenye wapenzi zaidi ya mmoja
. Kufanya mapenzi bila kinga
. Kujisafisha na maji mara kwa mara
. Kuwa uliwahi kupata PID kabla au magonjwa mengine ya ngono
Madhara Yatokanayo Na PID
PID ambayo haikupata tiba inaweza kusababisha makovu na vifuko vyenye maji yenye wadudu kwenye mkondo wa njia ya uzazi ya mwanamke. Vitu hivi vinaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye viungo vya uzazi.
Madhara yanayoweza kutokea ni pamoja na:
. Mimba nje ya mirija (ectopic pregnancy). PID ndiyo sababu kubwa ya mimba kutunga nje ya kizazi. Mimba huweza kutunga nje ya kizazi endapo PID imesababisha makovu ndani ya mirija ya uzazi. Makovu haya husababisha yai lililopevushwa kushindwa kusafiri ndani ya mirija ya uzazi kuelekea kwenye nyumba ya uzazi. Badala yake yai hunata ndani ya mirija ya uzazi . Mimba nje ya kizazi husababisha utokaji wa damu usio wa kawaida unaoweza kukatisha maisha ya mwanamke.
. Ugumba. Uharibifu wa viungo vya uzazi huweza kusababisha ugumba – kushindwa kupata ujauzito. Kadiri unavyozidi kupata PID mara nyingi zaidi, ndivyo hatari ya ugumba inavyozidi. Kuchelewa kupata tiba ya PID kunaongeza hatari ya ugumba.
. Maumivu sugu ya nyonga. PID inaweza kusababisha maumivu ya nyonga yanayoweza kudumu kwa miaka mingi. Makovu ndani ya mirija ya uzazi na viungo vingine vya uzazi huweza kuleta maumivu wakati wa kujamiiana na wakati yai linadodondoshwa (ovulation).
. Tubo-ovarian abscess. PID huweza kusababisha kutunga kwa usaha na kufanya majipu ndani ya njia ya uzazi. Mara nyingi majibu haya hutokea ndani ya mirija ya uzazi na ovari, ingawa huweza kuota ndani ya nyumba ya uzazi na shingo ya kizazi. Kama tiba haitatolewa, unaweza kupata maambukizo hatarishi kwa maisha.
Tiba Ya PID
Tiba ya mara moja kwa kutumia dawa itaondoa maambukizo yaliyosababisha PID. Lakini, hakuna njia ya kukarabati makovu au uharibifu kwenye njia ya viungo vya uzazi uliotokana na PID. Tiba ya PID yaweza kuwa:
. Antibiotics. Daktari atakuandikia dawa inayoendana na chanzo cha tatizo lako. Utasubiri siku kama tatu kuona kama dawa ulizopewa zinafanya kazi.
. Kumtibu Mwezi wako. Kuzuia maambukizi, yafaa mwezi wako afanyiwe uchunguzi na atibiwe.
. Kuacha kushiriki ngono kwa muda. Acha kushiriki ngono hadi utakapomaliza tiba na kuona kuwa umepona.
Katika ukurasa wetu mwingine, tutauzungumzia ugonjwa wa kuziba kwa mirija ya uzazi. Usisite kutoa maoni kuhusu ukurasa huu au kuuliza maswali uliyo nayo.
Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.