Umuhimu Wa Zinc Katika Mwili

 

 

Zinc ni madini muhimu ambayo hutumika na mwili kwa njia zisizoweza kuhesabika. Zinc ni madini yanayoshika nafasi ya pili kwa uwingi katika mwili baada ya chuma na yanapatikana katika kila seli. Madini ya zinc ni kirutubishi cha lazima katika mwili na mwili hauna uwezo wa kuyatengeneza wala kuyatunza. Kwa sababu hiyo, mwili unahitaji kayapata madini haya kila wakati kutoka kwenye chakula tunachokula. Zinc hupatikana kwa wingi katika chakula kinachotokana na mimea na wanyama.

Katika mada yetu ya leo tutazungumzia kazi zinazofanywa na madini ya zinc katika mwili, vyanzo vya madini ya zinc kwa mwili na madhara yatokanayo na ukosefu wa madini ya zinc katika mwili.

Faida Za Zinc Katika Mwili

Utafiti umeonyesha kuwa madini ya zinc yana faida nyingi sana katika mwili. Zinc ni muhimu katika utendaji kazi wa vimeng’enya zaidi ya 300 vinavyosaidia shughuli za kimetaboliki, umeng’enyaji wa chakula, ufanyaji kazi wa neva na shughuli nyingine nyingi.

Zinc ni ya lazima katika ujenzi na utendaji wa seli za kinga za mwili.
Madini haya ni kiungo muhimu mno kwa afya ya ngozi, ujenzi wa DNA na uzalishaji wa protini.

Zinc hutakiwa pia katika kusikia ladha na harufu. Kwa sababu kimeng’enya kimoja ambacho ni cha lazima ili kupata ladha na harufu sahihi hutegemea zinc, upungufu wa zinc unaweza kuathiri uwezo wako wa kusikia ladha na harufu.

Kuimarisha Kinga Za Mwili

Zinc husaidia kuimarisha kinga za mwili. Kwa sababu zinc ni muhimu katika ufanyaji kazi wa seli za kinga za mwili, upungufu unaweza kusababisha kushuka kwa kinga za mwili. Supplements za zinc huamsha seli za kinga za mwili na kupunguza madhara ya free radicals.

Kwa mfano, gramu 80-92 za zinc kwa siku zilionyesha kupunguza urefu wa mafua kwa asilimia 33.

Supplements za zinc hupunguza uwezekano wa maambukizo na kuinua kinga za mwili kwa watu wazima.

Kuongeza Kasi Ya Uponyaji Wa Vidonda

Zinc kwa kawaida hutumika katika mahospitali kwa ajili ya kuponya madonda ya moto, baadhi ya vidonda na kuumia kwa ngozi.

Kwa sababu madini haya yana kazi muhimu na kubwa katika utengenezaji wa collagen, utendaji wa kinga za mwili na uvimbe, ni ya lazima katika uponyaji wa vidonda.

Ngozi ya mwili wa binadamu ina asilimia 5 ya zinc iliyomo katika mwili.

Uwezekano Wa Kupunguza Baadhi Ya Magonjwa Yanayoendana Na Umri Mkubwa

Zinc inaweza kupunguza baadhi ya magonjwa yanayoendana na umri mkubwa, kama pneumonia, maambukizo na age-related macular degeneration (AMD.) Zinc inaweza kuondoa madhara ya free radicals na kuimarisha kinga za mwili kwa kuamsha utendaji wa T-cells na natural killer celss, ambazo zinaweza kuulinda mwili dhidi ya maambukizo.

Watu wazima wanaotumia zinc hupata matokeo mazuri baada ya sindano za influenza, hupunguza yamkini yakupatwa na pneumonia na huimarika katika ufanyakazi wa ubongo.

Utafiti mmoja ulionyesha kuwa matumizi ya gramu 45 kwa siku ya zinc yaliweza kupunguza yamkini ya maambukizo kwa asilimia 66.

Katika utafiti mkubwa wa watu 4,200 waliotumia supplements za antioxidants – vitamini E, vitamini na beta-carotene -wakaongeza mg 80 za zinc walipunguza upoteaji wa uoni na kwa kiasi kikubwa walipunguza hatari ya AMD.

Yaweza Kusaidia Kutibu Chunusi

Chunusi hutokea kwa saababu ya kuzibwa kwa tezi zinazotengeneza mafuta, bakteria na uvimbe. Utafiti umeonyesha kuwa kutumia zinc (kunywa au kupaka juu ya ngozi) kunaweza kutibu chunusi kwa kupunguza uvimbe, kudhibiti kasi ya kuongezeka kwa bakteria wa P.acnes, na kusimamisha shughuli za tezi za mafuta.

Watu wenye chunusi wana viwango vidogo vya zinc mwilini, kwa hiyo supplements za zinc zinaweza kupunguza dalili hizo.

Afya ya uzazi

Zinc ni muhimu katika ukuaji na ufanyaji kazi wa viungo vya uzazi vya mwanamme. Wanaume wenye upungufu wa zinc wameonekana kuwa na korodani ambazo hazikukua sawasawa na kuwa na idadi ndogo ya mbegu.

Zinc husaidia utengenezaji wa homoni muhimu za uzazi, kama testosterone na prolactin. Zinc pia huwezesha uzalishwaji wa kiungo kikubwa cha majimaji ya tezi dume. Supplements za zinc zimetajwa kuwa tiba ya tatizo la jogo kushindwa kuwika (erectile dysfunction) kwa watu wenye magonjwa ya figo ya muda mrefu.

Kupunguza Uvimbe (Inflammation)

Zinc hupunguza madhara ya free radicals na kupunguza aina fulani za protini zinazoleta uvimbe katika mwili.

Free radicals husababisha uvimbe sugu, sababu kubwa ya magonjwa sugu, kama magonjwa ya moyo, saratani na magonjwa ya meno.

Dalili Za Upungufu Wa Zinc

Ingawa ni mara chache sana mtu anaweza kuwa na upungufu wa zinc, hali hiyo inaweza kutokea kwa sababu ya matatizo ya vinasaba, watoto wanaonyonya kwa akina mama wenye upungufu wa zinc, watu waliotawaliwa na pombe na mtu ye yote anayetumia dawa za udhibiti wa kinga za mwili.

Dalili zinazoweza kutokea ni pamoja na:

. ukuaji mdogo wa mwili
. kuchelewa kukomaa viungo vya uzazi
. kutosikia ladha au harufu
. kukosa hamu ya chakula
. madonda kuchelewa kupona
. kuharisha
. nywele kupunyuka
. kushuka kwa kinga za mwili
. dosari za kitabia
. ukuaji mdogo wa mwili
. ukurutu

Chakula Chenye Zinc Kwa Wingi

Chakula cha aina nyingi kinachotakana na wanyama au mimea kina uwingi wa zinc, hali inayofanya kuwa karibu kila mtu anapata zinc ya kutosha. Chakula chenye viwango vikubwa sana vya zinc ni pamoja na:

. Samaki wa magome: chaza, kaa, kome na kamba
. Nyama: nyama ya ng’ombe, nyama ya nguruwe, nyama ya kondoo na nyama ya nyati
. Batamzinga na kuku
. Samaki: Flounder, sadini, samoni na samaki bapa
. Jamii ya kunde: chickpeas, lentils, black beans, kidney beans n.k.
. Mbegu: mbegu za maboga, korosho, hemp seeds, n.k.
. Bidhaa za wanyama: maziwa, mtindi na jibini
. Mayai
. Nafaka nzima: shayiri, quinoa, brown rice n.k.
. Baadhi ya mboga: uyoga, kale, njegere, asparagus, na beet greens.

 

Katika mada nyingine tutazungumzia umuhimu wa calcium katika mwili. Usisite kutoa maoni yako au kuuliza maswali uliyo nayo.

 

Pata ushauri zaidi kwa kututumia ujumbe kupitia ukurasa huu hapa chini, kwa kujaza fomu, au kututumia barua pepe kupitia promota927@gmail.com au tupigie simu  ndani ya  saa za kazi  kwa namba zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.

 

Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.