Chunjua Za Sehemu Za Siri – Genital warts – Tiba Ni Nini?

 

 

 

 

 

Genital warts – chunjua zinazoota seheme za siri – husababishwa na human papillomavirus. Kuna aina tofauti zaidi ya 100 za human papillomavirus (HPV) lakini ni aina kama 40 tu ya hizi ndizo zinazoweza kusababisha chunjua za sehemu za siri. Katika mada yetu ya leo tutaona dalili za genital warts na tiba za chunjua hizi za sehemu za siri.

Chunjua za sehemu za siri husababishwa zaidi na aina mbili za virusi (HPV-6 na HPV-11), na aina hizi mbili huhesabiwa kama virusi wasio na madhara makubwa kwa maana kuwa ni mara chache sana wanaweza kusababisha kansa. Aina moja ya kirusi huyu, HPV-16, anahesabaowa kama ni wa hatari na ndiye chanzo cha asilimia 50 ya kansa zote za shingo ya kizazi kwa wanawake. Aina nyingine za virusi wa hatari “high risk” ni HPV wa aina za 18, 31, 33, 35, 39, 45, 51, 52, 56, 58, 59 na 68. Saratani zote, asilimia 100, za shingo ya kizazi husababishwa na HPV.

Wadudu wanaenea kwa haraka sana kwa hupenya kupitia juu ya ngozi au kupitia sehemu laini zenye unyevu za siri wakati wa tendo la ndoa. Seli za mwili zikishashambuliwa, hupita kipindi cha miezi au miaka kadhaa bila kuonyesha dalili za kuwa kuna maambukizi.

Kwa kawaida, theluthi mbili za watu waliofanya mapenzi na mtu mwenye chunjua za sehemu za siri huota chunjua hizi.

 

Dalili Za Chunjua Za Sehemu Za Siri Ni Nini?

 

Pamoja na kuwa genital warts hazina maumivu, zinaweza kuwa kero kwa sababu ya sehemu zilizopo, ukubwa wake na miwasho. Ukubwa wa chunjua huwa kama milimeta moja mapana yake hadi sentimeta moja ya mraba endapo chunjua nyingi zitaungana. Chunjua huweza kuota sehemu zaidi ya moja.

. Kwa wanaume, genital warts huweza kutokea kwenye mrija wa mkojo, uume, au kwenye eneo la mkundu. Zinaweza kuwa kama vijinyama laini vilivyovimba visivyo na mkwaruzo (juu ya uume) au kama vijidole vinavyoning’inia (kwenye eneo la mkundu). Nyingine zinaweza kuwa na umbo la koliflawa, au zenye kukwaruza na zenye rangi nyeusi. Wakati mwingine hujificha kwenye unywele au zikawa ndani ya govi la mtu ambaye hajatahiriwa.

 

 

. Kwa wanawake, chinjua huwa na sura hiyo hiyo ila mara nyingi huwa kwenye sehemu zenye unyevu za mashavu ya ndani (labia minora) au kuzunguka tundu la kuma.

 

 

 

Tiba Ya Chunjua Za Sehemu Za Siri Ni Nini?

 

Hakuna tiba ambayo ni ya uhakika kabisa kwa chunjua za sehemu za siri. Kuna tiba nyingi zinazotumika, lakini hakuna yenye uhakika wa asilimia 100 katika kuondoa chunjua za sehemu za siri na kuzizuia zisirudie tana. Genital warts huweza kuondoka zenyewe kutoka asilima 10 hadi 20 ya watu walioathirika katika kipindi cha miezi 3 hadi 4.

. Cryotherapy: Njia hii hugandisha chunjua kwa kutumia naitrojeni ya maji (liquid nitrogen). Ni njia bora sana kwa sababu imetoa matokea mengi mazuri ikiwa na side effects chache sana.

. Laser treatment: Njia hii hutumika kwa chunjua za sehemu za siri zilizoenea au zinazojirudirudia. Mionzi ya laser huharibu kabisa uvimbe  uliotokana na HPV. Dosari ni bei yake kubwa, muda mrefu wa tiba, na kuacha makovu.

