Tatizo La Jogoo Kuwika – Erectile Dsysfunction
Kuna tatizo ambalo wengi huwa tunaliita ukosefu wa nguvu za kiume. Neno hili kama linavyotumika mimi naliona ni pana mno na halielezei hasa ni kitu gani kinamaanishwa kwani kuna matatizo lukuki ambayo yote yapo katika kundi la ukosefu wa nguvu za kiume. Leo tutazame tatizo ambalo limeliita tatizo la jogoo kushindwa kuwika au jongoo kushindwa kupanda mtungi. Kwanza tutazame muundo wa dhakari na nini kinatokea pale uume unaposimama.
Muundo Wa Dhakari
Dhakari ni kiungo cha uzazi cha mwanamme. Dhakari ina sehemu moja ndefu kuliko nyingine na mwishoni kuna kichwa (glans). Tundu lililopo kwenye kichwa (meatus) ni kwa ajili ya kutolea mkojo.
Ndani ya dhakari kuna vyumba viwili vyenye umbo la silinda vinavyoitwa corpora cavernosa vinavyotambaa urefu wote wa dhakari. Vyumba hivi vina uwingi wa mishipa ya damu. tishu na vifuko vya wazi. Mrija wa kupitisha mkojo na shahawa (urethra) unatambaa chini ya corpora cavernosa, ndani ya tishu zilizo kama sponji ziitwazo corpus spongiosum.
Ateri kuu mbili (moja ndani ya kila corpora cavernosa) na veni kadhaa zinatiririsha damu ndani na nje ya uume. Neva hupeleka taarifa kutoka na kwenda sehemu nyingine za mwili.
Nini Maana Ya Jogoo Kuwika (Uume kusimama)?
Tendo la uume kusimama huanzia ndani ya ubongo. Kutokana na kitu ulichokiona, ulichogusa, kunusa, kusikia au kuwaza, neva hupeleka taarifa za kikemikali kwenye mishipa ya damu iliyo ndani ya uume. Ateri zitalegea na kufunguka ili kuruhusu damu nyingi zaidi iingie, wakati huo huo veni zitaziba. Damu ikishakuwa ndani ya uume, msukumo huifanya damu inase ndani ya corpora cavernosa. Uume utatanuka na kuufanya uume usimame kwa muda mrefu.
Damu ikiacha kuingia ndani ya uume, veni zinafunguka, na uume unalegea.
Nini Maana Ya Jogoo kushindwa Kuwika
Hii ni hali inayomtokea mwanamme ambapo anakuwa na hamu ya kufanya tendo la ndoa lakini uume wake au hausimami kabisa, kukosa kusimama kikamilifu au kusimama kikamilifu kwa muda mfupi sana hivyo kukosa nguvu ya kufanya tendo lililokusudiwa. Nusu ya wanaume hupata tatizo hili wanapofikia umri wa miaka 40, idadi ikiongezeka kwa wanaume wenye umri mkubwa zaidi, kwa mfano asilimia 70 ya wanaume wenye miaka 70 huwa na tatizo hili. Ifahamike kwamba kila mmoja wetu huweza kupata tatizo hili kwa muda fulani kutokana na vitu kama uchovu, kupata kilevi, kutoelewana na mwenzi n.k. Tunasema mwanamme ana tatizo hili pale hali hii inapoendelea kwa kipindi kirefu, kwa mfano hali hii ikitokea kwa mwezi mzima mfululizo
Sababu Za Tatizo La Jogoo Kushindwa Kuwika
Kuna mengi yamesemwa kuhusu chanzo cha tatizo hili. Imani iliyoenea ni kwamba tabia ya vijana kujichua (kupiga nyeto) ndiyo inayosababisha tatizo hili. Mimi sijaona pahali wataalamu waliposema hivyo, nafikiri si kweli ukizingatia kwamba wataalamu wamekuwa wakiwashauri vijana kufanya hivyo kuliko kwenda seheme za machangudoa pale wanapozidiwa. Ukizingatia kwamba tendo la uume kusimama linahusisha ubongo, homoni, misuli na mishipa ya damu, tatizo katika hayo ndilo linaloweza kusababisha jongoo ashindwe kupanda mtungi. Baadhi ya sababu zinapelekea uume kutosimama au uume kukosa nguvu ni:
- Magonjwa ya moyo na kusinyaa kwa mishipa ya damu
- Unene wa kupindukia
- Ugonjwa wa kisukari
- Uvutaji wa sigara
- Utumiaji wa pombe
- High blood pressure
- Cholesterol nyingi katika damu
- Ugonjwa wa Parkinson’s
- Ugonjwa wa multiple sclerosis
- Upungufu wa homoni ya testosterone
- Tiba ya tezi dume
- Kuumia kwenye nyonga au uti wa mgongo
- Tiba ya mionzi kwenye eneo la nyonga
- Matatizo ya kisaikolojia
Madhara Ya Tatizo La Jongoo Kushindwa Kupanda Mtungi
Kuna madhara mengi yanayotokana na tatizo la jongoo kushindwa kupanda mtungi. Mwanamme anayepatwa na tatizo hili hushindwa kumridhisha mwenzi wake na hali hii huwezakusababisha matatizo makubwa katika mahusiano ya kimapenzi au katika ndoa. Hali hii hupelekea mwanamme huyu kuanza kuwa na wasiwasi na msongo wa mawazo, huanza kukosa kujiamini na kujiona ana mapungufu. Tatizo hili pia linasababisha mwanamme huyu ashindwe kumpa ujauzito mkewe.
Tiba Za Tatizo La Jogoo Kushindwa Kuwika
Ifahamike kwamba uume kusimama maana yake damu kuingia katika kiungo hicho, hivyo tiba ya uume kutosimama ni kutafuta njia ya kufanya damu ifike kwenye kiungo hicho kwa kiasi kinachotakiwa. Hii ni pamoja na kuondoa matatizo ya moyo, kupunguza unene, kupunguza cholesterol na kutumia dawa za kufungua njia za mishipa ya damu.
Njia nyingi zinatumika kuyafanya hayo hapo juu. Wenzetu hufanya hata upasuaji wa uume lakini kwetu sisi hilo bado sana. Kuna pampu zinauzwa kwa kusaidia damu ielekee na kujaza mishipa ya damu inayozunguka uume lakini hizi zinasaidia kwa muda mfupi. Dawa nyingine ambazo watu hutumia ni pamoja na viagra, Cialis na Levitra.
Ipo mimea mingi iliyothibitishwa kuwa inasaidia au kuponya kabisa tatizo la jongoo kushindwa kupanda mtungi na makampuni mbalimbali yamekuwa yakitengeneza dawa kutokana na mimea hiyo. Dawa hizo hupatikana kama vidonge au unga ambao hutumiwa kwa kunywewa kama chai au kahawa. Mimea maarufu iliyothibishwa ni pamoja na epimedium, ginseng na rhodiola rosea.
Mmea wa epimedium tutauzungumzia kwa kina katika ukurasa tofauti “Dawa Ya Jogoo Kushindwa Kuwika Ya Horny Goat Weed “. Wataalamu walibaini kuwa mmea huu ukikamuliwa hutoa icariin ambayo imetumika kutengeneza dawa ya kusaidia kuondoa tatizo la uume kushindwa kusimama kikamilifu. Dawa hii inatumika na watu wengi sana duniani.
Dawa nyingine ambayo inatumika na kuleta mafanikio makubwa katika kuondoa matatizo yanayowasumbua wanaume ni VIG POWER. Dawa hii inatokana na mimea ya Semen Cuscutae, Fructus Lycii, Rhixoma Diocoreae, Radix Rehmanniae Preparata na Cortex Moutan. Dawa hii huanza kuleta mabadiliko mwilini kwa muda mfupi sana na kumwezesha mwanamme kumudu tendo la ndoa, mara nyingi ikiwa katika muda wa dakika 30 tu.
Vig Power humwongezea uwezo wa kufanya tendo la ndoa mwanamme kwa:
1. Kuboresha figo
2. Kuongeza uwingi wa manii (Sperm count), kuongeza uwezo na kasi ya kutembea ya manii (Sperm Motility)
3. Kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanamme
4. Kuongeza uwingi wa oksijeni katika damu na kusaidia uume kusimama imara
5. Kuondoa tatizo la kuwahi kufika kileleni (Premature Ejaculation)
6. Kuondoa tatizo la jogoo kushindwa kuwika (Erectile Dysfunction)
7. Kuondoa tatizo la manii kutoka yenyewe pasipotarajiwa (spermatorrhea).
Katika kurasa nyingine tofauti tutajadili matatizo ya Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa wanaume, ugumba kwa mwanamme kutokana na kuwa na mbegu chache, tatizo la kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa wanawake na tatizo la kuwahi kufika kileleni mapema kwa wanaume.
Jee, una tatizo la jongoo kushindwa kupanda mtungi na ungependa kupata maelezo ya kina zaidi au kusaidiwa kupata dawa za kutumia? Usisite kuwasiliana nasi.
Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu ndani ya muda wa kazi kwenye nambari zifuatazo: 0 655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.