Blog
Sickle Cell Ni Ugonjwa Gani?
Sickle cell disease (SCD) ni kundi la maradhi ya kurithi ya chembechembe nyekundu za damu. Chembechembe nyekundu za damu zenye afya huwa za mviringo, na hutembea ndani ya mishipa midogo ya damu kusambaza oksijeni kwenye sehemu zote za mwili. Ndani ya mwili wa mtu mwenye ugonjwa wa sickle cell, chembechembe nyekundu za damu hugeuka kuwa ngumu na zinazonatanata na huwa na umbo la C, umbo linalofanana na kifaa cha shambani kiitwacho “sickle”. Seli hizi hufa mapema, hali ambayo husababisha mtu awe na upungufu wa damu kila wakati. Na, wakati seli hizi zikisafiri ndani ya mishipa midogo ya damu, hukwama na kuuziba mtiririko wa damu. Hali hii huweza kuleta maumivu makali na matatizo mengine makubwa kama maambukizi, acute chest syndrome na stroke.
Aina Za Sickle Cell Disease
Aina za ugonjwa wa sickle cell ambazo huonekana kwa wingi ni zifuatazo:
Kifua Kikuu (Tuberculosis-TB) Ni Ugonjwa Gani?
Kifua Kikuu (Tuberculosis) ni ugonjwa wa kuambukiza ambao mara nyingi hushambulia mapafu. Ugonjwa huu unachukua nafasi ya pili duniani ya vifo vinavyotokana na maambukizi yanayotokana na kitu kimoja. Ugonjwa wa kifua kikuu huenezwa na bakteria na kifua kikuu (TB) huenea kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia matone madogo yanayotolewa na mtu akikohoa au kupiga chafya. Awali, ugonjwa huu ulikuwa nadra katika nchi zilizoendelea, lakini maambukizi yalianza kuongezeka mwaka 1985, kwa namna fulani yakichangiwa na kuibuka kwa HIV, virusi waletao UKIMWI.
Vizazi vingi vya bakteria wa tuberculosis vimekuwa sugu kwa dawa ambazo zilikuwa zikitumika kuuponya ugonjwa huo. Watu wenye ugonjwa huo wanawajibika kutumia dawa za aina nyingi kwa muda mrefu ili waweze kupona.
Katika miaka ya katikati ya karne za 18 na 19, kulitokea milipuko ya ugonjwa huu huko Ulaya na Marekani Ya Kaskazini, kabla ya mwanasayansi kutoka Ujerumani, Robert Koch, kumgundua bakteria anayesababisha kifua kikuu mwaka 1882.
Kufuatia ugunduzi wa Robert Koch, ugunduzi na utumiaji wa chanjo na dawa za kuponya kifua kikuu ulileta imani kuwa ugonjwa huu ungetokomezwa. Mara moja Shirika la Umoja Wa Mataifa lilibashiri kuwa ugonjwa huu utakuwa umetokomezwa kufikia 2025.
Lakini katika miaka ya kati ya 1980 na 1990, TB iliongezeka kwa kasi duniani, hivi kwamba mwaka 1993 Shirika La Afya Duniani (WHO) lilitangaza hali ya hatari, kwa mara ya kwanza kabisa ugonjwa kutangazwa kwa namna hiyo.
Kwa bahati nzuri, kwa kufuata tiba kikamilifu, watu wengi waliopata TB hupona. Bila kupewa tiba nzuri, katika idadi ya wagonjwa wote wa TB, wagonjwa wafikiao hadi theluthi mbili watafariki dunia.
Tuberculosis Ni Nini?
Madakatari hutofautisha kati ya aina mbili za maambukizi ya kifua kikuu: latent na active.
Latent TB – bakteria hubaki ndani ya mwili bila kuleta madhara. Hawatoi dalili zo zote, na hawaambukizi, lakini wanaweza kuja kuanza kuleta madhara.
Active TB – bakteria wanaleta madhara na wanaweza kuambukiza kwa wengine.
Inaaminika kuwa karibu theluthi moja ya watu duniani wana latent TB. Kuna asilimia 10 ya uwezekano wa watu hawa kupata active TB, uwezekano huo ukichagizwa na upungufu wa kinga za mwili au kukosa mlo wa kutosha au kuvuta sigara.