 

. Elecrodesiccation: Njia hii hutumia peni ya umeme kuua chunjua.

 

 

 

 

Ni Zipi Dawa za Genital Warts?

 

Kuna dawa kadhaa zinazotumika kutibu chunjua za sehemu za siri na unaweza kuzitumia kama mbadala wa tiba nyingine.

. Podophyllum resin ni dawa inayotolewa na mtaalamu wa tiba
. Podofilox (Condylox) ni dawa unayoweza kuitumia nyumbani na ina uwezo mkubwa wa kutibu kuliko podophyllum resin. Dawa hii pia hutumika kwa kinga.
. Trichloroacetic acid au bichloroacetic acid haina uhakika sana na chunjua huweza kurudi, inaweza kusababisha maumivu na kujisikia kama unaungua.
. 5-Fluorouracil (Efudex) hutumika kama cream, huchukua muda mrefu kutibu, na ina madhara mengine mengi ya kiafya.
. Interferon alpha -n3 (Alferon N) ni sindano inayotumika kwa chunjua ambazo hazisikii dawa nyingine, lakini ina madhara mengine mengi.
. Imiquimod (Aldara) hutumika kama cream na maumivu wakati ukipaka hutokea.

 

Katika ukurasa mwingine tumezielezea chunjua za aina nyingine zikiwemo Common warts, flat warts, Filiform warts na Periungual Warts.

 

Usisite kuuliza maswali uliyo nayo au kutoa ushauri wako kuhusu mada yetu ya leo.

 

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba 0655 858027 au 0756 181651.

15 thoughts on “Chunjua Za Sehemu Za Siri – Genital warts – Tiba Ni Nini?”

  1. Nahisi ninalotatizo hili ila sikuweza kugundua kwa haraka,ila zakwangu zimenitokea pembezoni mwa sehemu yakutolea mkojo,mwanzoni nilikuwa najua ni fangasi sababu nilikuwa nawashwa sana,ila leo baada ya kusoma hii makala ndo nimegundua ni nini,kwa sasa Mimi ni mjamzito na nimesikia vinaweza kusababisha nikakosa mtoto,sijui mnanishauri nifanyaje naogopa sana

    1. Kutopata mtoto n uvumi ulioenea sana, alkini kitaalamu sijawi kuona imeandikwa hivyo. Nakushauri uzae kwanza ndipo uanze tiba. Huna haja ya kuogopa sana.

  2. Mimi pia ninalo hili tatzo na kama wiki mbili ila mm kwenye sehemu za zimetokea nyama nyeusi nawashwa sana pia naomba kuuliza ukifanya mapenzi na mtu ambae ana hili tatz naweza kumuambukiza

    1. Kusudi kuwa na uhakika tunashauri uende hospitali. Ugonjwa huu huambukiza kwa kujamiiana, kwa ye yote yule akijamiiana na mtu mwenye chunjua, naye ataambukizwa. Karibu sana.

    1. Kama upo Dar tunaomba uje ofisini, Machinga Complex. Kama ni nje ya Dar, utatumiwa dawa kwa bus. Tuwasiliane kupitia 0655 858027 au 0756 181651. Karibu sana.

  3. Mimi pia nina tatizo hilo ila nimetumia dawa inaitwa caustic pencil ila bado kma zinarudi tena nitumie dawa gani nyingine ambayo itanisaidia zisirudi?

      1. hivi tabibu ni kweli mtu akipatwa na chunjuwa basi taari atakua na maambukizi ya HIV ?niliwah skia doctor mmoja hivi kuzungumza kua hajawah ona mgonjw wa chunjuwa akawa amekosa maambukiz ya HIV je ni kweli hii

      2. Mimi vimenitokea kwenye ume wangu sehem mkojo unapotokea vinatokeza nje nisaidie nitumie dawa ipi ya hospital au ya asiri

  4. Me pia vinanisumbua hvyo vdude, , ni vichache na vdogo vdogo sana lakn vinanikera, , , nimeenda pharmacy nmepewa skderm cream bdo cjaitumia, , , je inafaa?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *