Ikitokea watoto wawili wakakua katika nyumba ya mimba ya mwanamke kwa wakati mmoja, watoto hawa huitwa mapacha. Wakati mwingine wanaonekana kufanana katika hali zote, lakini wakati mwingine wanaonekana kama vile wanavyoonekana watoto wengine katika familia. Watoto mapacha hutokea kwa namna nyingi tofauti.
Fraternal twins
Ujauzito wo wote huanza na mbegu ya kiume lulirutubisha yai. Yai lililorutubushwa huitwa zygote. Wakati mwingine mwanamke hutoa mayai mawili na kila moja likarutubishwa na mbegu ya kiume tofauti. Haaaaapa mapacha wawili hutokea na mapacha wa aina hii huitwa fraternal twins, au dizygotic twins.
Wakati wa ujauzito, watoto hawa wanaokua hupata oksijeni na chakula kutoka kwa mama yao kupitia placenta na umbilical cords. Fraternal twins wana placenta tofauti na umbilical cords tofauti. Kitaalamu hii huitwa dichorionic
Fraternal twins wanaweza kuwa wa jinsia moja au jinsia tofauti na jeni (genes) zao ni tofauti kama ilivyo kwa kaka na dada wengine wa familia. Mara nyingi mapacha wa jinsia moja huonekana tofauti. Kwa mfano, wanaweza kuwa nywele au rangi tofauti. Mara chache sana huonekana sawa. Fratenal twins huwa karibia asilimia 70 ya mapacha wote.
Mama Mmoja Baba Tofauti
Kama mama na mayai mawili au zaidi wakati akiwa katika siku zake, inawezekana ikatokea kwamba kila yai likarutubishwa kwa wakati tofauti-na hata na wanaume tofauti. Kwa hiyo inawezekana mapacha weakazaliwa wakiwa na baba tofauti.
Identical Twins
Wakati mwingine yai ambalo limerutubishwa hujigawa siku chache baada ya kutunga mimba na kutengeneza mapacha walio na jeni sawa. Kwa sababu mapacha hawa walitokana na zygote moja, huwa wanaitwa monozygotic. Identacal twins huwa ni wa jinsia moja.
Kuna Aina 3 Za Identical Twins
Karibia theluthi moja ya identical twins hujigawa mra baada ya urutubishaji na kufanya mapacha walio tofauti kabisa. Kama ilivyo kwa fraternal twins mapacha hawa huwa na placenta tofauti.
Asilimia mbili zilizobakia hujigawa baada ya kunata kwenye kuta za mji wa mimba. Kwa hiyo wanachangia placenta. Kitaalamu hii huitwa monochorionic.
Kwenye idadi ndogo sana ya identical twins, kujigawa kunaweza kukatokea hata baadaye. Katika hali hii mapacha huchangia mfuko wa ndani uitwao amnion, pamoja na kuchangia placenta. Kitaalamu hawa huitwa monoamnionic twins. Mara nyingi huitwa MoMo twins.
Sababu Za Kupata Mapacha
Dawa za Uzazi
Wanawake walioshindwa kupata mimba huweza kushsuriwa na daktari kutumia dawa za kufanya ovari zao zitengeneze mayai mengi zaidi. Hii inaweza kuongeza uwezekano wa kupata mimba -na uwezekano pia wa kupata fraternal twins.
In Vitro Fertilization
Hii ni pale daktari anapochukua mayai kutoka kwenye ovari ya mwanamkem kwa kawaida baada ya kutumia dawa za uzazi. Mayai hurutubishwa na mbegu nje ya nyumba ya mimba, kisha kuwekwa tena ndani ya nyumba ya mimba. Kwa sababu ni kazi isiyotabirika, mayai yaliyorurtubishwa mawili au zaidi hurudishwa ili kuongeza yamkini kwamba angalau moja litakua. Wakati mwingine mayai mawili au zaidi hukua na mama atapata fraternal twins au watoto zaidi.
Umri Na Asili Ya Mama
Wanawake wenye umri wa miaka zaidi ya 30 wana yamkini kubwa zaidi ya kutoa mayai mawili au zaidi kwa wakati mmoja, kwa sababu miili yao inatengeneza homoni ya kuboresha ovari zao kwa wingi zaidi. Akina mama wamarekani weusi wana yamkini kubwa zaidi ya kupata mapacha kuliko weupe, wanawake wa Asia wakiwa mwisho katika mstari.
Urefu Wa Mama
Wanawake wenye mapacha wana wastani wa nchi moja ya urefu zaidi ya wengine. Homoni ambayo akina mama warefu wanayo zaidi -insulin-like growth factor au IGF – yaweza kuwa ndiyo sababu. Inawezekana kuwa IGF humfanya mwanamke kutoa mayai zaidi kutoka kwenye ovari.
Maziwa
Utafiti mmoja ulionyesha kuwa akina mama waliokunywa maziwa au kutumia bidhaa zinazotokana na maziwa zaidi walizaa mapacha zaidi. Baadhi ya wanasayansi wanafikiri kuwa bidhaa hizi zinasababisha kuzalishwa kwa IGF zaidi ambayo itasababisha kuwa na mayai mengi zaidi katika mzunguko wa mwezi.
Sababu Nyingine
Mwanamke mwenye mama au dada mwenye fraternal twins ana uwezekano mkubwa zaidi wa yeye pia kuwapata. Na wanawake wenye BMI kubwa wana uwezekano mkubwa wa kupata fraternal twins.
Katika mada yetu ifuatayo, Tutachambua sababu za ugumba kwa mwanamke. Usisite kutoa maoni yako kuhusu mada yetu ya leo, tutafurahi sana kukujibu swali lo lote ulilo nalo.
Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya saa za kazi kwenda nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.