TB ni ugonjwa unaoshambulia watu wa rika zote na watu wa pande zote za dunia. Lakini ugonjwa huu hushambulia zaidi vijana na watu wanaoishi kwenye nchi zinazoendelea. Takwimu za 2012 zilionyesha kuwa asilimia 80 ya wagonjwa wa TB walitoka katika nchi 22 tu.
Kifua Kikuu Husambazwa Na Nini?
TB husambazwa na bakteria aitwaye Mycobacterium tuberculosis. Bakteria huyu husambaa kwenye hewa wakati mtu mwenye TB (ambaye mapafu yake yameshambuliwa) akikohoa, akipiga chafya, akitema mate, akicheka , au akizungumza.
TB huambukiza lakini siyo rahisi kuipata. Uwezekano wa kupata TB kutoka kwa mtu unayeishi au kufanya naye kazi ni mkubwa kuliko kutoka kwa mgeni. Watu wengi ambao tayari wamaeanza tiba sahihi angalau kwa wiki 2 hawaambukizi.
Toka antibiotics zilipoanza kutumika kutibu TB, baadhi ya aina ya bakteria hao wamegeuka sugu kwa dawa. Multidrug-resistant TB (MDR-TB) ni hali ambapo dawa haziwezi tena kuwaua bakteria wote, bakteria wanaosalia wakijijengea usugu wa dawa hiyo na dawa nyingine pia kwa wakati mmoja.
Multidrug-resistant TB (MDR-TB) inatibika kwa kutumia dawa za kipekee (very specific anti-TB drugs) ambazo ni chache na hazipatikani kirahisi. Katika mwaka 2012, karibu watu 450,000 walipata MDR-TB.
Watu wenye upungufu wa kinga za mwili huwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata active TB. HIV hudhoofisha kinga za mwili, na kuufanya mwili kupata shida ya kudhibiti bakteria wa TB. Watu wenye mchanganyiko wa HIV na TB wana uwezekano wa kupata active TB kwa kiwango cha asilimia 20-30 ukilinganisha na wale ambao hawana HIV.
Matumizi ya tumbaku yamedhihirika kuongeza uwezekano wa kupata active TB. Asilimia 20 ya TB duniani huhusishwa na matumizi ya tumbaku.
Dalili Za Kifua Kikuu
Wakati latent TB haina dalili zo zote, active TB huwa na dalili zifuatazo:
. Kukohoa, wakati mwingine kukiwa na makohozi au damu
. Kusikia baridi
. Uchovu
. Homa
. Kukonda kwa mwili
. Kukosa hamu ya kula
. Kutoa jasho usiku
Kifua kikuu huathiri hasa mapafu, lakini kinaweza kuathiri vile vile sehemu nyingine za mwili. Wakati TB imeathiri sehemu tofauti ya mwili, dalili zinaweza kubadilika. Bila kupata tiba, TB huweza kusambaa kwenye sehemu nyingine za mwili kupitia mfumo wa damu.
. Tb ikishambulia mifupa inaweza kuleta maumivu ya uti wa mgongo na kuharibu maungio ya mifupa
. TB ikishambulia ubongo husababisha meningitis
. TB ikishambulia maini na figo huweza kusababisha damu ndani ya mkojo
. TB ikishambulia moyo inaweza kuathiri uwezo wa moyo wa kusukuma damu na kusababisha cardiac tamponade ambayo inaweza kuua.
Tiba Ya Kifua Kikuu
Wagonjwa wengi wa TB wanaweza kupona kama dawa stahiki itakuwepo na kutolewa inavyopaswa. Aina ya dawa na urefu wa muda wa matumizi vitategemea umri wa mgonjwa, hali yake ya afya kwa ujumla, usugu wa mwili wake kwa dawa, kama TB in latent au active, sehemu yake ya mwili iliyoathirika (i.e mapafu, ubongo, figo)
Watu wenye latent TB wanaweza kuhitaji aina moja tu ya dawa, wakati watu wenye active TB (na hasa MDR-TB) watahitaji mchanganyiko wa dawa.
Antibiotics za TB hutakiwa kutumiwa kwa muda mrefu kidogo, muda wa wastani ukiwa ni miezi 6.
