
Upungufu wa damu ni hali ambapo mwili hauna chambachembe nyekundu za damu za kutosha ili kusambaza oksijeni sehemu zote za mwili. Mwili ukikosa kupata oksijeni ya kutosha kutoka kwenye damu yako, hautafanya kazi yake vizuri.
Chembechembe nyekundu za damu zina protini muhimu iitwayo hemoglobin. Protini hii hutunza oksijeni na huzisadidia chembechembe nyekundu za damu kuchukua oksijeni kutoka kwenye mapafu hadi kwenye mwili. Husadidia pia kuchukua kabini dayoksaidi kutoka mwilini hadi kwenye mapafu ili uweze kuitoa nje wakati wa kupumua.
Ili kuzitengeneza chembechembe nyekundu za damu na hemoglobin, mwili unahitaji kupata kila wakati madini ya chuma na vitamini. Bila madini ya chuma na vitamini, mwili hautatengeneza hemoglobin ya kutosha ili kusambaza oksijeni kwenye viungo. Ni kawaida kwa wanawake kupata upungufu wa damu wakiwa na ujauzito kwa sababu ya kukosa madini ya chuma na vitamini kwa kiwango cha kutosha.
Aina Za Upungufu Wa Damu Kwa Wanawake Wajawazito
Kuna aina tofauti za upungufu wa damu zaidi ya 400. Aina nyingine huonekana zaidi wakati wa ujauzito, nazo ni pamoja na:
. Iron-deficiency anemia, kutokana na kukosa madini ya chuma.
. Folate-deficiency anemia, kutokana na kukosa folic acid.
. VitaminB12 deficiency anemia, kutokana na kukosa vitamini B12.

Nani Anaweza Kupata Upungufu Wa Damu Wakati Wa Ujauzito?
Wakati wote wa kipindi cha ujauzito, kiwango cha damu katika mwili huongezeka kwa asilimia 20 hadi 30. Maana yake ni kwamba mwili unahitaji madini ya chuma zaidi kwa ajili kutengeneza chambechembe nyekundu za damu ningi zaidi. Unaweza kuwa kwenye hatari ya kupata upungufu wa damu endapo:
. Una mimba ya mapacha
. Hupati madini ya chuma ya kutosha katika chakula
. Kupata mimba za karibu
. Kupata hedhi nzito kabla ya ujauzito
. Kutapika mara kwa mara kutokana na morning sickness.
Jee, Ni Kawaida Kuwa Na Upungufu Wa Damu Wakati Wa Ujauzito?
Ndiyo. Kwa sababu uwingi wa damu huongezeka wakati wa ujauzito, upungufu mdogo ni wa kawaida. Upungufu wa madini ya chauma ni wa kawaida, ikiwa sailimia yapata 52 ya wanawake ikiathirika.
Upungufu wa damu mkubwa na hata ule wa kiasi uanatakiwa kupatiwa tiba ili kutunza afya ya kichanga aliyopo tumboni.
Upungufu Wa Damu Humuathiri Vipi Mtoto Tumboni?
Kichanga wa tumboni humtegemea mama katika kupata madini ya chuma, vitamini B12 na folic acid kwa kiwango cha kutosha. Upungufu wa damu unaweza kumuathiri kichanga, na hasa katika kipindi cha tatu cha ujauzito.
Endapo tatizo la upungufu wa damu halitatibiwa, kichanga atakuwa hatarini kuzaliwa na upungufu wa damu, hali ambay italeta matatizo katika ukuaji wake. Vile vile, upungufu wa damu unaongeza uwezekano wa mtoto kuzaliwa njiti na kuzaliwa akiwa na uzito mdogo.
Upungufu wa damu hauna uhusiano wa moja kwa moja na mimba kutoka, bali upungufu mkubwa unaweza kuleta matatizo mengine mengi.
Dalili Za Upungufu wa Damu Wakati Wa Ujauzito
Unaweza usisikie dalili yo yote mwanzoni. Baadaye unaweza kuona:
. Uchovu
. Baridi
. Kukosa pumzi.
Dalili nyingine ni pamoja na:
. Kizunguzungu au udhaifu
. Moyo kwenda mbio
. Kichwa kuuma
. Kupauka, ukavu wa ngozi
. Maumivu kwenye ulimi
. Miguu kuchezacheza.
Sababu za Upungufu wa Damu Wakati Wa Ujauzito
Ujauzito wenyewe ni sababu kwa sababu ya kuongezeka kwa ujazo wa damu. sababau nyingine ni kukosa madini ya chuma, vitamini B12 na folic acid katika chakula.
Sababu nyingine za upungufu wa damu wakati wa ujauzito ni:
. Baadhi ya magonjwa, ikiwa ni pamoja na sickle cell anemia na thalassemia
. Kuchangia damu
. Hedhi nzito kabla ya ujauzito
. Vidonda na uvimbe mbalimbali.
Tiba Ya Upungufu Wa Damu Wakati Wa Mimba

Tiba ya upugufu wa damu wakati wa mimba hutegemea uzito wa tatizo. Ukiwa na:
. Tatizo dogo au la wastani: Muuguzi atakupa dawa za kila siku za prenatal vitamin na madini ya chuma. Hivi vitakupa mahitaji yako ya kila siku ya madini ya chuma, vitamini B12 na folic acid.
. Tatizo Kubwa: Unaweza kutakiwa kuongezewa damu.
Mabadiliko katika ulaji yanaweza yakasaidia pia. Kula chakula chenye uwingi wa madini ya chuma kama spinach, nyama nyekundu na batamziga. Chakula cheye uwingi wa vitamini za kusaidia ufyonzwaji wa madini ya chuma (kama vitamini C) ni muhimu, pamoja na matunda, nyanya na pilipili.
Katika mada yetu nyingine tutajadili jinsi watoto mapacha wanavyopatikana. Usisite kutoa maoni yako kuhusu uandishi wa mada hii.
Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya saa za kazi kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.