Matumizi ya dawa za kifua kikuu huweza kusababisha sumu kwa ini, ingawa ni mara chache hili kutokea, linapotokea, linaweza kuleta matatizo makubwa. Madhara ya dawa hizi yanapojitokeza, ni lazima taarifa itolewe kwa daktari. Madhara hayo ni pamoja na:
. Mkojo mweusi
. Homa
. Homa ya manjano
. Kukosa hamu ya kula
. Kichefuchefu na kutapika
Ni muhimu kwa mgonjwa kuhakikisha kuwa anamaliza dawa, hata kama dalili za TB zitakuwa zimeondoka. Bakteria waliosalia na kuvumilia tiba iliyotolewa wanaweza kugeuka sugu kwa tiba hiyo na kupelekea kupata MDR-TB hapo baadaye.
Kataka mada nyingine tatajadili kuhusu ugonjwa wa homa ya ini (hepatitis) .
Ndugu msomaji, usisite kutoa maoni yako au kuuliza maswali kuhusu mada hii. Tutafurahi kuwa nawe na kukujibu.
Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.
Chunjua Za Sehemu Za Siri – Genital warts – Tiba Ni Nini?
Genital warts – chunjua zinazoota seheme za siri – husababishwa na human papillomavirus. Kuna aina tofauti zaidi ya 100 za human papillomavirus (HPV) lakini ni aina kama 40 tu ya hizi ndizo zinazoweza kusababisha chunjua za sehemu za siri. Katika mada yetu ya leo tutaona dalili za genital warts na tiba za chunjua hizi za sehemu za siri.
Chunjua za sehemu za siri husababishwa zaidi na aina mbili za virusi (HPV-6 na HPV-11), na aina hizi mbili huhesabiwa kama virusi wasio na madhara makubwa kwa maana kuwa ni mara chache sana wanaweza kusababisha kansa. Aina moja ya kirusi huyu, HPV-16, anahesabaowa kama ni wa hatari na ndiye chanzo cha asilimia 50 ya kansa zote za shingo ya kizazi kwa wanawake. Aina nyingine za virusi wa hatari “high risk” ni HPV wa aina za 18, 31, 33, 35, 39, 45, 51, 52, 56, 58, 59 na 68. Saratani zote, asilimia 100, za shingo ya kizazi husababishwa na HPV.
Wadudu wanaenea kwa haraka sana kwa hupenya kupitia juu ya ngozi au kupitia sehemu laini zenye unyevu za siri wakati wa tendo la ndoa. Seli za mwili zikishashambuliwa, hupita kipindi cha miezi au miaka kadhaa bila kuonyesha dalili za kuwa kuna maambukizi.
Kwa kawaida, theluthi mbili za watu waliofanya mapenzi na mtu mwenye chunjua za sehemu za siri huota chunjua hizi.
Dalili Za Chunjua Za Sehemu Za Siri Ni Nini?
Pamoja na kuwa genital warts hazina maumivu, zinaweza kuwa kero kwa sababu ya sehemu zilizopo, ukubwa wake na miwasho. Ukubwa wa chunjua huwa kama milimeta moja mapana yake hadi sentimeta moja ya mraba endapo chunjua nyingi zitaungana. Chunjua huweza kuota sehemu zaidi ya moja.
. Kwa wanaume, genital warts huweza kutokea kwenye mrija wa mkojo, uume, au kwenye eneo la mkundu. Zinaweza kuwa kama vijinyama laini vilivyovimba visivyo na mkwaruzo (juu ya uume) au kama vijidole vinavyoning’inia (kwenye eneo la mkundu). Nyingine zinaweza kuwa na umbo la koliflawa, au zenye kukwaruza na zenye rangi nyeusi. Wakati mwingine hujificha kwenye unywele au zikawa ndani ya govi la mtu ambaye hajatahiriwa.
. Kwa wanawake, chinjua huwa na sura hiyo hiyo ila mara nyingi huwa kwenye sehemu zenye unyevu za mashavu ya ndani (labia minora) au kuzunguka tundu la kuma.
Tiba Ya Chunjua Za Sehemu Za Siri Ni Nini?
Hakuna tiba ambayo ni ya uhakika kabisa kwa chunjua za sehemu za siri. Kuna tiba nyingi zinazotumika, lakini hakuna yenye uhakika wa asilimia 100 katika kuondoa chunjua za sehemu za siri na kuzizuia zisirudie tana. Genital warts huweza kuondoka zenyewe kutoka asilima 10 hadi 20 ya watu walioathirika katika kipindi cha miezi 3 hadi 4.
. Cryotherapy: Njia hii hugandisha chunjua kwa kutumia naitrojeni ya maji (liquid nitrogen). Ni njia bora sana kwa sababu imetoa matokea mengi mazuri ikiwa na side effects chache sana.
. Laser treatment: Njia hii hutumika kwa chunjua za sehemu za siri zilizoenea au zinazojirudirudia. Mionzi ya laser huharibu kabisa uvimbe uliotokana na HPV. Dosari ni bei yake kubwa, muda mrefu wa tiba, na kuacha makovu.
. Elecrodesiccation: Njia hii hutumia peni ya umeme kuua chunjua.
Ni Zipi Dawa za Genital Warts?
Kuna dawa kadhaa zinazotumika kutibu chunjua za sehemu za siri na unaweza kuzitumia kama mbadala wa tiba nyingine.
. Podophyllum resin ni dawa inayotolewa na mtaalamu wa tiba
. Podofilox (Condylox) ni dawa unayoweza kuitumia nyumbani na ina uwezo mkubwa wa kutibu kuliko podophyllum resin. Dawa hii pia hutumika kwa kinga.
. Trichloroacetic acid au bichloroacetic acid haina uhakika sana na chunjua huweza kurudi, inaweza kusababisha maumivu na kujisikia kama unaungua.
. 5-Fluorouracil (Efudex) hutumika kama cream, huchukua muda mrefu kutibu, na ina madhara mengine mengi ya kiafya.
. Interferon alpha -n3 (Alferon N) ni sindano inayotumika kwa chunjua ambazo hazisikii dawa nyingine, lakini ina madhara mengine mengi.
. Imiquimod (Aldara) hutumika kama cream na maumivu wakati ukipaka hutokea.
Katika ukurasa mwingine tumezielezea chunjua za aina nyingine zikiwemo Common warts, flat warts, Filiform warts na Periungual Warts.
Usisite kuuliza maswali uliyo nayo au kutoa ushauri wako kuhusu mada yetu ya leo.
Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba 0655 858027 au 0756 181651.
Homa Ya Ini – Hepatitis C
Baada ya kujadili kuhusu hepatitis A na B katika kurasa zilizotangulia, leo tutaona aina nyingine ya homa ya ini, Hepatitis C. Kama ilivyo kwa hepatitis A na B, ugonjwa huu husababishwa na aina nyingine ya kirusi aitwaye Hepatitis C virus (HCV). Ni vigumu kwa kinga za mwili kuuondoa ugonjwa huu, hivyo ugonjwa huu mara nyingi huwa ni wa muda mrefu (chronic). Asilimia 85 ya watu wanaopatwa na hepatitis C, wanashindwa kuuondoa kwa kinga zao za mwili. Baada ya muda mrefu, ugonjwa huo huharibu kabisa maini na kusababisha yashindwe kabisa kufanya kazi. Kitu kibaya ni kwamba virusi hawa wakiingia mwilini, hakuna dalili zo zote za awali zitakazojitokeza.
Kirusi wa hepatitis C hana uhusiano kabisa na virusi wengine wanaosababisha homa ya ini, kama hepatitis virus A au hepatitis virus B. Kirusi wa hepatitis C anatoka kwenye familia ya virusi ya Flaviviridae. Virusi wengine kutoka kwenye familia hii ni wale wanaoleta magonjwa ya homa ya manjano na dengue.
Uwepo wa virusi wa hepatitis C mwilini huzishtua kinga za mwili zianze kufanya kazi na hivyo uvimbe hutokea. Baada ya miaka kumi, ishirini au zaidi, uvimbe huu huweza kujenga makovu (cirrhosis). Maini yakishafikia kuwa na cirrhosis, yanaweza yakashindwa kufanya kazi zake inavyopaswa, hali inayoweza kupelekea madhara makubwa na hata kifo. Na, maini yenye cirrhosis yanaweza kupata saratani kwa urahisi zaidi.
Dalili Za Hepatitis C
Asilimia 75 ya wagonjwa wa hepatitis C hawapati dalili zo zote wanapoambukizwa HCV. Asilimia 25 inayobakia wanaweza kuona dalili zifuatazo:
. uchovu
. kukosa hamu ya kula
. maumivu ya misuli
. homa
Mara chache mgonjwa ataona mabadiliko ya rangi ya ngozi au macho (kuwa njano) kwenye hatua hii.
Baada ya muda, mgonjwa ataanza kuona matokeo ya kuwa na uvimbe wa muda mrefu uliotokana na kinga za mwili kujaribu kuwaondoa virusi wa hapatitis C. Wakati cirrhosis ikijijenga, mgonjwa anaweza kuona yafuatayo:
. udhaifu wa mwili
. kukosa hamu ya kula
. kukonda
. maziwa kukua kwa wanaume (gynecomastia)
. vipele kwenye viganja
. damu kutoganda upesi ukiumia
Maini hatimaye hushindwa kuendelea kufanya kazi cirrhosis ikikomaa, hali ambayo ni hatari kwa maisha ya mgonjwa. Mgonjwa anaweza kuchanganyikiwa au kuzirai (coma) kwa vile maini yatashindwa kuondoa baaadhi ya sumu nje ya mwili.
Kuongezeka kwa msukumo wa damu kwenye mishipa ya damu ya maini (portal hypertension) kunaweza kusababisha maji kujaa ndani ya tumbo na hatimaye kupelekea kuvimba kwa veni za kwenye koromeo ambazo zitachubuka kirahisi na kusababisha damu nyingi kuvuja. Kuongezeka huku kwa msukumo wa damu kwenye mishipa ya maini kunaweza kusababisha figo kufeli au kuvimba kwa bandama.
Pamoja na kusababisha damu ishindwe kuganda kwenye majeraha, hepatitis C iliyokomaa hufanya rangi ya ngozi na macho kugeuka na kuwa njano (jaundice) kwa sababu maini hayawezi tena kuondoa mchanganyiko wa vitu vya njano (bilirubin) unaotokana na chembe chembe nyekundu za damu zilizozeeka.
Hepatitis C Inaenezwaje?
Njia kuu ya kuenea kwa hepatitis C ni kupitia damu yenye virusi wa hepatitis C:
. Kuchangia sindano baina ya watumiaji wa madawa ya kulevya
. Kuchomwa sindano na wahudumu wa afya ambazo kwa bahati mbaya hazikuwa salama
. Mtoto kupata ugonjwa huu kutoka kwa mama yake anapozaliwa
. Kujamiiana bila kutumia kinga
. Kutumia vifaa vya kutobolea ngozi visivyo salama
Tiba Ya Hepatitis C
Virusi wa hepatitis C wapo wa makundi madogo tofauti yapatayo 6 na kila kundi lina usikivu tofauti kwa aina ya tiba itakayotolewa. Hali hii huifanya tiba ya hepatitis C kuwa na changamoto kwani inatakiwa uchunguzi wa kina kufanyika ili kujua aina halisi ya kirusi aliyo nayo mgonjwa ili apewe tiba anayostahili.
Kwa miaka mingi mchanganyiko wa sindano za interferon na vidonge vya ribavirin umekuwa ukitumika. Tiba hii imekuwa na mafanikio kwa karibu asilimia 60 tu ya wagonjwa. Tiba hii pamoja na kuwa haipatikani kwenye baadhi ya nchi, watu wengi wanaopata tiba hii hawamalizi dozi.
Maendeleo ya kisayansi yamewezesha kugundulika kwa dawa mpya ambazo tayari zimepasishwa na FDA na nyingine bado zinaendelea kugunduliwa, dawa ambazo wagonjwa wanaweza kuvumilia kuzitumia. Mfano wa dawa hizi ni mchanganyiko wa Telaprevir na boceprevir, Sofosbuvir (iliyopasishwa 2013) na Ledipasvir ya 2014.
Katika ukurasa wa mwisho wa mfululizo wa mada yetu ya ugonjwa wa homa ya ini, tutajadili homa ya ini ya hepatitis D na hapatitis E.
Usisite kutuandikia ili kutoa maoni yako kuhusu mada hii, tutafurahi kupata mchango wako na kuona kuwa tumekujibu.
Kwa mawasiliano tuma ujumbe wako kupitia ukurasa huu kwa kujaza fomu hapa chini , au tuma barua pepe kwa anuani promota927@gmail.com au piga simu kwenye nambari zifuatazo: 0655 858027 au 0756 181651.
Tafadhali ungana nasi kwenye ukurasa wa facebook wa LINDA AFYA YAKO ili upate mfululizo wa mada zetu zinazohusu afya ya binadamu na jinsi ya kuanza na kufanya biashara za mtandao zinazohusu virutubisho vya mwili kwa mtaji mdogo kabisa. Tunaomba uweke LIKE kwenye ukurasa huo endapo utakuwa umependezewa na mada zetu.
Hello world!
Welcome to WordPress. This is your first post. Edit or delete it, then start writing!